Tusaidiane hapa tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,564
Hivi ' logically ' tu Chombo cha Habari kikubwa na tegemezi nchini Tanzania kuamua kwenda kuwahoji Watoto wa Shule za Msingi tena wa Darasa la Nne na Darasa la Pili juu ya ' Utendaji ' wa ' Mtawala ' fulani kwa miaka yake minne gawanya kwa miwili ni sahihi na lina tija hasa Kimantiki?

Hivi kama kweli wanataka kupata ' mrejesho ' wa Kutukuka wa Uongozi wake wa miaka minne gawanya kwa miwili wa huyo ' Mtawala ' kwanini tu wasingeenda kuwahoji Watu ambao Kiuhalisia kabisa wapo ' matured ' enough na wa kutoka nyanja mbalimbali za Kitaaluma ili waweze kutoa yao ya moyoni?

Hivi nyie Chombo Kikubwa cha Habari na tegemezi nchini Tanzania mnapata faida gani kwa kuwafanya Watanzania wote ni Mangumbaru na Mapopoma? Yaani kabisa Mwandishi wa Habari uliyepikwa Chuoni unaacha kwenda kuhoji Watu wazima na wenye akili zao na unaamua kwenda kuwahoji Wanafunzi wa Darasa la Nne na la Pili ili wakupe ' tathmini ' yao juu ya Uongozi wa miaka minne gawanya kwa miwili ya ' Mtawala ' fulani?

Ni nani ' aliyeturoga ' vibaya hivi Sisi Watanzania ili kama vipi nimtafute na nikamuombe radhi / msahama ili ' atugomboe ' na tusiwe tena Wajinga na Wapumbavu kama tulivyo sasa? Endeleeni kumdanganya ila on the ground hali ni mbaya sana na sivyo kama hivyo mnavyodhani. Naisubiri kwa hamu mno 2020 kwani nahisi kuna ' maajabu ' makubwa yanaweza kutokea nchini Tanzania kama ' haki ' itatendeka na hakutokuwa na ' Ngendembwe / Hila / Figisufigisu '. Yangu macho!

Nawasilisha.
 
Halafu wakiwahoji wanakuja na habari wanafunzi watanzania waipongeza sana Serikali kwa kuwatengezea madawati wakati madawati tulichangishwa sisi wazazi

Kuna vitu vinaudhi na vinakera sana Mkuu. Hasira zimenipanda tayari ngoja tu ni log out nitarudi tena Saa 4 Kamili usiku labda ' Hasira ' hizi zinaweza zikawa zimepungua / zimeisha.
 
jana usiku walizima mitambo ili kuongeza ubora wa matangazo, sijui umeboreka? mnao angali mtujuze sisi ambao hatuna hata tv
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom