Tupo tayari mulipe dowans ila tu mara baada ya serikali kuwataja waliohusika katika hili!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupo tayari mulipe dowans ila tu mara baada ya serikali kuwataja waliohusika katika hili!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dguyana, Nov 7, 2011.

 1. d

  dguyana JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Mtazamo wangu upo sawa na Warioba kuwa deni la Dowanskuwa lipo kisheria na haliepukiki. Mi nadhani hapa ni kutumia maandamano kuilazimisha serikali kuwataja watu wote waliohusika kutuingiza katika sakata hili la tokea Richmond hadi dowans. Wapatikane na wachukuliwe hatua kali ikiwa mujawapo ni kufilisiwa. Nadhani kupatikana au kujulikana kwa watu hawa kutamaliza hasira za walio wengi mmoja wapo ni mimi.

  Au wana JF mnasemaje?
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Sawa kabisa naunga mkono oja,watajwe,wafikishwe mahakamani na mali zao zote zitaifishwe zilipe deni
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  ni kweli watu wawili tu miongoni mwao wana mali zenye thamani zaidi ya deni hili na wana uwezo wa kulilipa lakini tatizo ni kuwa mali zao zote hata 1% haijaandikwa kwa majina yao bali ni kwa uficho ambao uko organized vizuri kiasi kwamba mtu wa kawaida kujua sio rahisi!
  Wewe mwenyewe sio ajabu uko kwenye 'chain' ya DOWANS lakini hujijui. Ndio maana jamaa mmoja anasema kuwa hapa aje dictator aamue 'kuvunja' haki za binadamu na kukubali lawama kwa maana watu wanajua mali zao lakini kisheria huwanasi ngo!
  hapo kwenye red ni kuwa hawa jamaa wangelikuwa na huruna na wewe wasingekufanyia wanayokufanyia lakini sisi (watz) ndio tunawahurumia wakati tukijua fika kuwa wenyewe hawatuhurumii!
  Ni sisi tunaoweza kuamua hawa watu (DOWANS) wajulikane bali wao hawawezi kufanya hivyo maana ndo wenyewe! Kama kweli Mungu alikupa akili na ujasiri, basi amua moja badala ya kulalamika.
   
 4. d

  dguyana JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila ni kweli inawezekana wangu. Kama hivi tumeajiriwa na Makampuni binafsin You never know!!!. Ila inamaana hata hawa kina Warioba hawaujui ukweli jamani? Ina maana katika serikali hii hakuna hata mwenye huruma na Watz aamue kuweka mambo hadharani? Sina imani na Sitta kwani najua ni msaliti. Kama anaupenzi na nchi yake na ukweli anaujua kwanini asiweke kila kitu wazi?
   
Loading...