kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,425
- 13,935
Dawa za kulevya ni janga la kimataifa, tupigane nalo kwa kutunga na kutekeleza sheria kali saana, sio kwa kubahatishabahatisha. Tisitegemee watu kutajwa na kutajana uwe msingi wa kupambana na dawa za kulevya bali uchunguzi wa kina, kisayansi na kisheria uwe ndo msingi wa vita dhidi ya madawa ya kulevya. Vinginevyo taifa litakorogeka na kuwapa wauza madawa mwanya wa kutokea. Dalili sio nzuri kwa sasa kutokana na wananchi, wabunge, watumishi wa Mungu na hata mawaziri wameanza kugawanyika kuhusu namna vita hii inavyopiganwa.q