tupo kwenye mahusiano huu ni mwaka wa saba bado hatujaoana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tupo kwenye mahusiano huu ni mwaka wa saba bado hatujaoana.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VAMPA, Jan 17, 2012.

 1. V

  VAMPA Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu nina umri wa miaka 32 male, na mwenzangu ana miaka 27: mwenzangu ni mpare mi mnyakyusa. tulianza mahusiano mwaka 2006; kabla hatujaanza mikakati ya ndoa nikaenda masomoni mwaka 2008. ikawa vigumu kuendelea na mchakato, lakini baada ya kumaliza chuo naona bado hakuna dalili ya kufunga ndoa hivi karibuni kwani mwenzangu anahitaji ndoa ya kifahari wakati mimi uwezo huo sina, inanibidi nifanye kazi sana ili nijiweke fiti kwa hilo. natamani saana kuwa na mke jamani
  NISAIDIENI WAKUU UMRI UNAENDA.
   
 2. r

  rebeca Senior Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  afu huku kwenda kusoma ulaya kunapotezea sana watu muda afu wachumba hatuwaoni,hasa wanaumeeeeeeeeeeeeeeee mie nina ukame jamani......tukiangalia our tanzania brothers and sisters wanaowana na tayari wanasettle sie tunahangaika tu na maboksi........wewe mkaka may be you need to rethink about your decision...hii inaonyesha hamko compartible when it comes to finances huyo mwanamke atakusumbua siku za usoni,wewe unawaza kuwapelekawatoto weny shule za kawaida yeye anawaza kuwapeleka international school wkt hela hamna,,bado atataka anunue ka vitz kakuringishia mashosti wake wakati hela ya mafuta hajui ataitoa wapi inshort more trouble ahead.
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145


  Ukame wa nini tena??
  Box lako unalipigia pande zipi ndugu?
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee!!
  Inaonekana vipaumbele vyenu vinatofautiana sana.

  Je kuna mapenzi kwenye hayo mahusiano yenu? Nauliza kwasababu naona umeongelea mpaka kabila kitu ambacho sio muhimu sana ila hujasema kama mnapendana au angalau kwamba wewe unampenda. Yukirudi kwenye "tamaa" yako ya kuwa na mke, je unatamani kuwa na mke au unatamani yeye awe mke wako? Akiendelea kusema bila harusi ya kifahari msioane ukaona binti mwingine anaekuvutia na yuko tayari kwa ndoa/kufunga harusi isiyo na mbwembwe utamuoa yeye?

  Nwy ongea na huyo mwenzako, mwambie kwamba usingependa kusubiri sana na umueleweshe kwamba uwezo wa kufunga harusi ya kifahari hamna hivyo inabidi mtumie hicho kidogo mlichonacho. Muulize nini ni muhimu kwake kati ya kuwa mke wako na kuwa na sherehe kubwa (ili kujionyesha na kupata sifa I guess) ya siku moja tu na ambayo binafsi haitowafaidisha hata kidogo. Mkishindwa kuelewana inabidi myapitie tena mahusiano yenu kuhakikisha kwamba mko kwenye ukurasa mmoja, msije mkaingia huko nako kukawa kuchungu hata kama mtamanage hiyo harusi ya kifahari.
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kuna thread umeanzisha unamshangaa jirani yako kapata mchumba feisi buku ndani ya siku mbili na wameanza maisha. Hujajifunza tu?
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hamna kitu hapo wajilisha upepo tu.
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo hapa una maanisha neyeye aachane na huyu then acheck mbadala faster na waanze maisha?
   
 8. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hapo anataka harusi ya kifahari, ukijikakamua ukaoa atataka na maisha ya kifahari huyoo. kweli atakusumbua huyo ana mambo makubwa kuliko uwezo wako. cha msingi orodhesha opportunities na threats za kuja kuishi nae huyo bibie then fanya uamuz mkuu.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu nafikiri umeshamsoma huyo mchumba wako muda mrefu na kuna vitu ambavyo umeviona kwake ambavyo wewe vinakupa red colour na ambavyo huvioni vya kawaida.
  Kwake kutaka harusi ya kifahari sidhani kama ni kitu kilichoibuka mara moja tuu. May life style yake ni the same anapenda maisha ya juu na ya kifahari. Anapenda may be kwenda sehem za kifahari au matumizi ambayo hayaendani.
  Sasa hapo wewe akili kichwani mwako kuangalia type ya mke unayemtaka.
  Hebu kaa nae uangalie priority zake ni nini. Ni harusi ya kifahari ya siku moja au ni mume wa maisha yake. Je harusi ya kifahari ya siku moja ndio ya muhimu kuliko kuwa na mume wa maisha yake yote na mwenye mapenzi kwake.
  Au ni maisha gani anapenda. Na je anajua kuwa kuna maisha baada ya hiyo harusi ya siku moja ya kifahari. Je na wewe uwezo wako utamwezesha kumudu life gani. Mwambie uhalisia wa kipato chako na ajue kuwa hicho ndio kitawasaidia kuishi na kuendelea mbele kuwa na familia na kuitunza na hata maendeleo yenu.
  At least aelewe kuwa kuna maisha baada ya harusi ya siku moja ya kifahari. Na aelewe anaingia kwenye ndoa kukiwa na kusaidiana na kuishi kulingana na kipato na kuendelea yaani kuwa na maendeleo binafsi.
   
