Turudi kwenye akili zetu na tutambue kilicho muhimu kwa taifa letu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Moja ya skill ya uongozi ambayo kiuongozi mzuri anapaswa kuwa nayo ni kusimamia agenda mpaka anaona mwisho wake, lakini pili kuifanya hiyo agenda iwe ya wananchi wenyewe kwakuwa wao ndio wajenga nchi agenda isipokuwa ya wananchi hakuna kiongozi atakayeifanikisha.

Ifanye agenda yako iwe ya wananchi wakabidhi nao wataifanikisha, kazi ya viongozi ni kuratibu tu na kuonyesha njia.

Na hapa ndipo huwa inaonekana tofauti kati ya viongozi na mameneja.
Nguvu ya ushawishi ni muhimu katika kulenga watu kufanikisha kile ambacho kiongozi anataka kufanikisha pasipo kutumia nguvu ama kutumia nguvu kidogo.

Nguvu kubwa ya mabadiliko iko kwa wananchi wenyewe. Lakini imelala haiko motivated vya kutosha kujenga taifa lao kwa kuwa agenda halisi ya taifa lao haijajulikana na nchi imekaa kibinafsi.

Kama taifa Kuna kitu lazima kiwepo ambacho kimetuweka pamoja kitu Hiko ndicho Kinacho to motivate kusonga mbele sio pekee maendeleo yetu binafsi bali pia hamu ya kuona taifa letu likiendelea na kuheshimiwa kutokana na mafanikio yake na maadili ya watu wake.

Taifa hili haliwezi kudumu kwa kipindi kirefu pasipo maadili. Ndio msingi wa kwanza wa ujenzi wa taifa lolote kwasababu ndio yanayotuunganisha kama taifa na kutufanya binadamu wanaofikiri. Kinyume cha hapo ni fujo na disorder katika taifa.

Maadili ndio yatakayo nifanya nikuone kama ndugu katika taifa na kunifanya nihofie kukudhuru na niwe tayari kukulinda kwasababu tunachangia taifa.

Yatatusaidia kutambua haki za wengine na kuzilinda. Kulinda familia zetu na kuziheshimu na kujenga jamii zenye amani na mashirikiano mema.

Maadili yanaposhuka mfumo mzima wa kijamii na hata wa kiserikali uharibika. Leo tunazungumza kuhusu corruption lakini hatuangalii chanzo chake huko chini kwenye maadili ya jamii ndani ya familia na katika jamii. Tunachoona hapa ni framework inayofanya kazi pamoja, huku chini pakiharibika tusitegemee juu patakuwa salama the whole framework itaharibika.

Tunaambiwa katika sheria za Mungu mpende jirani yako kama unavyopenda nafsi yako, kama hii sheria ingekuwepo miongoni mwetu na kwenye mioyo yetu hakuna mtu ambaye angemuuzia mwenzake madawa ya kulevya katika mitaa yetu.

This care and love toward our fellow human beings, that is what we need in our country.

Kwahiyo tumesahahu wajibu huu wa kimsingi tunadhani tutajenga nchi yeyote ya Maana.

Hatutajenga nchi ya maana kama hatuna watu wanao behave well ambao wanaweza kupewa majukumu wakaaminiwa na kuyatimiza ipasavyo bila manung'uniko na bila ubinafsi bila kuangalia pesa kwanza bali interest za taifa kwanza.

Wajibu huu wa kimsingi hatupaswi kuusahau.

Sehemu ambayo hakuna upendo huwezi kukuta furaha. Tunahitaji kuona haki katika nchi hii ikitamalaki na watu wetu wakiheshimiana.

Hakuna sababu ya kugombana taifa hili litafanya kazi vyema tukipatana na kuangaliana kama ndugu ambao tuna majukumu ya pamoja.

Turudi kwenye akili zetu na tutambue kilicho muhimu kwa taifa letu na tuweke mbele. Hili taifa ni zaidi ya tuliopo Leo. Ni wajibu wetu kutengeneza mazingira bora kwa wanaokuja.

Na hili iwe ubinafsi kwenye familia au katika ngazi ya taifa.

Kinachobomoa taifa hili ni ubinafsi wetu tunaweza kufanya Mambo makubwa sana kama tutajitoa pasipo ubinafsi kulijenga taifa hili. Tubadilike.

Tutakaporudi kwenye akili zetu na kujua kilicho bora na muhimu kwa taifa letu na kujua mambo ambayo hayana tija kwa taifa letu na kuachana nayo tutaendelea.

Bila maadili hatutaweza kujenga taifa lolote la Maana. Kama tunataka kuendelea ni lazima tujenge maadili ya taifa. Watu wetu wawe responsible kwa matendo yao na hata maneno yao. Kuna vitu ambavyo tunapaswa kuvibadili vya kimsingi kwenye familia zetu na jamii zetu kwa ujumla.

Uasherati, uzinzi, ulevi wa kupindukia vitu hivi kwa namna moja ama nyingine vinaturudisha nyuma. Na wajibu wetu ni kumtengeneza raia mwema na decent katika taifa lake na katika familia yake. Mtu ambaye anawajibika ipasavyo kwake binafsi na jamii inayomzunguka.

Nidhamu hii ni muhimu na ya kimsingi katika taifa letu. Na ndio msingi wa taifa lolote imara.

Tukisahau maadili tukadhani hayana Maana katika ujenzi wa taifa, matokeo yake huwa hayajifichi tuwe tayari kwa kitakachotokea tutalia lakini hakuna atakayetusikiliza kwakuwa tulisahau kujenga msingi .
 
Back
Top Bottom