Tupromote hii project: Unakaribishwa kwa maswali

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,208
1,755
Tunapenda mitaa yetu iendeshwe kidijitali.


Hivyo tumejaribu kuleta suluhisho mahususi katika kuboresha huduma za serikali za mitaa nchini, lengo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo popote pale hatakama huko mbali basi ni rahisi kupata taarifa zako au nyaraka muhimu kutokea mtaani kwako.

Ebu jiulize kuna baadhi ya taarifa ambazo ni ngumu kuzipata mtaani kwako hasa unapokuwa safarini, lakini pia kuna umuhimu wa kuomba taarifa zako ziandaliwe hatakama uko mbali.

Taarifa ambazo unaweza kuzikosa ni kama vile taarifa za misiba, ushiriki matukio ya mtaa n.k

Taarifa unazoweza kuomba ni kama vile barua za utambulisho, kujua kama namba yako ya nida iko tayari kupitia serikali ya mtaa wako kwa kuwa wao upokea taarifa hizo n.k

Je ungependa kuendelea kusumbuka kila wakati kwenda office ya mtaa wako au kata bila shaka isingependeza ila kwa vitu vichache sana unaaweza fanya hivo.


Muundo wa mfumo na utendaji kazi.

Mfumo uliundwa kwa lengo la kusimamia shughuli za mitaa inayopatikana katika kata husika hapa hatukuweka kimkoa au kiwilaya bali kila kata ndani ya wilaya ita host portal yake na kwasababu ndani ya office ya kata kuna umuhimu wa kuwepo miundo mbinu ya ICT hatakama office ya mtaa haitakuwa na vitu hivyo basi shuguli zote zinahamia kata na kupunguza gharama za kila mtaa kuwa na miundo mbinu hiyo.

Ingawa hatukuweka msimbo hapa, msimbo upo kwenye saraka binafsi.


Utendaji kazi

Wasimamizi wa mfumo huu wenye taarifa za wakazi wa mtaa husika ni Mtendaji wa mtaa(uwezo wa kusimamia kila aina ya taarifa nitaweka baadae), mwenyekiti(uwezo wa kusimamia taarifa kazaa), balozi(yuko chini ya mwenyekiti) na wajumbe.

kabla ya kuelezea kazi zao kiufupi niweke namna mfumo unavyofanya kazi.

ukiwa kwenye kurasa ya kuingilia utaweka jina la kuingilia na nywila, endapo utakosea mara tatu basi itabidi usubiri baada ya dk 30 hii hata uzime na kuwasha computer hautaweza labda ubadili ip address au saa ya computer.

Endapo utasahau nywila basi itabidi ufanye marejesho ya akaunti.

Mradi umegawanywa katika sehemu tatu,

Eneo la wakazi(haihitaji kuingia ndani ya mfumo bali utaweza ingiza namba ya simu au nida na kuweka maombi au maoni yako na mfumo utajua unapeleka mtaa gani kulingana na ulikosajiliwa),

Eneo la viongozi wa mitaa na msimamizi mkuu
mfano iwapo kata ina mitaa 25, mfumo utawatambua viongozi, wakazi , nyaraka, matukio, maombi, matangazo na mengineyo kulingana na mitaa yao bila kuchanganya taarifa.

Wakazi wanaweza kuomba Barua za utambulisho kwa taasisi fulani, Kuomba/kuulizia kitambulisho cha nida ikiwa kiko tayari, Kutoa malalamiko na mapendekezo katika mitaa yao.

Viongozi wanaweza kusajili mwanachama mpya wa mtaani, na uwezo wa kuunganisha taarifa za mwananchi kwa NIDA api kwa MAOMBI YA KITAMBULISHO CHA NIDA(Hakuna haja ya mwananchi kwenda kujiandikisha NIDA katika ofisi ya NIDA) kipengele hiki kinapatikana katika hali ya test kwa sasa.

Maongezeko
Anachoweza kuona kiongozi wa mtaa

Anaweza kuona idadi ya raia, kaya, viongozi, hati rasmi, kutuma tangazo kwa raia wote kupitia nambari za simu za raia zilizosajiliwa, kipengele hiki kinafanya kazi kwa sms api.

Vipi kwa mkazi

Anaweza tuma aina yoyote ya ombi au pendekezo kwa viongozi wake wa mtaa

Anaweza pokea taarifa na arifa muhimu kupitia ujumbe wakati ombi lako limechakatwa



NB: MNSIMAMIZI MKUU WA MFUMO NI MTENDAJI KATA NAYE ANAW3EZA KUONA TAARIFA ZA MTAA MZIMA INILA KUFANYA EDITING ISIPOKUWA KW A MAMBO MUHIMU TU.

Mambo hayo ni kama kuona idadi ya wakazi na viongozi wa kata nzima, waliokufa na waliopo.

Mengine yatawekwa kulingana na maswali na maoni yatafanyiwa kazi


snap

 
Project inainekana itakua good sana, sema nina wasi wasi na mwitikio wa wananchi ambao ndio walengwa.
 
Project inainekana itakua good sana, sema nina wasi wasi na mwitikio wa wananchi ambao ndio walengwa.
Kitu nilichoangalia mitaa mingi hata office Ao hawa computer lakini hii si sababu haiwezekani ofisi ya mtaa ikose computer hata mbili na hapa pia itapunguza swala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa ICT kwa sababu wataajiriwa kwenye office za mitaa yao pia hataambo ya chaguzi za viongozi wa mitaa inabidi waweke vijana na serikali ikifanya hivyo basi kuna jambo zuri mno kimaendeleo kwa wananchi .


Serikali za mitaa Inatakiwa kwenda kidijitali ili kusaidia wananchi wao kwa mambo mengi labda tukipata maswali ya wananchi kupitia hii forum tunaweza ongeza vitu vingi ambavyo ni muhimu zaidi.


Tunaomba ushirikiano wenu ndugu zangu ni
 
Kitu nilichoangalia mitaa mingi hata office Ao hawa computer lakini hii si sababu haiwezekani ofisi ya mtaa ikose computer hata mbili na hapa pia itapunguza swala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa ICT kwa sababu wataajiriwa kwenye office za mitaa yao pia hataambo ya chaguzi za viongozi wa mitaa inabidi waweke vijana na serikali ikifanya hivyo basi kuna jambo zuri mno kimaendeleo kwa wananchi .


Serikali za mitaa Inatakiwa kwenda kidijitali ili kusaidia wananchi wao kwa mambo mengi labda tukipata maswali ya wananchi kupitia hii forum tunaweza ongeza vitu vingi ambavyo ni muhimu zaidi.


Tunaomba ushirikiano wenu ndugu zangu ni
Mkuu walengwa ni watanzania maelezo kingereza. Jaribu kuandika kwa kiswahili chepesi maana watanzania kingereza kinatutia uvivu
 
Digital divide unaizungumzia vp?
Mfano watu wasio na smart bado wanaweza pata taarifa kwa mtu mzima mwenye feature phone bado anaweza pokea taarifa kama alivyo mtu mwenye smartphone.



Na ndio maana tunaita mtaa information management system akina kijiji chenye mtaa hivyo maeneo mengi yenye mitaa yana access na internet swala la msingi ni miundombinu hapo kwenye office ya kata.

Hata hivyo hatuwezi bridge digital divide kwa asilimia 💯 kwa sasa hivyo tumejaribu kucover maeneo hayo kwa asilimia hizo kwakuwa Tanzania ni underdeveloped country tunajua hata vijiji baadae vitakuwa mitaa.

Vipi nimejibu swali au bado
 
Back
Top Bottom