futurestar
JF-Expert Member
- Oct 15, 2014
- 245
- 77
Kanali Patrick Karegeya alikuwa mkuu wa wa shirika la ujasusi la Rwanda (NISS) na Apollo Gafaranga alikuwa mmoja wa Informer wake. Karegeya alijaribu kumpindua Kagame ktk jaribio lililoshindwa kabla ya kukimbilia nchini Afrika Kusini kuishi Uhamishoni. Serikali ya Afrika kusini ilimpa ulinzi wa askari na wanausalama ili Kagame asiweze kumfuatilia huko.
Baada ya Karegeya kukimbilia Afrika kusini, haraka sana Kagame akaunda kikosi cha kumfuatilia huko kilichoitwa "Escandot de la Mort" yani kikosi cha kifo. Kagame akamteua Appolo Gafaranga kuwa mmoja wa wajumbe wa kikosi hicho. Huyu ni yule aliyekuwa informer wa Patrick Karegeye.
Kikosi hiko kikapewa mafunzo maalumu na jukumunmoja tu la kumuua Karegeya na washitika wake. Mwaka 2010 Apollo Gafaranga akaanza mawasiliano ya siri na Patrick Karegeye akijifanya anachukizwa sana na utawala wa Kagame. Karegeya akafurahi kuwa amepata mshirika wa kumng'oa Kagame. Wakaendelea kuwasiliana.
Gafaranga akawa anasafiri mara kadhaa kwenda Afrika kusini kukutana na Karegeya na kupanga mipango ya kumpindua Kagame. Mara zote Karegeya alikua na ulinzi wa wana usalama aliopewa na serikali ya Afrika kusini. Gafaranga akamshauri Karegeye awakatae askari hao waliokuwa wakimlinda kwa kuwa wanaweza kutumika kuvujisha siri. Karegeya akapokea ushauri huo na kuomba serikali ya Afrika kusini imuondolee ulinzi huo.
Disemba 25 mwaka 2013 Gafaranga aliwasiliana na Karegeya na akapanga kwenda kumsalimia Afrika kusini. Alifika Afrika kusini na akapokelewa na rafiki yake Karegeya ambaye alikua amemchukulia chumba kwenye hoteli ya Sandton, mjini Johanersburg.
Gafaranga na Karegeya wakawa wanakutana chumbani hapo kupanga namna ya kumpindua Kagame. Disemba 31 Karegeya akaenda chumbani humo. Alipoingia, akaweka kibao "do not disturb". Alipoingia ndani wakati akiongea na rafiki yake, mara wakatokea watu wawili waliokua wamejificha bafuni. Wakampiga risasi kwa kutumia silaha yenye kiwambo cha sauti. Walipohakikisha wamemuua wakamlaza kitandani wakamfunika na kuondoka. Hivyo ndivyo Kagame alivyofanikiwa kuzima uasi wa Karegeya aliyekua mkuu usalama wa taifa la Rwanda (NISS).
____________
Habari hii inapatikana ktk kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI cha Yericko Nyerere. Kitabu chenye kurasa zaidi ya 700 chenye mengi ya kujifunza.
[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Habari hii ya Kanali Karegeya inatufundisha kutomuamini yeyote kwenye harakati za mapambano. Karegeye alimuamini Gafaranga kwa sababu tu alikua kijana wake wa kazi. Karegeye hakujua kama kijana huyo aliyemuamini sana ndiye atakayekuja kumuua.
Wakati Karegeya anaasi serikali ya Kagame, na kukimbilia Afrika ya kusini, Gafaranga nae alijifanya kuasi. Akaanza kuwasiliana na Karegeya kwa siri jinsi ya kumpindua Kagame. Kumbe Gafaranga yupo kazini.
Karegeya pamoja na kwamba alishawahi kuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Rwanda hakujua kama ule ni mtego. Alidhani Gafaranga ameasi kweli. Akampa siri zote. Gafaranga nae akazifikisha kwa Kagame.
Kagame akaongeza watu wawili nchini Afrika kusini. Watu hao Gafaranga aliwaingiza chumbani kwake na kuwaficha bafuni. Karegeya alipoingia wakaibuka kutoka bafuni na kumuua kabla ya kutokomea.
Na kwa kuwa walikua wanatumia majina bandia haikua rahisi kuwakamata. Walitoroka kwa barabara kwa kupitia mpaka wa Msumbiji na baadae Tanzania kisha Rwanda.
Hili liwe funzo kwetu hasa kwa vijana wanaofanya siasa za upinzani. Vijana wengi wa opposition nchini (hasa Chadema) hutokea sana kuwaamini watu kwa jina tu la "kamanda". Umekutana na mtu siku mbili anajiita Kamanda, unamuamini na kumpa siri zako. Kumbe mwenzio yupo kazini.
Wapo watu wa usalama wengi wanaovaa magwanda, wanashiriki mikutano ya chama, wanachangia chama, na wengine wanakuwa hadi viongozi wa chama lakini ni ma "agent" wapo kazini. Mtu anajiunga na chama chenu kutokea chama kingine, hata miezi miwili hana anapewa nafasi ya kugombea uongozi. Mnamuamini kiasi gani?
Usimuamini mtu kirahisi kwa kigezo tu cha ukamanda. Jipe muda wa kutosha kujiridhisha. Yupo mtu anaweza kuitukana serikali ukadhani ni mwenzio ukaungana nae, kumbe yeye ana kazi maalumu. Ukaingia mtegoni, ukanasa. Be careful.!
Kujifunza haya na mengine mengi tafuta kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI cha Yericko Nyerere. Kina madini mengi ya kujifunza. Ni kurasa 700 zilizosheheni. Kinapatikana kwa TZS 80,000/= tu. Wasiliana na Yericko kupitia 0715 865 544.
Picha chini ni Kanali Patrick Karegeya enzi akiwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Rwanda (NISS).