Tupende vy Nyumbani; Hii brand inatengenezwa kwa umahiri mkubwa sana, Karibuni sana!!

mKUU umenikumbusha mbali miaka ya 70 mwishoni na 80mwanzoni. Nimeitengeneza hii kitu kupata hela za kulipia mahitaji shule. Ndugu tunatoka mbali!!!!
Hii mitambo kiboko wengine imetukuza maeneo ya mto manchira wazee wetu walikuwa na vijiwe vyao pale vya kuhifadhia hiyo mitambo na kuzalisha hiyo kitu! lol
 
Mkuu umenikumbusha mbali...! Hii kitu ndo imenisomesha, hongera mama mnafanya kazi kubwa kutulea
dscf0310.jpg


Enzi zilizopita kidogo mama ntilie hawakuwepo, biashara hakika ambayo watoto tuliokulia mazingira ya kimaskini ambao ndio wengi wetu hapa tumesomeshwa kwa hii stile ya kiuchumi ambayo mama zetu walijitahidi kufa na kupona hadi leo tumefikia tulipo. Tungejaribu kufanya utafiti tutashangaa wengi tu tumesomeshwa kwa kutegemea hii mikorogo ya komoni iuzwayo vilabuni. Asante mleta mada kwa kuturudisha tulikotoka.
 
Back
Top Bottom