TUPO SALAMA? Mwili wakutwa ufukweni Kawe jijini Dar ndani ya kiroba

Mungu anisamehe hapa. Usikute huyu marehemu pengine alitaka kujifanya steling wa bongo muvi, kajitupa majini kashindwa kujiokoa na kukimbiwa na madirectors uchawara.
 
Uchunguzi umesha fanyika na kungundulika ni Mtanzania? Na Chanzo cha kifo chake unakijua?? Huo utawala wa udhalimu upo wapi??
Kuna kitu unajua nn? Alipotekwa Roma mkatoliki Kuna kiongozi alijitokeza na kuahidi kwamba Mkatoliki atapatikana kabla ya j2, na kilichotokea kila mtu alishika mdomo kwa bumbuwazi. Connect the dots brother, hope you are not that dumb!
 
Mwili wa mtu asiyejulikana umekutwa kwenye fukwe za Kawe ukiwa umefungwa kwenye kiroba Asubuhi Hii na Hadi sasa haujatambulika kuwa ni mwanaume au mwanamke.

Mashuhuda wanasema kuwa wavuvi wameusogeza ufukweni hapo, na kuucha, Jeshi la Polisi lina Taarifa na Wapo Njiani Kuelekea Eneo la Tukio.

View attachment 568584
Chanzo: Times Fm
Dah ya dunia mengiiii
 
Naona wako bize kwa mbinu hii ya kufunga binadamu wenzao kwenye viroba. Basi sawa endeleeni
 
inasikitisha ila mtoa mada please tujuze zaidi hasa ulipoandika kuwa maiti hiyo imekutwa ufukweni ,HALAFU wavuvi wakaosogeza ufukweni;kama hili limefanyika ni kosa kubwa mno maana kukutwa kwa ile maiti lile eneo tayari ni crime scene,hawa wavuvi wasingehamisha ule mwili maana tayari wameshaharibu vielelezo vya kuishahidi ambavyo vingesaidia polisi (foresinc dept)sijui kama tunayo ndani ya jeshi letu la polisi,walichotakiwa kufanya ni kitoa taarifa polisi na kulinda ile crime scene,maana kutokana na soli za viatu vyao,finger prints,kuwa zimeshachafuliwa upelelezi utakuwa mgumu zaidi,ni vema watanzania tukatambua umuhimu wa kulinda hizi crime scenes ili kuwarahisishia polisi kazi.
'

666
 
Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu walishawahi kuwa na nia ya kuanzisha (kuhalalisha) matendo haya. Hapa ni Yericko Nyerere kabla hajaverify account yake (alipokuwa na account fake). Naweza kuanzisha kampuni ya kuua na nikapewa leseni hapa TZ? (licence to kill) au LTK
Hatuwezi jua, anaweza kulisaidia jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kama alifanikiwa nia yake au la! Na kama hakufanikiwa, alisitisha nia yake au aliamua kufanya shughuli hizi bila kibali alichokuwa anakitaka?
Licence to kill what? Kuku, mbuzi, ng'ombe , antelope??? Fafanua vizuri mkuu

666
 
Huko Kenya kipindi cha Moi watu waliokuwa wakimpinga waliuawa katika msitu mnene nje ya nairobi ikijulikana kama Ngong naona na huko nchini kwetu shughuli inakua kwa kasi.

Kwa sasa mauaji ya namna hii inaonekana Tanzania imeiacha Kenya kwa mbali. Wenzetu wanapiga hatua kwenda mbele, sisi tunaenda walikotoka.
 
MIMI SIJASEMA HUYU NI BEN ILA HATA SAANANE INAELEKEA KIFO CHAKE KILIKUWA KAMA HIVI
Yes dear. Nimekupata. Nilisema sidhani kama huyu atakuwa kauwawa kwa kumuandika vibaya mtu kwenye mtandao. Inawezekana wamedhulumiana au haya mambo ya wivu wa kimapenzi...
 
Kwenye Kiroba?? Duh hii style nani anawajua watumiaji wake??
 
Back
Top Bottom