Turudisheni kwenye chama kimoja

togo

Member
Nov 8, 2010
40
1
kutokana na hali ya kisiasa nchini mimi naona ni bora tukirudi kwenye chama kimoja ,kwanza 20% tu ndio walitaka vyama vingi the rest hawakutaka.kwanza nani kasema demokrasia lazima iwe ya vyama vingi kama sio propaganda za wazungu,vyama vingi vinagawa watu badala ya kuwaunganisha ,vinawagawa katika misingi ya dini,rangi,ukanda ,ukabila.
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Toa mapendekezo:

Chama kipi?

Akili yako ni sawa na abiria wa daladala anayeishi Segerea anayetembea kutoka Posta hadi Karume kuvizia daladala yenye siti. Akikutana na daladala la kwenda kwao linaloelekea Posta anapanda, anarudishwa nyuma alikotoka, anatozwa nauli mara mbili.

Ukiamua kwenda mbele, nenda mbele.
 
togo

Member
Nov 8, 2010
40
1
mbona mwalimu nyerere aliweza kuvipiga marufuku hata leo hii hiyo inawezekana kwa sababu wanasiasa wa afrika hawapo kwa ajili ya watu wapo kwa maslahi yao tu,JK akiwa rais,Lipumba makamu wa rais,Slaa waziri mkuu,wakaamua kujipa mishahara minono na wakapitisha azimio la kuwa na chama kimoja hakuna wa kuwazuia ni mfano tu ambao umetokea zanzibar kwani kuna Cuf tena kule njaa na uroho wa madaraka ya wanasiasa ndio umeleta vyama vingi,
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,957
4,623
kutokana na hali ya kisiasa nchini mimi naona ni bora tukirudi kwenye chama kimoja ,kwanza 20% tu ndio walitaka vyama vingi the rest hawakutaka.kwanza nani kasema demokrasia lazima iwe ya vyama vingi kama sio propaganda za wazungu,vyama vingi vinagawa watu badala ya kuwaunganisha ,vinawagawa katika misingi ya dini,rangi,ukanda ,ukabila.

Da! jamaa unaturudisha mwaka 1991!
so tubaki na CCM tu?
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
tunaweza kuunda chama kipya ila kimoja mi naunga mkono hoja na huu ubabe wa ccm bora chama kimoja!
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
mbona mwalimu nyerere aliweza kuvipiga marufuku hata leo hii hiyo inawezekana kwa sababu wanasiasa wa afrika hawapo kwa ajili ya watu wapo kwa maslahi yao tu,JK akiwa rais,Lipumba makamu wa rais,Slaa waziri mkuu,wakaamua kujipa mishahara minono na wakapitisha azimio la kuwa na chama kimoja hakuna wa kuwazuia ni mfano tu ambao umetokea zanzibar kwani kuna Cuf tena kule njaa na uroho wa madaraka ya wanasiasa ndio umeleta vyama vingi,
naunga mkono hoja mkuu na zanzibar TAYALI WANACHAMA KIMOJA BADO BARA TUU!
 
Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
308
Naunga mkono hoja 100%.

Kama hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi ni heri turudi tuwe na chama kimoja na iwe hakuna kupiga kura ni kupokezana tu kama ufalme vile!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom