Tupeni tathmini, upepo wa ushindi CHADEMA ukoje katika kata hizi?

Kata ya Mpwapwa mjini Chadema jana ilifunika mbaya nipo njiani kutuma thread mpya na picha zenye kuonesha matukio muhimu. Naibu waziri Viwanda ambaye ni mbunge ahaha asema hajawahi kuona upinzani Mpwapwa ktk maisha yake. Asema kinaganaga ameshitushwa sana na aliyoyaona. Kamanda Mnyika aliongoza harakati hizo za mapinduzi Mpwapwa ambapo madiwani wote ni CCM
 
tatizo hawa madiwan we2 wanarubuniwa na fedha za ccm kuachia kiti,nnachoomba kweli kama mabdliko bsi tujitolee kwa hali na mali .ukomboz si lelemama,naomba watunz wa riwaya waanze kutunga riwaya za ukombozi tanzania baada ya uhuru.watanzania wasome vitabu kama harakat za ukomboz,morani.
 
Kaka Nanyaro, mie sina shaka na Arusha; wasiwasi wangu ni huko kwingine. Tunasikia CHADEMA wamesimamisha mwizi kata ya Mwawaza Shinyanga, bado hakuna jibu la maana kutoka kwa wahusika.

Arusha ina kata mbili, hali ikoje katika kata nyingine 27?

ww usilete ishu za magamba humu ndani....thibitisha kama ni mwizi, au lini alikuibia..... Kama umetumwa kuchafua watu huku syo paalah pake, nenda kaungane na lusinde na chemba mporomoshe mijitusi yenu hko....
 
kilala kheri cdm kakatika uchaguz nawatakia mafanikio makubwa na ushindi mnono....tupo nyuma yenu kwa lolote baya au zuri...
 
Tuzidi kumwomba Mungu chaguzi ziishe kwa amani,maana magamba wana kila hila mbaya kwa ajili ya kutetea ushindi.
 
Tuzidi kumwomba Mungu chaguzi ziishe kwa amani,maana magamba wana kila hila mbaya kwa ajili ya kutetea ushindi.

Mimetonywa kwamba huko Songea jana hali ilikuwa tete nakuzua tafrani kubwa hadi wapiganaji watatu wa CDM kuumizwa vibaya kwa mapanga navijana wanaosadikika kuwa ni gre/guards. Kwasasa majeruhi wote wako hospitali.
 
Kaka sikia nikuambie CHADEMA ni Arusha mjini, Moshi Mjini,labda Mbeya Mjini kwine hakuna kitu. Wanataka kuwaaminisha wananchi tu lakini bado hawajajipanga. Wakipata ka kata kamoja basi kelele hizo.

NB: Hawawezi kuchangia thread hii maana iko direct.

Nisingependa sana kuamini hili, katika pita pita zangu na shughuli zangu za vijijini, jana tarehe 27/10/2012, nilikuwa maeneo ya wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, Pale kata ya Miyenze nilikuta akina Dr. Slaa, Mh. Kasulumbayi (MB) wakihitimsha kampeni zao za udiwani, Honestly, mwamko wa wapiga kura ni mkubwa sana. Ujue pia maeneo yale yanapakana na wilaya Ya Igunga (upande wa kaskazini-mashariki), ambako pia mchuano kati ya CCM na CDM unakuwa mkubwa sana. Kwa hali niliyoiona jana, Unaweza kutegemea lolote baada ya dakika 90. Najua idadi ya watu kwenye mikutano SI HOJA SANA, LAKINI NILIWAONA pia akini Juma Ntimizi wa CCM-TABORA maeneo hayo hayo wakishawishi wapiga kura kwa mbinu mbali mbali. Kwa jicho langu kama mpita njia niliweza kulinganisha hamasa ya wapiga kura katika ile mikutano miwili .... Mh, any thing can happen my brothers. Upande wa pili, kule wilaya ya sikonge, kata za Kiloleli na Ipole, Nilichelewa mikutano, lakini ukisikiliza wapiga kura wenyewe wanakiri mvutano mkubwa upo, tena kati ya vyama vitatu ( CCM, CUF na CDM), CUF wana advantage kwa kata ya Ipole, kwasababu kata hiyo inapakana na kata ya Chabutwa ambapo paliwahi kuwa na diwani wa CUF miaka ya nyuma (sijui kwa sasa). labda nikuambie tu Annael (Ndugu yangu) vuguvugu la mabadiliko siyo kitu cha siku moja, na wachambuzi wa mambo ya siasa wanaenda mbali kidogo zaidi ya kushinda "kakata kamoja" kama ulivyosema. Hata kama chama kikishindwa kwasababu moja au nyingine, tunaangalia pia mwamko wa wananchi generally, Je inaleta picha gani kwa miaka kadhaa ijayo ? Elimu ya uraia, inaongezeka au inapungua ? Ule mpishano mdogo wa idadi ya kura ni kigezo kimoja tu ambacho hatuwezi kukipuuza, maana hata timu mbili zikicheza au zikiwa na uwezo unaolingana, MWISHO WA SIKU PATATAKIWA MMOJA TU NDIO AWE MSHINDI. Na siasa ni hivyo hivyo !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom