Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

Status
Not open for further replies.

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,277
4,682
Kwa kuwa Katiba ya Tanzania ya 1977 inaniruhusu kutoa maoni yangu alimradi sivunji sheria, na kwa kuwa slogan/ motto/ kaulimbiu ya JF ni "where we dare to talk openly", basi napenda kusema haya yafuatayo.

Nimekuwa nafuatilia kwa kina mjadala wa Mahakama ya Kadhi na mambo ya udini kwa ujumla katika nchi yetu. Wengi wanadai kuwa Tanzania ni secular state, haina dini. Pia kuwa haipaswi kuchanganya dini na siasa katika utawala wa nchi kwani madhara yake yanafahamika.

Sawa, haya ni maoni na hoja za watu mbalimbali. Lakini mimi nataka kujua swala moja, wanasema Tanzania haina dini, je ni kwa nini katika orodha ya sikukuu zinazotambuliwa rasmi kiserikali kuna Idd, Krismas, Pasaka, etc? Hizi ninavyojua ni sherehe za zile dini zinazoitwa za "kweli",i.e Uislamu na Ukristo.

Na pia katika sherehe hizi, viongozi wa kitaifa hualikwa na kuhutubia as if wako katika shughuli za kitaifa. Sasa inakuwaje serikali ya Tanzania haiizitambui sherehe kama Diwali za wahindu au zile zetu sisi tunaoitwa "wapagani"?

Ni lini na ni wapi Serikali yetu hii imewahi kuingilia kati udhalilishaji wa dini yetu "wapagani" ambao kila siku tunatukanwa kuwa tunaabudu mashetani na hao wakristo na waislamu? Kuna mhubiri mmoja wa Kiislamu aliwahi kushtakiwa Mahakama Kuu aliposema Yesu si Mungu, na likawa zogo la kitaifa, lakini sijawahi kusikia serikali hii hii imeingilia kati kuhusu udhalilishaji wa wazi wa imani zetu za jadi na hao watu wa dini za "kweli".

Pili, viongozi wa kitaifa wanapowaita viongozi wa "dini" sijawahi kuona Mwanamalundi au Nyunguyamawe wakiwa pale Ikulu na ngozi na manyoya yao na singa zao mikononi zaidi ya kina Askofu fulani na Shehe fulani. Hii inaashiria nini kwa wale wanaodai kuwa Tanzania haina udini? Ina maana kina Mngungwa mwa Mnyenyelwa sio viongozi wa "dini"?

Tatu, katika "documents" zote za Kiserikali zinazohitaji sahihi au uthibitisho toka kwa viongozi wa dini sijawahi kuona cheo cha "mfumu" zaidi ya "padre", "imamu/sheikh", "mchungaji", na maneno kama hayo (rejea fomu za kuomba mikopo bodi ya elimu ya juu). Sasa kwa mtu kama mimi ninayeambiwa naabudu "mashetani" wapi serikali inanitambua katika hizo documents zake?

Nne, katika mijadala yote na makongamano ya kitaifa yanayohusisha viongozi wa dini nai lini kina sie tuliwahi kufuatwa na kuitwa? Je, kina Pengo watakubali kukaa meza moja na sisi tunaoabudu "mizimu" ili tujadiliane masuala ya Taifa letu?

Inavyoonekana, ukiongelea dini hapa Tanzania unamaanisha Uislamu na Ukristo. Hata huu mjadala wa Mahakama ya kadhi, wahusika wakuu wa malumbano ni hao hao. Sisi tukiamka kuchangia tuaambiwa "wapagani" na waabudu "mizimu" na "uchawi" hivyo hatuna "locus standi" ya kuongea!!

Ukweli ni kuwa Tanzania ni nchi ya dini "kuu" mbili, Uislamu na Ukristo. Ndo maana hata katika kufanya maamuzi mengi ya kitaifa wataitwa mashehe na mapadre/ wachungaji kuwakilisha upande wa kidini. Waislamu na wakristo wamefaidi rasilimali nyingi tu za nchi hii at the expense ya watu wa dini nyingine (mf. majengo ya TANESCO Morogoro kutumika kwa ajili ya chuo kikuu cha Kiislamu). Najua baadhi yenu humu mtaudhika na ukweli huu, kuwa nina "pepo" na kuwa "nishindwe na nilegee"!!!

Yapo mengi tu ya kuweza kuthibitisha kuwa nchi hii ni ya kidini na hizo dini zinafahamika.

Hivyo for any critical observer (ambaye ataweka upenzi wa kidini pembeni, Koba you get me?) ataniunga mkono kuhusu issue hii, unless aamue kufumba macho na kuita nyekundu kuwa nyeupe iliyopitiliza rangi!!!

