Tupo katika kizazi kibovu sana kimaadili

May 22, 2017
65
298
Tunaishi katika kizazi cha mbwembwe, yaani mtoto anayejua kuongea Kiingereza vyema ni bora sana hata kama hajui kupika, kufua nguo, kuosha vyombo, hana adabu wala heshima. Tumewekeza kwenye Birthday parties zaidi wazazi kuliko kuwaandaa watoto ki-fikra kuwa wanawake bora na wanaume bora.

Mama bora hufanya make up ya ubongo wa watoto wake kwa kupanda mbegu bora za akili, adabu, uwajibikaji na njia ya kupanda elimu na kumtambua Mwenyezi Mungu wakiwa wangali wadogo.

Wanawake wengine hutumia muda mwingi kufanya make up ya sura zao na maumbo yao, huku watoto wakiwa hawana msingi mzuri wa elimu, adabu, hofu ya Mungu sababu ukosefu wa mama bora. Mtoto aliyekosa make up ya ubongo toka kwa mama na Baba bora huwa na tabia mbaya ukubwani.

Baba bora ni chanzo cha faraja na nguzo ya kuegemea katika nyakati za shida na raha kwa mtoto, wakati Mama bora ni mzizi wa wema, unyenyekevu, adabu na kisima cha amani na upendo kwa watoto wake. Mama ndio pumziko halisi la mtoto.

Mtoto wa kike wa miaka 10 asiyeweza kufua nguo zake za ndani, kuosha vyombo, kufanya usafi anaandaliwa kuwa Mwanamke asiyeweza kuwajibika na chanzo cha tatizo kwenye ndoa yake.

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 asiyeweza kutoa vyombo wakati amemaliza kula, kufua nguo, kutandika kitanda anaandaliwa kuwa mwanaume asiyejua kuwajibika na kupoteza mbegu ya uwajibikaji.

Kwa kifupi tupo katika kizazi kibovu sana kimaadili na malezi mabovu, wazazi wanyenyekevu na wenye hofu ya Mungu na wanaojua kuwafunza watoto wao kwa viboko na kinywa thabiti ndio watakaofaidi matunda ya malezi bora, ila kwa wale kila baada ya dakika picture ya mtoto kwenye social media tutavuna tulichopanda.🙊🙊
 
Ukweli mtupu tumewekeza kwenye mambo yasiyona tija kwa watoto hasa wazazi Hawa wa digital ni hatari kizazi kijacho kitaangamia kwa kukosa maarifa
 
Wanaangalia marudio ya "HUBA" kwa sasa, subiri iishe waje kukuchamba 😂
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom