Tupigeni kura, wakichukua uongozi kwa nguvu ya dola hatutajuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupigeni kura, wakichukua uongozi kwa nguvu ya dola hatutajuta

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Oct 8, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Serikali ya Kikwete inaonyesha kila dalili za kuibaka demokrasia kwa kutumia nguvu ya dola. Ninayaona haya kutokana na matukio ya hivi karibuni.
  • Tamko la jeshi la wananchi (JWTZ) - hii ilikuwa na lengo la kuwachonganisha wapinzani kwa wapiga kura wasiokuwa na uelewa wa kutosha hasa wa vijijini kuwa ni wagomvi na wakipewa nchi wataitumbukiza katika migogoro kama walivyo majirani wetu.
  • Tafiti zisizokuwa na kichwa wala mkia - Matokeo ya utafiti yaliyotangazwa na REDET jana yana lengo la kuwakatisha tamaa wale wote wanaunga mkono upinzani kuwa wananchi wengi wa Tanzania bado wana imani na Kikwete na hivyo wao ni wachache sana hivyo kura zao hazitabadili matokeo ya mwisho ili wasipige kura, ama kura zikiibiwa wasishituke sana wajue kuwa waliowengi wanaunga mkono serikali kitu ambacho siyo kweli.
  • Taarifa za jeshi kuwa kuna dalili za kutokea machafuko zinaweza kutumika pia kuhalalisha kuwekwa amri ya jeshi kuwakataza watu kukaa jirani na vituo vya kupigia kura, hii itarahisisha wizi wa kura kwa kubadilisha karatasi za kupigia kura na kuwekwa zile wanazozitaka.
  Hata hivyo nawashauri wapiga kura wenzangu kuwa tupige kura kwa wengi wetu na tuwapelekee salamu kuwa hatuwataki, hata wakiiba nafsi zao zitawasuta kama ambavyo zimewasuta Zanzibar na kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa.

  Nawashauri pia kuwa tuzilinde kura zetu kwa njia ya kistaarabu ili kuwanyima fursa ya kuweka amri za kijeshi, hivyo kufanikisha zoezi la kuwatoa madarakani bila kumwaga tone la damu.

  Aluta Kontinua
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  CCM hawawezi kushinda uchaguzi kwa njia yoyote ile. Hii ni taarifa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.


  Soma hizo karama takatifu na kuzirudia siku ya uchaguzi halafu tuone CCM inatokea wapi mbele ya Mwenyezi Mungu.
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona Plsalms inamistari 5 pekee, naomba uangalia na uundike upya mkuu
   
 4. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I wish kila mmoja angekuwa na moyo kama huu
   
Loading...