Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

Unatakiwa kufanya palizi angalau mara 2 kwa mwaka (Kuna kuchomeana mashamba) na miti ikue vizuri, pia Kuna pruning kila mwaka bei inategemea mahali ulipo. Jumla palizi 30 kwa miaka 15

Kuhudumia shamba kwa miaka 15 bila kuingiza hata shilingi ni rubbish. Mfano njombe/iringa shamba la miti yenye miaka 7 na ardhi wanauza 3-6m, miaka 3-4 laki 5-7
Wewe ni muongo sana! Hivi miti yenye miaka 3 unapalilia?

Tuulize tuliotoka iringa miti inapandwaje na inakia vipi
 
Iringa miti ukipanda hakuna palizi labda ikifikia miaka 4 unaanza kufanya prooning na sio kupalilia.
 
Yah reasoning yako inamantiki mkuu,vipi lakini,ulishawahi kuwekeza kwenye miti?
Uwekezaji wa miti kwangu mimi hauna tija, unahudumia shamba miaka zaidi ya 10 halafu unakuja kuuza mti kwa sh 20,000 na unapoukata inabidi upande mwingine na kuja kuvuna tena miaka 10 ijayo so elfu 40 kwa miaka 20.

Fanya kilimo cha miti ya matunda hutajuta mfano mchungwa mmoja hata ukiuza chungwa 300 kwa sh 50 = 15000 so kwa miaka 10 = 15,000*7= 105,000/=
Huo Mchungwa mmoja wa kutoa matunda 300 ni upi?

Halafu miti ya machungwa inakaa mingapi kwenye heka moja? Vs Miti ya Mbao nayo inakaa mingapi kwenye heka moja?

Mwisho huku mitaani tunanunua mpaka 50/- kwa chungwa moja, means huko Shamba ni pungufu ya hiyo
 
Iringa miti ukipanda hakuna palizi labda ikifikia miaka 4 unaanza kufanya prooning na sio kupalilia.
Mkuu, nitaleta picha nikienda shambani zinaoonesha shamba lililo pandwa miti, paliliwa/fyekwa mwezi wa 12. Na picha za mfano wa mashamba safi ya njombe. Huku ukiacha kichaka umekaribisha moto Kama wachangiaji wengi walivyoeleza juu
 
Huo Mchungwa mmoja wa kutoa matunda 300 ni upi?

Halafu miti ya machungwa inakaa mingapi kwenye heka moja? Vs Miti ya Mbao nayo inakaa mingapi kwenye heka moja?

Mwisho huku mitaani tunanunua mpaka 50/- kwa chungwa moja, means huko Shamba ni pungufu ya hiyo
Spacing hilo ni somo refu sana. Nimetumia mchungwa kama mfano tu wa mazao ya muda mrefu embe, mchungwa/citrus nyingine 150, parachichi/macadamia 75, papaya 650. Miti inategemea na aina 2.5*3 etc
 
Ndio nimeifanya, ninafahamu bei ya mti shambani na gharama za kutunza shamba kwa miaka yote mpaka kuja kuvuna. Hii sio biashara kwangu mimi
HII BIASHARA NDIO IMEMPA MKINGA NGUVU YA KUMUONDOA MWARABU KARIAKOO,TATIZO WATU WANAANGALIA HATUA MOJA MBELE.
 
hamjambo humu,

Hii ndio miezi ya balaa kwa wawekezaji wa misitu. Ukisikia simu toka shambani unahisi kufa kufa hivi.
Malila ulini- inspire sana kny miti bless up, moto ni changamoto kubwa sana lakini mapambano yanasonga mbele.
 
Umenigusa, nimeishapigiwa mara tatu. we acha tu
Duuh pole,
Jirani yangu anapumulia mashine, moto umelipuka shambani kwake, mimi jasho linanitoka bila kujali niko ndani ya kiyoyozi. Nimetuma madogo wakamsaidie jirani.
 
Malila ulini- inspire sana kny miti bless up, moto ni changamoto kubwa sana lakini mapambano yanasonga mbele.
Daah, Hongera sana.
Mimi bado naotesha kama sina akili nzuri. Ujio wa Mchina pale Mafinga, miti itakuwa almas sana siku chache zinazokuja. Please go on.
 
Unatakiwa kufanya palizi angalau mara 2 kwa mwaka (Kuna kuchomeana mashamba) na miti ikue vizuri, pia Kuna pruning kila mwaka bei inategemea mahali ulipo. Jumla palizi 30 kwa miaka 15

Kuhudumia shamba kwa miaka 15 bila kuingiza hata shilingi ni rubbish. Mfano njombe/iringa shamba la miti yenye miaka 7 na ardhi wanauza 3-6m, miaka 3-4 laki 5-7
Sasa mkuu huoni kama nikinunua shamba lenye miti ya miaka 3-4 kwa laki 5-7 then baada ya miaka mitatu nikaliuza kwa mil 3-6, huoni kama ni faida nzuri nikitoa gharama ya palizi kwa miaka hiyo mitatu?
 
Mkuu miti ya umri huo eka ngapi ndo inauzwa kwa bei uliyoiweka hapo?
 
Ushuhuda: Baada ya kufuatilia kilimo cha miti kupitia humu JF niliamua kujilipua na Mikaratusi, nilipanda 2016 kwa sasa ina miaka 3, mikaratusi inakimbia jamani huwezi amini, hapa nafikiria kuvuna nguzo niwauzie watu wa Cable Tv's.
 
Tatizo lako una panda ekari 2 . Miti ukitaka udaidi panda kuanzia ekari 50.

Imagine 50×400= unakua na miti 20000.

20,000x20000= 400,000,000

Hii ina maana kila baada ya miaka 10 unavuna mil 400
Uwekezaji wa miti kwangu mimi hauna tija, unahudumia shamba miaka zaidi ya 10 halafu unakuja kuuza mti kwa sh 20,000 na unapoukata inabidi upande mwingine na kuja kuvuna tena miaka 10 ijayo so elfu 40 kwa miaka 20.

Fanya kilimo cha miti ya matunda hutajuta mfano mchungwa mmoja hata ukiuza chungwa 300 kwa sh 50 = 15000 so kwa miaka 10 = 15,000*7= 105,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom