Tupo tayari kulipa kodi ya nchi bila kujali ukubwa wake

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
431
577
Ndugu zangu habarini ! Poleni kwa changamoto zinazowakabili kutoana na mihangaiko mnayokabiliana nayo.

Niende kwenye mada, ndugu zangu Watanzania wapotayari kulipa kodi kwaajili ya maendeleo yao bila kujali kiwango watakachotakiwa kulipa kwa serikali yao.

Ila kutokana na madhaifu kadhaa kutoka kwa Serikali yao inapelekea masuala ya ulipaji wa kodi kuwa ni kaa la moto kwa Watanzania hawa.

Baadhi ya madhaifu hayo ni kama ifuatavyo:

*Kodi zinazopendekezwa haziwahusishi wananchi wao ambao ni wadau wa kodi.

*Kiwango cha kodi kinachotozwa nikikubwa hakizingatii hali ya maisha ya mlipa kodi

*Kwenye kitu kimoja kuwa na kodi zaidi ya moja huo ni mzigo mkubwa sana kwa milipa kodi

*Baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali mishahara yao haitozwi kodi hii hukatishatamaa kwa walipakodi wengine.

*Baadhi ya viongozi wa Serikali mishahara yao kuwa siri halafu hao ndio wanaopendekeza viwango vya kodi kwa walipa kodi na kujiita wazalendo kwa nchi yao jambo hili huondooa kujua maumivu ya mlipakodi na inakuwa vigumu kusikia kero za mlipakodi

*Walipakodi wa vijijini hawana haki ya kutumia hela inayotokana na kodi zao. Kodi wanazolipa watu wa kijijini zinaenda kujengwa miji ambayo ishajengwa tayari . Na nyingine zinatumika kujenga sehemu aliyotoka kiongozi mkuu hivyo hufanya maeneo wasitoka viongozi wakuu kuendelea kuwa maskini zaidi

*Kodi nyingine zinaanzishwa kimkakati tu ili kuwafanya walipakodi wajue kuwa serikali ya chama fulani ipo na inawatetea wananchi wake. Utakuta kodi kubwa inaanzishwa ghafla kiongozi mwingine anajitokeza kuiondoa ili apate huruma ya wapiga kura kwa kipindi fulani.

* Kodi nyingine zipo kwaajili ya kuwafanya maskini waendelee kuwa maskini zaidi ya hapo awali. Hii kodi ipo zaidi kwa mkulima yaani kila hatua anapiga mkulima kwaaili ya maendeleo ya mazao yake na maisha yake yamejaa msururu wa tozo na kodi za ajabu.

Hitimisho: Ombi kwa watunga sera za kodi wazingatie uwazi, hali ya kipato ya mlipakodi , kodi ilete manufaa kwa kila mlipakodi bila kujali tabaka la uongozi ama uchama wa wananchi kwakuwa kodi tunalipa wote kwa viwango vilivyopitishwa na serikali na maendeleo tupewe wote bilakujali matabaka yetu.
 
Back
Top Bottom