TURKANA: Mwanafunzi aliyefukuzwa shule alipiza kisasi kwa kuwaua wanafunzi 5 na mlinzi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
sko.jpg


Wanafunzi watano na mlinzi mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi ya Leo asubuhi katika Shule ya Sekondari ya mchanganyko ya Lokichogio huko kaunti ya Turkana

Akithibitisha tukio hilo, Kamishna wa Kaunti ya Turkana Seif Matata amesema mmoja wa wauaji ni mwanafunzi aliyekuwa amesimamamishwa masomo shuleni hapo kutokana na utovu wa nidhamu

Wanafunzi kadhaa pia walijeruhiwa ambao idadi yake Kamishana hakuitaja na kusema hadi atakapowasiliana na hospitali

Mwanafunzi huyo ajulikanaye kwa jina la Abrahamu na ametokea kabila la Toposa huko Sudan Kusini na alisimamishwa masomo kutokana na utovu wa nidhamu.

Mwanafunzi huyo alisikika akisema atakuja kuichoma shule moto kulipiza kisasi cha kufukuzwa
Wanafunzi watatu wa kidato cha pili waliuawa kwenye darasa ambalo walikuwa wakilitumia kulala.

Mwanafunzi huyo akiambatana na wengine watatu alikuja asubuhi na kumuua mlinzi kisha kuelekea kwenye bweni la wavulana ambako ndipo walifikiri wanafunzi waliomsababishia kufukuzwa walikuwa wakilala kisha kuhamia bweni la wasichana na kuwajeruhi wengine kadhaa

Polisi bado wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo

==================================================
Five students and a night guard were shot dead early Saturday morning at Lokichogio Mixed Secondary School in Turkana County.

Confirming the incident, Turkana County Commissioner Seif Matata said one of the attackers was a student at the school who was on suspension.

3.30AM

The attack, according to Mr Matata, occurred between 3:30am and 4am.

"Several students were injured. We cannot confirm the number until we liaise with the hospital," Mr Matata told journalists in Lodwar town before leaving for the school, which is about 200 kilometres from the Kenya-South Sudan border.

The student was only identified as Abraham and, according to Mr Matata, he is from the Toposa tribe of South Sudan.
Form Two class where three out of the six students were killed as they slept. The class acts as a dorm for some students.
"The preliminary information we have is that this attack was carried out by a student of the school in the company of other unknown people,” he said.

“There was a student who comes from South Sudan and he was suspended from school because of indiscipline."

The student is said to have issued threats to his teachers and students after he was kicked out of school.

GIRLS

"He was heard telling fellow students that he is going to burn the school or he will come back and avenge because of the suspension,” the county chief said.

“Now what we are told is that early this morning he came with about three other people and killed the watchman. (They) proceeded to the boys' dormitory where they targeted particular students whom they thought were behind his suspension."

The administrator said the gunmen shot the targeted students before moving to the girls' dormitory where they injured several others.

"So we are appealing to everybody to remain calm while the police do the investigation and apprehend the culprits," said Mr Matata.


Source: Daily Nation
 
duu kuna watu wana hasira na akili ndogo mpaka unaogopa yaani kufukuzwa una mpereka mtu kwa muumba.
 
Watu waliotoka kwenye maeneo au mataifa yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe wana roho mbaya sana Sudan Somalia Middle East etc kuua kwao ni kama kuchinja kuku. RIP watoto mliopoteza maisha Mungu awapokee kwenye a Uzima wake wa Milele.
 
Hilo eneo nihatari sana
unakuta mwanamke na watoto wake wanao fuatana umli kama njiwa wakitembea kila mtu na AK47!
Kila jamii inamiliki Bunduki tena sio ya mchezo mchezo!
 
Back
Top Bottom