Tusaidiane kuhusu mapenzi na chuki kwa Kikwete na CCM yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusaidiane kuhusu mapenzi na chuki kwa Kikwete na CCM yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Oct 12, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  umekuwa na hisia hata minyukano baina ya wapenzi na wapinzani wa Kikwete na CCM yake. Wapinzani wanajitahidi kumshauri huku wapenzi wake wakijitahidi kuonyesha kuwa kufanya hivyo ni kumchukia huku wapinzani wakisema ni kumpenda. Je wewe kama mwana JF unalionaje hili?

  Mfano, Kikwete ameshauriwa na wapinzani aache kukwepa matatizo na kukimbilia nje huku mashabiki zake wakisema safari zake za kuombaomba ni neema kwa taifa. Kikwete ameshauriwa kuachana na style yake ya kutawala kwa kutumia autopilot huku watu wake wakisema anachofanya ni uungwana. Kikwete ameshauriwa abadili kauli mbinu yake ya maisha bora kwa watu ambayo yametafsiriwa na wapinzani kama maisha bora kwa wote walio wake na chama chake.

  Kikwete ameshauriwa aachane na mitandao ya kifisadi na kuwahudumia wananchi. Wapinzani wake wanasema muda unamwacha mkono.

  Je wewe unasemaje? Ni mapenzi au chuki hata umbea au uzalendo?
   
 2. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hakuna Rais anaweza kufuata kila neno la mwanasiasa. Hakuna Mwanasiasa yeyote duniani anayemtakia mema mpinzani wake, hivyo atajitahidi kupiga propaganga ili aliyeko madarakani aonekane hafai. Njia pekee ya kuwakomesha wanasiasa wa aina hiyo kwa kiongozi kutokuwa na papara ya kuharakisha kuongelea jambo la wanasiasa, na hili ndilo analolifanya Rais KIKWETE. Maneno kama "RAIS ANAKIMBIA MATATIZO", RAIS ANATAWALA KWA STYLE YA..", RAIS ANA MITANDAO YA KIFISADI" ni maneno mepesi sana tena yanayotolewa na wanasiasa ambao hawajakomaa kisiasa na wanaosukumwa kusema hivyo na uwezo mdogo wa wananchi kuchambua mchele na pumba za wanasiasa.
   
 3. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa nangatuka ni kweli kabisa unalosema. Je na hii hali mbaya ya maisha iliyopo mitaani unailinganishaje na hii mada. Hakuna ajira kwa vijana, ufisadi uliokithiri hata matrilioni yamefichwa nje ya nchi, deni kubwa la taifa linalokuwa siku hadi siku, wanyama wanatoroshwa kila siku, ofisi za serikali zimekuwa ni nyumba za ufisadi. Tuishie tu na rushwa ya waziwazi hata kwenye uchaguzi wa CCM imeonekana wazi na hakuna hata aliyekemea. Na haya je ni maneno au wamesababisha wapinzani?
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mimi sioni mapenzi au chuki zinachochote kwake...kwa sababu ndogo tu, hana uwezo wa kazi aliyomo. umpende umchukie havisaidii chochote. labda umsaidie kwa kumtoa umpumzishe na zigo asiloliweza
   
 5. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe asilimia fulani,swali unafikiri anaongoza vizuri au unaionaje hali ya nchi na wananchi kiuchumi kabla yake?
   
 6. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kaka sio kila jicho lina lensi inayoona.
   
 7. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  you are right 100%. kwa case ya rais wetu matatizo yapo hayapo? hata adui yako anaweza kukuonya, japo angefurahia anguko lako-sembuse mwanasiasa mwenzio. kama wanakuambia ukweli na wewe hufuati tu kwa sababu ni wapinzani wako, yakikupata utasemaje? wamekuloga au? usipuuzie au kuchelewa kutake action ya jambo fulani eti kwa kuwa aliyesema si mwenzio, sio rafiki au ndugu au mwanachama mwenzio. hata hao wa karibu yako wanaweza kukutosa vilevile, kwani mioyo yao unaiona!
   
Loading...