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole,mie nadhan hapo onesha mcmamo wa kuoana mapema iwezekanavo na muweke wazi kuwa huna uwezo wa kufanya aruc ya kifahari na huon umuhim huo,kuna mambo mengine bila kuonesha mcmamo inaweza ikakucost badae maana hapo kuna harufu c nzuri,chukua hatua mapema ijijue km ndio ushaumizwa ujipange mapema!ni nadra sn mwanamke kugoma kuolewa kisa anataka haruc ya kifahari!
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Mie mwanaume asiyekuwa na maamuzi huwa ananikera sana.
  Utakuja kushindwa hata kufanya maamuzi ndani ya nyumba kisa mke???
  Kwani anayeoa mwenzie ni nani?? Au wewe ndo unaolewa???

  Fanya maamuzi na wewe ukiamua umeamua unangoja eti anataka ndoa ya kifahari???

  Acha hizo bana sema nimeamua ndoa itafanyika hivi na hivi kwisha kama hataki huyo ana lake jambo??

  Usikute anakutega ushindwe aendelee na mambo zake wewe hujui shauri yako
   
 12. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kumbe bado hujaolewa na wewe, basi niruhusu mimi nikuchumbie
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Piga chini fasta aisee,tena mkimbie kama Tsunami!
  I have a case ya mwanamke wa sampuli hiyo,kaolewa harusi kubwa mlimani city(njemba ilichukua mkopo ofisini),majuzi kujifungua akadai kama sio south africa basi masaki trauma centre,do you know the bill ya kujifungulia pale trauma centre?dola elfu tatu walimkamua jamaa (another personal loan),ndo maisha gani sasa hayo kwa kijana wa kwenye 30's ambaye hata plot hana?
   
 14. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Huyo dada anaonekana anapenda vitu vya hali ya juu, kaa naye chini uongee naye ya kuwa huna uwezo wa kuwa na ndoa ya kifahari ila unahitaji yeye awe mkeo. Hivyo inabidi mkubaliane mfanye sherehe ya kawaida tu kutokana na uwezo ulionao.
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  DA, inaamini katika msingi wa 'ushauriano' katika ndoa?
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Mleta mada, mwambie agharamie hiyo harusi ya kifahari kama anajimudu, asikulazimishe kujikuna usipofikia unless amekupa hicho kijiti ujikunie!!
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  mwambie afanye kitchen party na sendoff za kifahari wewe utafanya harusi ya uwezo wako..... au kama vipi akupe hela ya kufanya ufahari anaoutaka

  ila tukirudi kwenye uhalisia, mwanamke kama amekupenda kwa dhati wala hatotaka harusi ya kifahari, ukimtamkia ndoa tu atakuwa tayari mara moja, huyo anayekuzingua mwaka wa sabab sas na WALAKINI hapo, hebu chunguza........
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Naamini sana ila sasa si ameshamshauri kuwa wafanye ndoa ya kawaida yeye anataka ya kifahari???

  Kuna ushauri gani tena hapo anataka kama sio maamuzi???? Huo ndo ushauriano unaotaka kwa upande mmoja kulazimisha kitu kisichowekana kwa lazima.............. yeye hana uwezo analazimisha sasa utafanyaje kama sio kutumia uanaume..............please note simtetei huyu mwanaume hata kidogo but hana uwezo afanyeje sasa anamtafutia balaa akaibe??? Akubali kwa kidogo kilichopo
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  DA, mimi silazimishi ushauriano unaoudhani kama ulivyoandika! I am a true follwer of the principle of consultation katika nyanja zote za maisha. Na hii haimaanishi kuwa siwezi kufanya maamuzi.

  Sasa niliona kama umemaanisha uanamme ndo unatumika kuamua kana kwamba lisemwalo na mwanaume ndo ssahihi!

  What if in this given scenario, huyo dada yeye ana mbumba? Wakishauriana si wanaweza tu kufikia uamuzi kuwa wafanye harusi ya kifahari?

  Otherwise me and you are kinda in the same line!
   
 20. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana kijana.uchumba wenu unaitwa uchumba sugu. Suala la ndoa ni tendo la Kimungu,na Mungu anawasilana nawe kwa viashiria vinavyojionesha, si juu ya JF kukwambia fanya nini. Sie tunakuonyesha 'hiyo red,maana yake moto. Hiyo nyeupe,maana yake moshi mweupe(wa vatkan?),hiyo nyeusi maana yake kiza kinene'. Chukua maamuzi sasa. VUNJA UKIMYA,ONGEA NAYE. KWELI UTAKUWEKA HURU.Inawezekana mchumba wako anania njema,anataka akili yako ichaj na iwe kali kama wembe ktk kusaka mihela,mwambie maji ya mto huo anaotaka uogelee ww huyawezi na harusi ya siku moja ni tofaut kabisa na maisha mnayotamani kuyafikia. Kumbuka,SUTI na Makochi mtu atapata toka kwa baba yake lakin MKE mwema hutoka kw MUNGU. Kila lakheri.
   
Loading...