Tupia hapa: Ubabaishaji wa mabasi ya kwenda mikoani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupia hapa: Ubabaishaji wa mabasi ya kwenda mikoani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ozzie, Aug 5, 2012.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya sana, kwetu hakuna uwanja wa ndege; na hata kama ungekuwepo sijui kama ningeweza kumudu usafiri. Na ningemudu kusafiri naamini bado ningepata shida zilezile za Air Tanzania na Precision air.

  Zamani zile nikipata nafasi ya kwenda kusalimu wazazi, nilikuwa naenda KAMATA kupanda Scandinavia. Hawa hawakuwa wababaishaji, ila walipokufa nafasi yao imejazwa na magari UCHWARA kama SUMRY, Mbeya Express, n.k; ambayo yanajinyumbulisha kuwa yenye kiwango cha kufanana na Scandinavia Express; wakati hawatakuja kufikia chembe ya huduma waliyokuwa wakiitoa.

  Leo nilitakiwa niwe Safarini kwenda Mkoani. Nilikata ticket ya Mbeya Express Ijumaa hii. Lakini nimefika hapa Ubungo, jamaa wa Mbeya Express wanasema gari letu lina matatizo hivyo wanataka tupande SUMRY mbofumbofu. Wao wanaita 'kufaulisha'. Mimi nimekataa. Sasa 'naunda kamati' nifanye uamuzi wa kurudi nyumbani na begi zangu. Nashukuru wamerudisha nauli, ljapo haihusishi gharama za kunileta Ubungo Bus Terminal na kunirudisha nyumbani (ni kama elfu 40).

  Hii ni mara yangu ya sita kubadirishiwa gari. Mara ya mwisho ilikuwa wiki tatu zilizopita. Nilikata ticket gari ya SUMRY siku moja kabla ya kusafiri, siku ya pili nafika Ubungo wakasema gari haikurudi toka mkoani, hivyo wakanipandisha kwenye gari iitwayo TAQWA. Shida nilizopata kwenye gari hiyo, zimenifanya leo nisikubali 'kufaulishwa'.

  Hivi haya magari kwanini wana huduma mbovu kiasi hiki? Hakuna mshindani anayeweza kuja? Au waje wadhungu pia wawekeze wawafundishe waswahili adabu? Na kwanini wakatishe abiria ticket ilhali wakijua hawatakuwa na gari? Na wengine huwa wanadanganya, wanajifanya gari kama imeharibika kumbe itakuwa walikuandikia muda usio sahihi ili pindi utakapofika wakupakie kwenye gari lingine, na hivyo kutopoteza pesa yako.
  INAUDHI SANA.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kuna tetesi kuwa usafiri wa treni unarudi kwa kasi...... POLE SANA KWA YALIYOKUKUTA
   
 3. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sumry ni kati ya kampuni za usafirishaji zenye ubabaishaji wa hali ya juu,kwa experince yangu sintokaa nipande mabasi yao na si mshauri yeyote kupanda
   
 4. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duh.....pole mkuu...
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tabia za mabasi ya Sumry sawa na mmiliki wake.
   
 6. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi sitaki hata kulisikia hili jina la Sumry maana jumamosi ya wiki iliyopita nilisafiri na moja ya basi lake kutoka Mbeya saa Moja Kasorobo asubuhi lakini cha kushangaza Basi lilifika Dar saa tatu asubuhi siku ya jumapili kutokana na kuharibika njiani. Halafu mmiliki anayanadi mabasi yake kwa jina la "Sumry High Class" badala ya "Sumry Low Class"
   
 7. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nimeona malalamiko mengi yanatoka pande za mbeya,sumbawanga na mikoa jirani huko.Pande za kwetu Kaskazini naona tatizo sio kubwa Kama lenu huko sasa sijui wawekezaji wanapaogopa kuwekeza huko au nini.Manake hadi bungeni nilimsikia mama mmoja mbunge akilalamika ila poleni kwa yanayowakumba
   
 8. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Mwaka 2010 narud tabora toka dsm nilikata mabruk kufika ubungo naambia mabruck bov so wakanfaulsha kwny nabel la khm dah
   
 9. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  kizaazaa kingne nilipanda muro kufika kizengi(tbr) likaroga aisee tulilala pal sikunzima ndo wakatupa buk10 tukapand nbs
   
 10. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ila kiukweli kwa kule tabora-dsm,nbs wanajitahidi sana kutoa huduma bora zisizo na ubabaishaji!
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nilipanda sumry toka mbeya kuja dar, tukasimamishwa Inyala eeti gari haina insurance tulikaa zaidi ya saan 2 tunasubiria. GARI HAZIFAI HIZO!
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nikiona magari ya Sumry/Hekima huwa nafumba macho. Hayafai, panda kama safari haikupangwa, ni ya ghafla au kuna dharula ya kufa mtu, vinginevyo utaliaaa.
   
Loading...