PAC yashtushwa na mtaji wa 150,000 wa mwekezaji Mlimani City

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,507

milimanicity-ad.jpg
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati hiyo pia imeelezwa kuwa mwekezaji katika mradi wa uwekezaji wa Mlimani City alikuja na mtaji wa Dola za Marekani 75 (Sh 150,000) kuwekeza katika mradi huo.

Kamati hiyo ambayo iko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali pia imebaini madudu katika mradi huo na kuagiza wote waliosaini mkataba huo waitwe na kuhojiwa.

Aidha, kamati hiyo imeshangazwa na hatua hiyio na kuhoji taaaisi kubwa kama ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) inayoaminika ndani na nje ya nchi ilishindwaje kukopa fedha za kuendesha mradi huo hadi kukubali mwekezaji wa aina hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka, amesema kuna vitu vingi vimejificha katika mkataba huo hivyo ni lazima kuwe na watu watakaowajibika.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amekiri mkataba huo kuwa na matatizo hivyo wanachukua hatua kuyatatua.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala, Profesa David Mfinanga, amesema wameunda kamati kupitia upya mkataba huo.

Chanzo: Mtanzania
 
Kuna thrd iliwahi kuletwa hapa ikieleza UD kuwa kitovu cha graduate wapuuzi. Wanajiita ni wakongwe. Ni Wezi, wala rushwa, nk. Bahati mbaya awamu hii rais anaiona UD kama hazina ya kupata watendaji wake serikalini. Hapo ndo tunatoa wanasheria wakongwe wanajidai kutusaidia kueleza historia ya sheria na mazagazaga yao. Walikuwa wapi wakati wa mkataba huu?

Wamuulize Luhanga na Mukandara. Hawa ni ma-Prof. Wawili ambao walifyonza mradi huu.
Prof. Mkandara nadhani alijaa skandari na sijui kwa nini aliachwa mpaka kaifanya UD kuwa kama sekondari.
 
muwekezaji%2Bpic.jpg

Namuona hapo Lusinde akiwa ameshika lisimu likubwa ndani ya Kamati ya Hesabu za Serikali PAC.Dah.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.

Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.
Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.

"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"
Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana) , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.

Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.

"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.
Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.

Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.
"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.

Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.

Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha
 
Wasomi wetu hawajawahi kuisaidia nchi hii kila anayepewa nafasi anaiba kadiri awezavyo kuanzia raisi hadi vijitaasisi, na mambo makuu kwao ni kujenga nyumba, kununua gari na kuanzisha vijimiradi nakuiacha taasisi nyingi za umma zikifilisika au kurudi nyuma..."wakati mwingine bora bashite"

Nafikiri nimuhimu sana tukiangalia namna bora mitaala yetu itakavyo badilishwa nakutuandalia wasomi wafia nchi. Ila bado kila ninapowaza juu ya elimu namwona mwalimu aliye na maslahi duni kubebeshwa jukumu la kuandaa taifa bora
 
Mwekezaji huyo mwenye mtaji wa 150,000 ametoka nchi gani? Au usikute mwekezaji mwenyewe ni mmoja wa viongozi wa chuo au mwanasiasa flani kawatumia kijanja! Yaleyale ya TRL ya wahindi.
 
View attachment 678879
Namuona hapo Lusinde akiwa ameshika lisimu likubwa ndani ya Kamati ya Hesabu za Serikali PAC.Dah.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.

Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.
Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.

"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"
Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana) , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.

Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.

"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.
Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.

Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.
"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.

Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.

Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha
Tumeingia kwenye majanga ya mikataba mibovu kutokana na watendaji wetu kushindwa kupitia mikataba kifungu kwa kifungu, na kazi mojawapo ya PAC ni kuangalia kasoro kama hizi. Sasa Mtu kama LUSINDE aliyeishia Darasa la saba la kuungaunga anajua kitu gani kuhusu mikataba tena ambayo ndani yake kuna mahesabu?. Aidha mikataba mingi inaandikwa kwa lugha ya malikia, Magu mwenyewe ambaye inadaiwa ni PhD holder kiingereza kinampiga chenga sasa ndiyo itakuwa huyu aliyeishia Darasa la saba? Hii Nchi ina vituko!
 
View attachment 678857 Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati hiyo pia imeelezwa kuwa mwekezaji katika mradi wa uwekezaji wa Mlimani City alikuja na mtaji wa Dola za Marekani 75 (Sh 150,000) kuwekeza katika mradi huo.

Kamati hiyo ambayo iko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali pia imebaini madudu katika mradi huo na kuagiza wote waliosaini mkataba huo waitwe na kuhojiwa.

Aidha, kamati hiyo imeshangazwa na hatua hiyio na kuhoji taaaisi kubwa kama ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) inayoaminika ndani na nje ya nchi ilishindwaje kukopa fedha za kuendesha mradi huo hadi kukubali mwekezaji wa aina hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka, amesema kuna vitu vingi vimejificha katika mkataba huo hivyo ni lazima kuwe na watu watakaowajibika.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amekiri mkataba huo kuwa na matatizo hivyo wanachukua hatua kuyatatua.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala, Profesa David Mfinanga, amesema wameunda kamati kupitia upya mkataba huo.

Chanzo: Mtanzania
Mwanaccm Mukandara yuko wapi ? Huyu anajua kila kitu
 
It doesn't sound right... ngoja nipitie makarabrasha yangu!!

But all in all, issue ni kwamba alikuja na shilingi ngapi au issue mtaji alitoa wapi?! Hata kama alikuja na shilingi 10 lakini project yake ilionekana viable investments kwa investors/financial banks na hivyo wakaamua ku-finance hiyo project; sasa tatizo lipo wapi?!

Core issue ya Mlimani City haiwezi kuwa Mwekezaji alikuja na dola ngapi bali ikiwa kama mkataba wenyewe ni wa kifisadi au hapana! Na huo ufisadi haukutokana na Mwekezaji kuja na laki unusu bali hulka yetu ya wizi.

Kwa mfano, sikuona sababu ya msingi kwanini UDSM na usomi wao wote ule bado walikubali ku-lease kwa miaka 50 kwa prime are kama ile.

Matokeo yake, original investor alifanya biashara kwa miaka takribani 5 tu, akapiga bei, na hivyo kuonesha tayari alisharudisha gharama... at least, kwa kuongeza na pesa aliyouzia tayari ingemwachia faida ya kutosha!!
 
Back
Top Bottom