Turudi nyuma nani alimteka Nondo? Je serikali inahusika?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Abdul Nondo amewahi kutekwa na watu wasio julikana,kwa upande wa serikali na wapambe wao na uchunguzi wao hadi kwenye simu na minara wakaja na hoja kuwa Nondo alijiteka mwenyewe

Yaani chombo cha polisi na usalama wa Taifa wakaaminisha Watanzania kuwa Nondo kajiteka mwenyewe,bila kusahau kauli nzito kutoka Lumumba za kejeli na dharau dhidi ya Nondo kuwa amejiteka mwenyewe

Mpaka kuna lugha ngumu imewahi kutolewa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Mwigulu kwa Abdul Nondo

Nondo kapelekwa mahakamani,pamoja na ushahidi wenye utata mahakamani umemuachia huru mara mbili kuwa Nondo hana hatia

Sasa turudi nyuma Nondo alijiteka au alitekwa?

Vyombo vya serikali kwa makusudi viliwahadaa Watanzania kuwa Nondo alijiteka kumbe wenyewe ndo watekaji?

Wewe kama mtanzania una bado imani na vyombo vya usalama Tanzania ?

IGP Sirro tuambieni nani anahusika na utekaji Tanzania? Intelligensia ya polisi imeshindwa kubaini waliomteka Nondo wakaja na majibu kuwa alijiteka?

Watanzania bado tunajiuliza ni nani alimteka Nondo,

Mwigulu,Lugora na IGP tunasubiri majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_4043.JPG
 
Jibu ni amejiteka, ni mahakama tu inakataa kutoa ushirikiano....ndio maana huwa tunatamani Mr Kazi angekuwa Mkuu wa huu muhumili pia.
 
Back
Top Bottom