Turudi enzi za kampeni na tuangalie hotuba ya rais ya mwisho wa mwezi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Turudi enzi za kampeni na tuangalie hotuba ya rais ya mwisho wa mwezi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Manyanza, Mar 3, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi na vyama mbalimbali vilitoa sera na ahadi zake kwa wapiga kura... kwa mapenzi ya NEC na TISS, CCM wakarudi Ikulu pamoja na kutumia nguvu ya pesa na mambo mbalimbali yaliyokiuka sheria ya gharama za uchaguzi. lakini ishu ilikuwa kwa rais kutoa ahadi ambazo watu walikuwa na mashaka nazo kama anaweza kuzitekeleza ukizingatia zile za mwaka 2005 hakufikia hata robo ya utekelezaji.
  Nimeshituka sana juzi nilipokuwa naisoma hotuba yake ya mwisho, hasa sehemu niliyo nukuu hapo chini

  Ndugu Zangu;
  Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. *Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. *Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. *Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. *Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo. *Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. *Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama


  inavyoonekana kwa kauli ya kikwete keshashindwa kuongoza na kuwaletea maendeleo wananchi wake... uungwana ni vitendo bora aonyeshe uungwana wake kwa kuachia kiti ili na wengine wakikalie kuliko kuendelea kujikaza huku uwezo wa kufikiri umefika mwisho na ukiangalia maandamano ya CDM yanampa presha.... yeye pamoja na mawazir wake (WASILLA + SIMBA SOFIA)
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uliyosema ni kweli tupu amepatwa na woga na mstuko baada ya kupewa taarifa na tiss/kuona maandamano yanavyopokelewa na raia, Huyo JK alisema tusichague "vyama vya msimu", vinakuja wakati wa uvhaguzi tu, leo CDM wameamua kufanya kazi(kama alivyo ahidi DR kuwa asiposhinda atatembea nchi nzima kuhamasisha) Yuleyule JK anasema wasubiri uchaguzi ujao, huyu rais wetu kweli ni MAHOKA!!!!!!!!
   
Loading...