kalibu xana njombe
Safi sana, najiandaa kuzama njombe
Safi sana, najiandaa kuzama njombe
Naam,
Fedha inatokana na shughuli yenyewe. Huwa naanda vitalu vya miche, nauza miche mingi, faida nanunulia mashamba na kuendeleza, kwa hiyo ni uwekezaji unaojiendesha wenyewe. mwanzo nilikuwa nanunua vimisitu vidogo nafuga, akija mteja napiga bei, kwa hiyo vikaniinua sana. Huku nina miche na kule kamsitu kamepata mteja, basi siku zinasonga.
Niko njombe pia napiga parachichi. Nimeangukia pua mara mbili kwenye parachichi, yaaani miche ilikufa sana. Nikagundua miche ya bei rahisi ni hasara. Sasa hivi natumia miche ya bei mbaya, haifi.
Kule Lutukira niliangukia pua kwenye Tangawizi, ile namalizia camping, bei ikashuka vibaya nikaondoka fasta.
vp mkuu heka ya miti yenye miaka 2-3 huwa unauzaje/wanauzaje na mm mwaka huu nataka niingie hukoNaam,
Fedha inatokana na shughuli yenyewe. Huwa naanda vitalu vya miche, nauza miche mingi, faida nanunulia mashamba na kuendeleza, kwa hiyo ni uwekezaji unaojiendesha wenyewe. mwanzo nilikuwa nanunua vimisitu vidogo nafuga, akija mteja napiga bei, kwa hiyo vikaniinua sana. Huku nina miche na kule kamsitu kamepata mteja, basi siku zinasonga.
Niko njombe pia napiga parachichi. Nimeangukia pua mara mbili kwenye parachichi, yaaani miche ilikufa sana. Nikagundua miche ya bei rahisi ni hasara. Sasa hivi natumia miche ya bei mbaya, haifi.
Kule Lutukira niliangukia pua kwenye Tangawizi, ile namalizia camping, bei ikashuka vibaya nikaondoka fasta.
Mimi sio muuzaji wa miti chini ya miaka 15. Halafu bei sio uniform na wakati mwingine bei huwa inaathiriwa na shida za muuzaji hasa kwa miti midogo. Mapanda sasa hivi wanauza Tsh 1.5M mpaka 2.5M kwa eka kwa miti ya umri huo.vp mkuu heka ya miti yenye miaka 2-3 huwa unauzaje/wanauzaje na mm mwaka huu nataka niingie huko
Pines huwa nauza Tsh 80/ na mlingoti Tsh 100/unauza bei gan mche wa paina na milongoti
Mlachake bado uko Iringa mkuu?
Mimi huwa naweka mpaka 40 meters, lakini moto wenye Kimbunga huwa unavuka.Kuna kitu wanaita fireline, yaani unaacha kama hatua kumi au ishirini kutoka kwa shamba la jirani
Safi sana man. Iringa nilihama tango 2012 nipo huku kwa wazaramoMlachake bado uko Iringa mkuu?
Kanyagio bado tuko wote sana. Tulipofanya yetu Mufindi tukahamia Njombe pamoja. Bado tunakimbiza miti ya mbao. Baadae tukaenda wote Mkuranga kule. Sio muda mrefu atavuna kitu cha ukweli pande za Mufindi.
poa, miye niko kwa Wamakonde huku.Safi sana man. Iringa nilihama tango 2012 nipo huku kwa wazaramo
Muhimu sana ukatie bima. Mimi nilikuwa nimepanda heka 100. Miti ilikuwa na miaka 6. Na nilipanda miti ya malawi ya miaka 10 unavuna. Lakini mwaka jana mwezi wa 8 hapo shamba lote liliungua moto. Kuna wajinga walikuwa wanagombania shamba la urithi,mmojawao akaamua kulichoma hilo shamba,ambalo lilikuwa umbali kama wa mita 500 kutoka shambani kwangu. Mashamba mengi sana yaliungua. Wakati linaungua shamba langu nilikuwa kwenye proces ya kukatia bima. Lakini mwaka huu nafanya mpango nipande parachichi. Mwisho miti inalipa saaaaana. Lakini nakushauri kama ndio unataka kuanza kuwekeza huko kwenye miti. Panda parachichi mkuu. Miaka mi3 unaanza kuvuna. Na soko lipo kubwa sana,kuna kiwanda kimefunguliwa na rais juzi kati kiko Rungwe mbeya. Kuna kiwanda kinajengwa njombe. Kuna soko liko Italy. Panda parachichi mkuu
Uko njombe sehem ganPines huwa nauza Tsh 80/ na mlingoti Tsh 100/
Niko itipura. Moto ulikowaka mwaka janaUko njombe sehem gan
Niko itipura. Moto ulikowaka mwaka jana
LupembeUko njombe sehem gan
Ule uliokula mpaka miti ya jimbo kuu la njombe ulilamba na yako pia? Mi shamba moja lilipona kimiujiza aisee. ule moto ndo uliishia kwenye shamba langu.njia ya kwenda songea
Kwa nini unalazimika kurudia neno changamoto mara nyingi hivyo mkuu ? Ungeandika tu 'zipo changamoto zifuatazo' halafu ukazitaja tu moja moja.Changamoto ya kwanza ni ardhi salama kwa kilimo hiki.
Changamoto ya pili ni manpower kwa ujumla wake
Changamoto ya tatu ni sera za nchi yetu
Changamoto ya nne ni miundombinu isiyo rafiki sehemu zenye ardhi nzuri na salama.
Changamoto ya tano ni hujuma inayotokana na sbb nyingi
Changamoto ya mwisho kipato kuyumba kwa wawekezaji.
Nilikuwa nimepiga cha Makambako, nisamehe bureKwa nini unalazimika kurudia neno changamoto mara nyingi hivyo mkuu ? Ungeandika tu 'zipo changamoto zifuatazo' halafu ukazitaja tu moja moja.