Tupo wana CCM huru tunaounga Katiba Mpya Movement, CHADEMA endeleeni kuchochea Moto

The lobbyist

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
868
1,000
CCM ina makundi ya wanachama wa aina kadhaa lakini, haya makundi ndio 'prominent'.

CCM kindakindaki yaani hawa ni kama CCM lialia. Hawa wapo wengi kiasi na ni wazee wazee Kwa wingi wao. Hawana maslahi yoyote na chama, wengi wao wamepigika mno ki maisha. Hata hawajui kwa nini wanaipenda chama, yaani wamejikuta wanaipenda tu. Hawa hawapo frontline sana.

CCM maslahi, hawa ni kama wale wanachama wa upinzani wanaohamia CCM wapate uteuzi, and the likes. Hawa ndio wale 'zidumu fikra za Mwenyekiti' cha muhimu 'tumbo lake lijae chakula'. Hawa wapo frontline kwa kila kitu kupigania chama maana mambo yao yanategemea uhai wa chama. CCM maslahi ndio kundi kubwa zaidi kwenye chama, wahamiaji ni wachache sana. Ila mara nyingi hujikuta chemistry zao zina match Kwa sababu wanakuwa na common interest. Hawa ndio wanufaika wakubwa wakubwa wa chama na mifumo ya utawala. Hawa huwatumia wana CCM wenzao kujinufaisha zaidi.

CCM limbukeni. Hawa ni wengi kiasi. Hawajui misingi ya chama, na hawajui chochote kuhusu chama. Hawa hawawezi kufanya analysis ya chochote kile kuhusu siasa, wao ili mradi ni CCM hewalaaa. Yaani hawa ni wale ambao wapo wapo tu hata hawajielewi. Hata ukiwa 'confront' vizuri kuhusu jinsia yake anaweza kukukwambia yeye ni 'ke' ilhali ki bailojia ni 'me'. Yaani wapo hvyo yaani.

CCM huru. Hawa ni wale wanachama wachache sana wanaojielewa sana. Hawa wana logic reasoning kubwa kubwa. Wanajitegemea kwenye shughuli zao za ki uchumi bila hisani ya chama. Hawa wanaamini katika misingi ya chama 'Jembe na Nyundo'. Hawa ni wachapa kazi by nature. CCM Music yupo kundi hili. Hawa hawapo kwenye frontline politics sababu wanaona utoto mwingi kwenye majukwaa ya siasa.

Kwa mfano: CCM huru wanaamini wapinzani ni wepesi sana tukienda nao hoja Kwa hoja. Ki msingi wapinzani hawana hoja za maajabu, hoja zao ni za kawaida sana, hazistui.

Sasa, CCM huru tunaunga mkono movement ya katiba mpya. Ni kweli katiba yetu imezeeka, na ndio maana hata JK aliasisi mchakato wa kuandika katiba mpya. JK ni mwana CCM, na anakubali kweli kuna haja ya kuandika katiba mpya.

Sasa, nyie CCM lialia, CCM maslahi, CCM limbukeni muache kutuharibia chama kwa kushupaza shingo.

Katiba mpya ni muhimu na tunaitaka kwa ajili ya mustakabali mzima wa nchi yetu, na sio kwa ajili ya mustakabali wa maslahi yenu wenyewe kwa wenyewe.

CCM ni chama cha wananchi na sio cha wanufaika wa chama.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,332
2,000
Kazi mnayo.. wananchi wengine na sie tunafata ya Rais wetu.. kwani yeye yupo kundi lipi?
 

The lobbyist

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
868
1,000
Kuna wana CCM wanatoa mifano Mbowe mbona yupo Mwenyekiti miaka na miaka.

Sasa, unajiuliza CHADEMA wanataka katiba mpya ya CCM ama ya nchi? Hii hoja inatoka wapi? Hawa sasa ndio CCM maslahi na CCM limbukeni.

Wanatuharibia chama sana hawa
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,782
2,000
Kabla ya kuibadili inapaswa kwanza tufahamu hiyo Katiba ni nini na inapatikanaje?

Halafu pia tuifahamu hii iliyopo uzuri na mapungufu yake.

Maana nyimbo za katiba mpya ni nyingi wakati hii tuliyonayo hata sio kila mtu anaifahamu kiasi Cha kujua uzuri na udhaifu wake.
 

The lobbyist

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
868
1,000
Kabla ya kuibadili inapaswa kwanza tufahamu hiyo Katiba ni nini na inapatikanaje?

Halafu pia tuifahamu hii iliyopo uzuri na mapungufu yake.

Maana nyimbo za katiba mpya ni nyingi wakati hii tuliyonayo hata sio kila mtu anaifahamu kiasi Cha kujua uzuri na udhaifu wake.
Ni wajibu wako mwenyewe kujua hayo. Majukumu hayo unampa nani akufanyie?

Nchi chini ya utawala wa CCM ikusomeshe bure nako unataka kuipa jukumu la kukuchambulia katiba?
 

mgunga pori

JF-Expert Member
Jul 23, 2016
3,128
2,000
Kabla ya kuibadili inapaswa kwanza tufahamu hiyo Katiba ni nini na inapatikanaje?

Halafu pia tuifahamu hii iliyopo uzuri na mapungufu yake.

Maana nyimbo za katiba mpya ni nyingi wakati hii tuliyonayo hata sio kila mtu anaifahamu kiasi Cha kujua uzuri na udhaifu wake.
Elimu
Elimu
Elimu
Mifumo yetu nishida sheria ya uchaguzi 1985 inataka elimu ya uraia vs siasa iwe inatolewa kila mara lakini waaapi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom