Turejee kwenye Utumishi wa kuzingatia miundo ya Utumishi na Nyaraka zake

Mizega

Senior Member
Feb 10, 2021
143
303
Utumishi wa Umma unaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya 2002, Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003, Sera ya Menejimenti ya ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 1999 pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009.

Nyaraka hizi muhimu zinaweka umbile la utumishi wa umma unaotofautisha kada moja na nyingine kulingana na elimu ya mtu, hali kadhalika nyaraka hizi zimezaa Muundo wa Utumishi wa Umma unaoweka viwango vya elimu na ubora pamoja na maslahi ya kila kada na upandaji wa daraja moja kwenda jingine ili kuandaa watumishi waandamizi ndani ya taasisi na muundo wa taasisi husika ambao wakiwa waandamizi watakuwa na sifa ya kushika nafasi za madaraka ndani ya kada na taasisi husika.

Kwa miaka mitano mfululizo nyaraka hizo zimekanyagwa na matokeo yake viongozi wengi walioteuliwa walipewa nafasi nje ya miundo na kada zao. Mfano, Mwalimu wa Michezo anapewa U DAS kazi ambayo ni ya muundo, Katibu wa Tawi Chama anapewa ukurugenzi wa Halmashauri kazi ambayo ina muundo wake na Sheria zake zimeweka bayana.

Ni muda mwafaka sasa kuurejesha utumishi wa umma katika mstari wake kulinda hadhi ya utumishi na kupandisha watumishi madaraja ili kuandaa viongozi waandamizi ndani ya miundo yao na taasisi zao.
Ya nyuma yanashangaza.
 
Mwendazake alikua ni wa hovyo hovyo..hakujari weredì na miundo katika utumishi..natumai sasa tutarejea kwenye mstari sahihi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naunga mkono hoja! Wakati wa kuichezea nchi umeshapita. Turudi kwenye misingi sahihi.

Kama una kimada wako, mfungulie genge au duka la nguo auze! Siyo kumpa zawadi ya Ukurugenzi wa Halmashauri, Ukuu wa Wilaya au Udas!
 
Mtu anaingia kazini kwa cheo cha U DAS, yaan anaanza kazi na u DAS au anaanza na ukurugenzi moja kwa moja kutoka kitaa, hana uzoefu wala hajui hili wala lile matokeo yake ni utumishi usio na tija
 
Utumishi wa Umma unaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya 2002, Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003, Sera ya Menejimenti ya ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 1999 pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009.

Nyaraka hizi muhimu zinaweka umbile la utumishi wa umma unaotofautisha kada moja na nyingine kulingana na elimu ya mtu, hali kadhalika nyaraka hizi zimezaa Muundo wa Utumishi wa Umma unaoweka viwango vya elimu na ubora pamoja na maslahi ya kila kada na upandaji wa daraja moja kwenda jingine ili kuandaa watumishi waandamizi ndani ya taasisi na muundo wa taasisi husika ambao wakiwa waandamizi watakuwa na sifa ya kushika nafasi za madaraka ndani ya kada na taasisi husika.

Kwa miaka mitano mfululizo nyaraka hizo zimekanyagwa na matokeo yake viongozi wengi walioteuliwa walipewa nafasi nje ya miundo na kada zao. Mfano, Mwalimu wa Michezo anapewa U DAS kazi ambayo ni ya muundo, Katibu wa Tawi Chama anapewa ukurugenzi wa Halmashauri kazi ambayo ina muundo wake na Sheria zake zimeweka bayana.

Ni muda mwafaka sasa kuurejesha utumishi wa umma katika mstari wake kulinda hadhi ya utumishi na kupandisha watumishi madaraja ili kuandaa viongozi waandamizi ndani ya miundo yao na taasisi zao.
Ya nyuma yanashangaza.
Wachumba na mirupo ilitesa kwa zamu aisee
 
Back
Top Bottom