Tupunguze Idadi ya Wabunge ili Tusomeshe Watoto Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupunguze Idadi ya Wabunge ili Tusomeshe Watoto Wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kubwajinga, Jan 28, 2010.

 1. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tupunguze Idadi ya Wabunge ili Tusomeshe Watoto Wetu.

  [​IMG][​IMG]  Juzi nilisoma tamko la kushangaza na kusikitisha kwenye gazeti la Mwananchi lililotolewa na Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Omar Makungu, kuwa wana mpango wa kuongeza idadi ya wabunge ili kuondoa misuguano ndani ya vyama vya siasa.


  Yaliyotamkwa;
  1. Inasemekana kuwa Dar es salaam itaongezewa wabunge na kuwa na jumla ya wabunge 17.
  2. Kisa kimojawapo kilichotajwa cha kuongeza wabunge eti ni kuwa, kuna baadhi ya wanene kwenye serikali ya JK ambao wanataka kugombea ubunge kwenye majimbo ambayo tayari yana wabunge wenzao wa CCM na hivyo italeta vurugu.
  3. Vigezo vilivyotajwa kutumika kuongeza wabunge ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa Jengo la Bunge kuwa bado lina nafasi ya viti 23, kama vile ni lazima ukumbi uliojengwa na wachina lazima ujazwe.
  Swali ;
  1. Je, hivi kweli tunahitaji kuongeza idadi ya wabunge na hivyo kuongeza gharama kwa nchi au kuwapunguza wabunge ambao wingi wao haujaisaidia nchi?
  2. Kama tunaongeza, kwa nini tuongeze wabunge kwa vigezo laini kama vilivyotajwa badala ya kuangalia maslahi ya nchi hasa tukielewa kuwa uchumi wetu uko hoi?
  Hoja ya Tunayofahamu:
  1. Kwa sasa hivi, nchi yetu iliyomasikini na yenye zaidi ya 50% ya bajeti inayotegemea misaada, ina Bunge la Muungano lenye wabunge 323, ambapo 232 ni wa majimboni na waliobaki wakiwa ni wa-mapambo. Pia TZ yetu ina watu karibu milioni 40 tu na ukubwa wa km za mraba 945,200.
  2. Ukilinganisha na Marekani wenye utajiri na mkubwa, nchi kubwa (mara kumi zaidi ya yakwetu = 9,827,000 Sq. km) na watu zaidi ya milioni 300, wao wana wabunge 435 tu. Kwa nini hatufuati sheria za kiuchumi zinazoeleza wazi kuwa unapokuwa hujitoshelezi kimapato, basi unatakiwa upunguze matumizi?
  3. Kwa nini tuongeze wabunge badala ya kuwapunguza? Kila Mbunge anatugharimu sio chini ya TShs. 15,000,000 kwa mwezi au TShs. 180,000,000 kwa mwaka (Dr. Slaa naomba msaada hapa). Hii gharama ya kumuweka bungeni mbunge Mmoja tu ni sawa na kusomesha UDSM waalimu 180 au mainjinia 150 au madaktari 150 kila mwaka. Lipi ni bora, kumstarehesha mbunge 1 au kusomesha mainjinia 150?
  Maoni;
  1. Badala ya NEC (Tume ya Uchaguzi) kuiongezea nchi mzigo wa wanene, serikali kwa kushirikiana na Bunge, zipunguze majimbo ya ubunge na tufute kabisa wabunge wa kuteuliwa mpaka hapo uchumi wetu utakaponawiri. Ni wazi Serikali ya JK haiwezi kulikubali hili, sasa kwa nini wapinzani msilitumie hili kama wimbo wa kuwaimbia wananchi mapema mpaka walielewe hili?
  2. Kwa hali ya uchumi wetu, hatupaswi tuwe na zaidi ya wabunge 5 kwa kila mkoa, yaani tuwe na bunge la watu 100-125. Hakuna mbunge atakayeshindwa kuzungukia jimbo lake au hata mkoa mzima angalau mara 4 kwa mwaka.
  3. Bunge la watu 125 kwa makadirio ya haraka-haraka lingeokoa zaidi ya TShs.36,000,000,000. Hii ni sawa na Tution Fees ya Madakitari 24,000 kwa mwaka mzima au sawa na majengo 5 ya wadi ya watoto Muhimbili kila mwaka. Kwa nini tusipunguze wabunge tukapata pesa ya kusomesha?
  4. Hii tabia ya viongozi wetu Tanzania, ya kufuja vichache tulivyo navyo kwa kuendelea kujipangilia matumizi bila kuangalia hali yetu ya uchumi duni inapaswa ikome. Inapaswa tuanze kuwawajibisha wale wote wanaojipangilia matumizi bila kuangalia uwezo wa nchi au manufaa ya hayo matumizi kwa taifa. Ningeomba tuanze na hawa majaji wa NEC.
  5. Hatuhitaji nyongeza ya wabunge bali tungefurahi kama wakipunguzwa maana wingi wao haujaonesha kama unatusaidia.
  6. Badala yake, tutumie pesa yetu kiduchu tuliyonayo kuwekeza kwenye elimu ya watoto wetu ili tuache kuendelea kuogopa nchi jirani zetu waliotuzidi kielimu.
  Mungu ibariki Tanzania. Naomba kutoa hoja wana-JF.


  Soma Utafiti wa UWAZI.ORG
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  101% right
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Na kama hiyo haitoshi, leo Marmo kasema wanaongeza idadi ya wabunge wa viti maalum (wanawake) eti wafikie 40% na kuwa hiyo ipo kwenye katiba. Hivi katiba inawazuia kufikia % hiyo kwa kugombea majimboni? Tatizo kubwa la serikali yetu ni vipaumbele!
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Zanzibar pekee kuna Baraza la Wawakilishi, wapo 50 kama sikosei, halafu na wengine wanakuja kushiriki bunge la Jamhuri ya Muungano. Huwa najiuliza sana kama kuna mahitaji kiasi hicho!!
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Ebwana hilo swala la kwamba wanataka kuongeza wabunge ili wajaze ukumbi unatania right?

  Please say so!
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Freetown,
  Inabidi pia Tume ya Uchaguzi (NEC) kujiuzulu. Wawe wameshurutishwa kutoa hayo maamuzi au la sio hoja tena.

  Kwa wao kutoa matamko ya kuwa wanaongeza wabunge ili kuondoa msuguano ndani ya CCM, ina maana hawafanyi kazi zao kwa manufaa ya Taifa bali wanawatumikia hao wachache ambao wanajiona kuwa ni lazima waingie bungeni hata ikibidi kwa kutengewa majimbo maalumu kwa ajili yao.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..kwa kweli hapa nakubaliana na wewe 100%.

  ..sasa basi viongozi wa vyama vya upinzani viyakatae mapendekezo haya.

  ..waandishi wa habari, na asasi z kijamii pia wanapaswa kulikemea suala hili.
   
 8. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hawa akina Marmo ndio wote wanaotakiwa kuachia ngazi sasa maana bongo zao zimeshapita expiration date.

  Hawaangalii uwezo wa nchi kubeba hizo gharama za wabunge wapya na function ya hao wateule, wanachojadi ni kuwa na statistics tu watakazozitumia kujisifia kwenye makongamano nje ya nchi.

  Zaidi ya hayo, nafasi zikiongezwa utasikia wanaopewa ni wake zao, vimada wao na watoto wao. Kwa nini starehe ziwe kwao nongwa watuachie sisi?
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..wabunge wanawake wa viti maalum wawe wanateuliwa kwa term moja tu. baada ya hapo kama wanataka kuendelea kuwa wabunge basi wakagombee kwenye majimbo.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hata Wabunge wakiwa 100 peke yao kama hakuna mikakati madhubuti ya Elimu,Afya n.k hali itakuwa mbaya tu...hoja hapa sio kuwa na wabunge wengi ama wachache.
   
