Tupia Top 4 yako kwa msimu wa EPL wa 2018/19

Mtoa mada naomba nikukumbushe, EPL kuna kitu kinaitwa "Second season syndrome" yaani homa ya msimu wa pili.

Timu nyingi bingwa zinakumbwa na huu ugonjwa wa kushindwa kutetea taji kwa msimu unaofata. Zinakamiwa sana, halafu zinakumbana na ule uchovu wa kuchukua ligi msimu uliopita.

Ndio maana haishangazi kuona tunaenda mwaka wa 10 sasa hamna timu iliyotetea taji lake pale epl toka Man Utd ya Sir Alex ilivyofanya hivyo msimu wa 2008/2009.

Ila kwa upande mwingine sioni wa kumzuia Man City, maana Liverpool inayopewa na nafasi naona nao hawana bahati, wamekuwa ni wakimbiza mwenge tu.
Second season syndrome kwa City kama ulivyosema
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom