Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

njia ya kwenda songea
Ndio njia kwenda songea. Tunaingilia pale kuna kibao cha frank yule aliwatika miche ya parachichi pale barabarani na kule ndani karibu na magereza ana shamba kubwa la maparachichi,nafikiri tayari ana soko Italy
 
Nilipoamua kuingia kwenye hii game nilianza na eka moja na nusu kule Kilolo, Mheshimiwa Mbunge Mwamoto alinipa msaada mpaka kufika kile kijiji na nikapata shamba eka moja na nusu kwa Tsh 22,000/. Nikaagiza hela jamaa wanioteshee, hawakuotesha lote, msimu uliofuata nikakaza buti mwenyewe, nikamalizia kipande, yaani miaka miwili nikaotesha eka moja na nusu.
Wakati wote nilikuwa nasoma game kwa madogo na wenyeji. Nilipolijua game, nikawatimulia vumbi kwa speed ya 120km/h. Imebaki historia pale kijijini. Huwa nawapitia siku nikienda kukagua misitu, basi kukiwepo maji tunakunywa.
Mkuu Mwaka Gani Vile :)
 
Ushauri wangu Ni kuwaa wawekezeeni watoto wenu wenye miaka 1-15 wao wakifika miaka 36 watawakumbuka sana so msipande kwaajili yenu
 
Mi ni mmoja wa washawishi wa kilimo cha miti na parachichi.Changamoto niliokutana nayo ni MOTO.shamba langu la miaka 4liliungua moto mwaka jana, mashamba mengine yanaendelea vizuri.kuna gharama za kutengeneza njia za kuzuia moto kila mwaka.haipungui lak3 kwa heka 10.kila mwaka.
Nimegundua kwamba kama shamba lipo barabarani milingoti ni mizuri zaidi inavumilia moto kuliko paini.
 
Hongera sana, naona mambo ya fedha yamekunyookea mpaka kufanya uwekezaji huu.

Mimi nimesitisha shughuli zangu zote na sasa nipo kwenye kilimo mazima 100%. Kuna potential kubwa sana huku iwapo utapata access ya masoko na bei za uhakika. Njombe, iringa, mbeya neema imefunguka tushindwe wenyewe
Kweli mkuu, ila watu ni walalamishi tu.njombe ardhi bado ipo kubwa tu ni nguvu zako tu.Siku hizi wameingia wapemba na kusomba mikaa bado mtu umekaa unalalana hakuna ajira.
 
Hii inategemeana na unapoishi. Hiyo bei ni miti ya Iringa

Kuna sehemu, kuna miti inaitwa mburumatare (sijui hili jina ni common maeneo yote au laa), hii miti baada ya miaka 5 unavuna na mti mmoja unauza kati ya Tsh 50-70 elfu. Hapo bado unabaki na mabanzi na kuni ambazo pia unaweza kuziuza. Hivyo hiyo biashara si kichaa kama wengine wanavyodhani

Uzuri wa hiyo miti, ukikata, unachipuka mwingine ambao Baada ya miaka 5 mwingine unaweza kuuza tena kwa kati ya Tsh 50-70

Wazo la kupanda miti ya matunda pia ni wazo zuri, kwani ukipanda miti ya matunda ya asili kama miparachichi unaweza kuvuna hata kwa miaka 10 (mazao yakiwa mengi katika peak yake)

Uzuri wa biashara ya miti, ukipanda ikikaa ndani ya miaka 2 bila kusumbuliwa, unaendelea na mambo mengine huku shamba lako likiendelea kukutengenezea utajiri
Melia azedaracht

Ni jamii ya muarobaini
 
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
Chanzo ilikuwa nini mkuu?
 
Uko vizuri,
Nilipokuwa chuo, niliotesha miti 250 tu nyumbani kwetu, sasa hivi nasumbuliwa mno. Nimewaambia ile nimeiacha kwa ajili ya dharula maana ni hela kiganjani sio benki ukute ni jumamosi hawafungui, yaani nikiinua simu tu, mpunga ndani maana ndo imebaki hiyo tu iliyokomaa. Kila siku Wachina wa Mafinga wanapitia vimisitu vyetu kupitia madalali wao, nasema bado sana. Jirani yangu juzi kavuta mpunga wa maana pale Mapanda, kauza kwa mchina vigogo, miye bado kwanza.
Inaumri gani hii miti?
 
Kila biashara ina changamoto zake. Ila binafsi niseme yafuatayo.
1. Kuwekeza kwenye Kilimo cha miti kinafaa sana kwa mtu mwenye malengo ya mda mrefu.
2. Kwa wale wanaotokea mikoa yenye ardhi hasa za urithi haihitaji mtaji bali nguvu yako tu inatosha. Miche unawatika mwenyewe, mashimo unachimba mwenyewe na kupanda, kuzuia moto utafanya mwenyewe na prooning fanya mwenyewe.
3. Faida ya kuwekeza kwenye miti ni kubwa kuliko hasara na vijana wengi kutoka iringa, njombe, nk waliojielewa mapema mambo yako njema.
4. Kwa ambao hawana mashamba ya urithi bei ya eka moja ni 150000-200000 hivyo ukiamua kufanya hiyo biashara fanya kila mwaka panda eka ya miti kwa mtaji mdogo

Ushuhuda wa kweli mimi nikiwa a,level mwaka 2009 nilianza kupanda miti na nilifanya hivyo miaka yote iliyofuata hadi namaliza chuo kikuu mwaka 2014 nilikuwa na miti zaidi ya eka 15 na hadi sasa naendelea kupanda miti kwa kwa juhudi kubwa sana. Na miti yangu hadi sasa inatosha kupasuliwa na ni mikubwa sana tu. Ninavyoongea hadi sasa naweza kuuza zaidi ya 60+mlns ya pesa.

Nishauri tu vijana wenzangu kuna haja ya kuamua unataka baadae uwe na uchumi wa aina gani na uitwe nani. Amka sasa na ufikirie ardhi ya kijijini kwenu au ya familia bado ipo iddle kabisa nenda ikakupe matunda ya maisha ili baadae uitwe majina tofauti ya udon
Hizi bei za mashamba ulizoweka hapa ni za kununua shamba na kulimiliki kabisa au kukodisha tuu?
 
Ku prone, kuna watu wengi wanataka kuni mkuu, kwanini kwako iwe gharama

Kwanini utoe hela mfukoni, wakati unacho prone chenyewe ni mali
Pande za iringa, njombe kuni ni bwerereee, hata mabanzi wanajibebea bure. Mikoa mingine sawa
 
Back
Top Bottom