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Kwani wakipewa term moja idadi ya wabunge itapungua? Angalia hoja ya mleta mada; kupunguza idadi ya wabunge kuokoa fedha. Kupunguza term ya service ya mbunge ni jambo lingine, kwani hata huyo mpya atakayekuja atatumia fedha zile zile so tutakuwa hatujaokoa kitu.
   
 12. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli dah umaskini unazidi kutawala si maisha yetu tu sasa mpaka akili zetu sijui lini wanasiasa wa watanzania wataweza kuongea ukweli na kutekeleza ukweli safari bado ndefu
   
 13. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndio mahesabu yao kuwa kwa vile kuna viti vitupu basi wavijaze. Hawa wenzetu wamelewa madaraka.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Gabu,

  ..kuna mchangiaji ameeleza kwamba Waziri Marmo amegusia kuhusu kuongezwa kwa idadi ya wabunge wa viti maalumu wanawake ili wafikie 40% ya bunge.

  ..sasa mimi nilikuwa naendeleza mjadala kuhusu wabunge wa viti maalum kwamba wapewe kipindi kimoja tu.

  ..kwa upande mwingine naungana na wengine wanaopendekeza kwamba idadi ya wabunge isiongezwe, na zaidi ingekuwa vema kama ingepunguzwa.

  ..zaidi, gharama za uendeshaji bunge letu, ikiwemo mishahara na marupurupu, zipunguzwe.
   
 15. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JokaKuu,
  Labda waandishi wa habari na asasi za kijamii ndio wasaidie kulizima hili, maana The Citizen limeripoti kuwa wabunge wa CCM na wa upinzani wote wanaelekea kukubaliana na huo uamuzi.
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa habari hao hao wakishapata popularity wanachukua form kugombea ubunge, unategemea watalizima hili? Nasikia Mkamia anapasha misuli kuwania Dodoma, sasa sijui ni mjini au kwa mzee JSM !!
   
 17. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi ndio wanavyofikiria wabunge wetu. Hakuna hata mmoja anayeuliza gharama za hiyo shughuli zitabebwa na nani.
   
 18. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  [FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Makabe primary school standard two pupils doing their schoolwork sitting on the floor due to shortage of desks, as captured by photographer Peter Mgongo, in Dar es Salaam on Tuesday.[/FONT]
  Hii ndio hali halisi ya shule zetu. Wanafunzi wanasomea chini. Hivi tunawaanda hawa malaika kuwa wanasayansi kweli kkwa staili hii?
  Idadi ya Wabunge ipunguzwe na pia kuwepo na mkakati mahsusi wa kuendeleza elimu yetu hapa nchini
   
 19. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Obi,
  Umeweka picha inayotueleza mengi sana.

  Wabunge wapunguzwe kulingana na uwezo wetu. Pale uchumi utakapokua basi ndio tufikirie kati ya kujenga shule, hospitali na kuongeza wabunge.

  Hivi sasa tuna wabunge wengi ambao kwenye majimbo yao hakuna shule wala hospitali za maana, lakini gharama za kuwahudumia hao wabunge zinazidi gharama za kujenga hospitali na shule majimboni mwao.

  Ni vema tukaangalia upya wapi tunatumia pesa yetu badala ya kuwakubalia hawa wanene wanaotaka kuongeza wanene wengine kati yao.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Kubwajinga, Naunga mkono hoja yako ndugu yangu. Kuongeza idadi ya Wabubnge hakuongezi tija yoyote katika nchi yetu bali ni kuongeza tu gharama kubwa zisizo na msingi wowote. Bunge lenyewe ni Bunge butu liko pale kuhalalisha sera za chama tawala hata kama sera hizo hazileti maenedeleo yoyote kwa nchi yetu. Ukiangalia tangu bunge hili lichaguliwe 2005 hakuna chochote walichokifanya ambacho tunaweza kuwapongeza na hata wakiongeza idadi zaidi ya Wabunge hakuna chochote watakachofanikisha maana wameweka mbele maslahi yao binafsi, ya chama chao (ccm) badala ya yale ya Taifa.
   
Loading...