NB:Kinachonisikitisha zaidi hizi dini "kuu" 2 ni za nje,sio zetu Waafrika na zimetumika katika maouvu yote ambayo historia ya dunia hii imeshuhudia: utumwa, ukoloni, ubepari, ukandamizaji, mauaji (kama ya wale wahindi wekundu kule Amerika ya kusini yaliyofanywa na wamisionari wa kikatoliki wa Kireno), vita vya kidini (crusades),n.k...

Tulimkosea nini Mungu sisi watu weusi?
 
Ninakuunga mkono kwa hoja yako hii ibambasi. Mimi natamani sana serikali yetu ingejiondoa kabisa kwenye mambohaya ya kidini moja kwa moja, sio tu hizi dini ngeni tulizoletewa eti kustaarabishwa, bali hata hizo dini zetu wenyewe za asili zisiingizwe kabisa kwenye utendaji na maamuzi ya serikali.

Ukweli sasa ni kwamba ni unafiki tu wa viongozi na sisi wenyewe wananchi wa kuamini eti serikali yetu au vyama vyetu havina udini. Huu ni upuuzi mtupu (people are in self denial even when every evidence shows that we're sitting on a religious time bomb).
Mbaya zaidi ni kuwa hatuna viongozi sasa wa kitaifa wanaoweza kusimama na kuwazungumzia wananchi kama waTanzania kwanza zaidi ya kingine chochote. UtTanzania sasa unakuja katika nafasi ya tatu katika orodha kama hii:
1. Utafutaji wa mali (fedha), hata kama ni kwa kutoa roho za wengine
2. Udini - kila mwenye dini yake, hasa hao wenye dini kubwa
3. uTanzania, n.k.

Ni lini tena tutaanza kujisikia vizuri zaidi kwa kujua kuwa sisi sote ni waTanzania, kwanza, kabla ya mengine haya? Pengine hili halitatokea tena milele!

Kuhusu dini yako ya asili ibambasi (Upagani)- itabidi wewe na wenzio mnaoamini dini hizo nanyi muanze kutembelea chumba cha "MAELEZO" mara kwa mara kama hawa waTanzania wenzetu wenye dini zao wanavyofanya. Kadri ya makelele yenu mengi mtakavyoyafanya, ndio kadri ya serikali yenu itakavyoanza kuwakumbatia na kuwapa 'haki' zenu. Na sisi wengine tusioamini dini yoyote ile, nadhani wakati umefika na sisi kuanza kupiga kelele na mayowe.
Tutaangalia ni vipi serikali yetu hii itakavyotupatia haki zetu pia, ikiwa ni pamoja na kutotumia kodi zetu kwa kusherehekea au kuendeleza shughuli za hizi dini zenu.
 
Waislamu, Wakiristu na Wahindu ktk sherehe zao wanawaalika viongozi wa serikali na ni dini zilizo andikishwa rasmi na mahala pao pa kuabudia panajulikana ama ni msikiti, kanisa au temple la wahindu!

Sasa kama nyinyi wachawi na waabudu mizimu kama ofisi zenu huwa kwenye giza au makaburini mutatambulika vipi? na lini muliwaalika viongozi wa Serikali ktk matambiko yenu wakakataa kuhunduriya? au lini mulipeleka maombi ya kusajiliwa mukakataliwa?

Waswahili husema usione vyaeleya vimeundwa! Wakiristo na Waislamu wanawafuasi wengi TZ kwasababu ya kujitangaza na kuonyesha uzuri wa dini zao ndio maana wanatambulika!

Ndugu zetu Wapagani au Wa Tanzania wenzetu mimi nawashauri kama munataka kuhudhuria ktk hafla za Kiserikali na mutambulike basi muji-organize kwanza, mujulikane muko wapi, ofisi zenu ziko wapi, wafuasi wenu ni wangapi na mujiandikishe rasmi Serikali kwa kuonyesha nani kiongozi wenu, halafu pia munaweza kupewa misaada toka Serikalini!
Je, wanao abudu Jua, nyoka, mamba, Shetani, Simba, Mizimu nk. ni dini moja au ni tofauti? tukiwa tunalalamika tu bila ya kujitambulisha na kuwaalika wa Tanzania wenzenu ktk dini zenu ni lini mutatambulika?
 
Waislamu, Wakiristu na Wahindu ktk sherehe zao wanawaalika viongozi wa serikali na ni dini zilizo andikishwa rasmi na mahala pao pa kuabudia panajulikana ama ni msikiti, kanisa au temple la wahindu!

Sasa kama nyinyi wachawi na waabudu mizimu kama ofisi zenu huwa kwenye giza au makaburini mutatambulika vipi? na lini muliwaalika viongozi wa Serikali ktk matambiko yenu wakakataa kuhunduriya? au lini mulipeleka maombi ya kusajiliwa mukakataliwa?

Waswahili husema usione vyaeleya vimeundwa! Wakiristo na Waislamu wanawafuasi wengi TZ kwasababu ya kujitangaza na kuonyesha uzuri wa dini zao ndio maana wanatambulika! CCM inawafuasi wengi TZ kwasababu ilijitangaza ktk kila pembe ya nchi lakini angalia vyama kama TADEA,NRA,UMD,DP, nk. vimebaki kudorora DAR bila ya kuhangaika kutafuta wanachama! sasa vitatambulikaje?

Ndugu zetu Wapagani au Wa Tanzania wenzetu mimi nawashauri kama munataka kuhudhuria ktk hafla za Kiserikali na mutambulike basi muji-organize kwanza, mujulikane muko wapi, ofisi zenu ziko wapi, wafuasi wenu ni wangapi na mujiandikishe rasmi Serikali kwa kuonyesha nani kiongozi wenu, halafu pia munaweza kupewa misaada toka Serikalini!
Jee, wanao abudu Jua, nyoka, mamba, Shetani, Simba, Mizimu nk. ni dini moja au ni tofauti? tukiwa tunalalamika tu bila ya kujitambulisha na kuwaalika wa Tanzania wenzenu ktk dini zenu ni lini mutatambulika?
 
Waislamu, Wakiristu na Wahindu ktk sherehe zao wanawaalika viongozi wa serikali na ni dini zilizo andikishwa rasmi na mahala pao pa kuabudia panajulikana ama ni msikiti, kanisa au temple la wahindu!

Sasa kama nyinyi wachawi na waabudu mizimu kama ofisi zenu huwa kwenye giza au makaburini mutatambulika vipi? na lini muliwaalika viongozi wa Serikali ktk matambiko yenu wakakataa kuhunduriya? au lini mulipeleka maombi ya kusajiliwa mukakataliwa?

Waswahili husema usione vyaeleya vimeundwa! Wakiristo na Waislamu wanawafuasi wengi TZ kwasababu ya kujitangaza na kuonyesha uzuri wa dini zao ndio maana wanatambulika! CCM inawafuasi wengi TZ kwasababu ilijitangaza ktk kila pembe ya nchi lakini angalia vyama kama TADEA,NRA,UMD,DP, nk. vimebaki kudorora DAR bila ya kuhangaika kutafuta wanachama! sasa vitatambulikaje?

Ndugu zetu Wapagani au Wa Tanzania wenzetu mimi nawashauri kama munataka kuhudhuria ktk hafla za Kiserikali na mutambulike basi muji-organize kwanza, mujulikane muko wapi, ofisi zenu ziko wapi, wafuasi wenu ni wangapi na mujiandikishe rasmi Serikali kwa kuonyesha nani kiongozi wenu, halafu pia munaweza kupewa misaada toka Serikalini!
Jee, wanao abudu Jua, nyoka, mamba, Shetani, Simba, Mizimu nk. ni dini moja au ni tofauti? tukiwa tunalalamika tu bila ya kujitambulisha na kuwaalika wa Tanzania wenzenu ktk dini zenu ni lini mutatambulika?
 
Kila kukicha Watanzania wanaambiwa wasichanganye dini na siasa, lakini serikali yetu imejikita na udini kila kona

Nyimbo ya Taifa inamuomba MUNGU japo kuna watu wasiomwamini huyo Mungu

Viongozi wa kidini kila kukicha wako ikulu.

Waislam wakishindwa kwenda kuhiji, serikali inaingilia kuwapeleka kwa pesa za walipa kodi wasio Waislam wala wasio na dini.

Ukitembelea ofisi za serikali utashangaa zilivyopambwa na mapambo ya Krismasi bila kujali hisia za wasio na dini.

Iddi ikifika, serikali ya Zanzibar inaita wanajeshi na vikosi vinginevyo kufanya gwaride la iddi.

Sasa tukizungumzia udini serikalini tutakua tunafanya makosa?

Je, huyo Huseni Mwinyi mbona hasemi mambo haya ya magwaride ya iddi kama ni uvunjaji wa katiba? Maana alikua anang'ang'ania Zanzibar haiwezi kujiunga na OIC kisa Katiba haiwaruhusu. Je, katiba hiyo inaruhusu mambo ya wanajeshi kutumiwa kuentertain watu kwenye sherehe za kidini?

Pesa zilizotumiwa na logistics zingetumika kuwanunulia dawa za mbu ngapi hawa wanajeshi huko Zenji?
 
Hee?? hivi kumbe ni kweli kulikuwa na gwaride la EID??

Mi niliona picha kwa Michuzi ila nilidhani ni kuburudisha tu kibaraza kwani EID na ri GWARIDE wapi na wapi???
 
Game Theory acha uchokozi.

Halafu tofautisha dini na utamaduni au desturi. Mie ni mkristo, lakini siku ya Iddi huwa natinga kanzu yangu na kibaraghashia, nazama kwa washkaji zangu waislamu (ninao wengi tu) kwenda kukata pilau na sharbati. Nasi tukiwa na ubarikio nawaalika wanakuja wanaimbisha mapambio kama kawa. Na hapo sijasilimu wala wao hawajabatizwa, ni desturi zetu, ukarimu wa kiafrika.

Wahindi wakiwa wanafanya maandamano ya ile dini yao huwa wanapata ulinzi wa polisi na hata barabara zinafungwa, nimeyaona sana Dar, huu nao ni udini? Jibu langu ni HAPANA, serikali inawa-support wananchi wake kuyafanya yale wanayoamini yanawafaa alimuradi hawavunji sheria. Hii ni njia mojawapo ya serikali kuwa karibu na watu wake, si katika msiba tu, hata katika starehe kama sikukuu za Idd na Krismas na Diwali nk, serikali inakuwepo maana wote hao ambao sikukuu hizo zinawahusu ni wa serikali hiihii.

Na kama wasio na dini wana jambo lao wanahitaji support, waseme tu, kama halivunji sheria mtapewa kama ni bendi ya polisi mnataka au kusindikizwa, au chochote. Nashangaa anayewatetea wasio na dini ambao hawajawahi kujitokeza kama kundi kudai walichokikosa! Kama hao wanayo shida waseme.
 
Wasio na dini wasitake practice ya imani yao (ya kutokuwa na dini) iwe official. Ni kosa. Wasio na dini wanataka serikali itende kana kwamba wote hatuna dini. That is forcing their religious practice (of rejecting God) on all of us.

Serikali ya Tanzania si ya dini. Hilo ni sahihi zaidi kuliko kusema serikali haina dini. Hakuna serikali yenye dini lakini ziko serikali kadhaa duniani ambazo ni za dini moja au nyingine.

We need not ban God from the public square. Those that have banned God from their own lives may not force us to do the same in our public life.

Serikali ya Tanzania inashirikiana na madhehebu ya dini kwa karibu. That is as it should be. Inatambua ukweli kwamba kuelimisha, kutibu na kuendeleza Watanzania kwa ujumla ni kazi inayofanywa vizuri kwa ushirikiano kati ya serikali na dini za Watanzania.
 
kama Serikali haina dini kwa nini watu hawaendi makazini siku ya Eid na Christmass?. je si kuukumbatia udini huo na kuua uchumi kwa kutofanya kazi?.

Ukijibu swali hilo utagundua kwamba ni vigumu kutenganisha wananchi na taasisi zao. majeshi ni ya wananchi ndo maana hata majina yao yanareflect wananchi mfano,JESHI LA WANANCHI TANZANIA(JW), JESHI LA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO(POLISI).japo serikali haina dini lakini haiwezi kufanya mambo ya kujiweka mbali na wenye dini(walio wengi) ambao ndo wanaimiliki hata wa hiyo serikali yenyewe.tusiongopeane bwana wasio na dini Tz ni wachache mno,kwani hata wanaoabudu mizimu nao ndo dini yao hiyo.

ndo maana tukipata majanga mfano ukame,watu wa dini huomba mvua katika ibada maalum. sasa kama hilo serikali inalikubali na wala haitoi tahadhari kwamba haitambui ibada hizo, kuna ubaya gani kwa taasisi za umma mfano majeshi yetu kuwaburudisha watu wenye dini wakati wa sherehe za sikuu zao mafano Eid na Christmass? sizungumzii kipaimara au harusi ya raia hapa, nazungumzia sherehe zenye kuinvolve mass kubwa.

Halafu dhana ya serikali kutokuwa na dini msingi wake haswa ni katika kutekeleza majukumu ya kiutawala pasipo na dhulma, ama kuegemea katika kundi fulani na kulinyima haki kundi jingine, au kufungwa na taratibu za kundi moja na kuacha mawazo kutoka kundi jingine., dhana hiyo hailengi katika vitu kama Gwaride au kuwaarika watu ikulu, haya siyo msingi wa msingi wa dhana hiyo. unaweza kutowaalika mashehe na mapadri ikulu lakini ukatenda mambo ya Udini, unaweza usiandae gwaride la Eid lakini ukawa mdini kupita kiasi.isitoshe kama mashekhe na mapadri wanamwalika Raisi katika majumba yao ya Ibada kuna ubaya gani Raisi kuwaalika hao Mashekhe na mapadri Ikulu(makazi rasmi ya raisi).

Kwa kuwa wasio na dini ni wachache basi nadhani ni haki ya walio na dini ambao ni wengi kuendelea kulobby mfumo wa sera ili zikidhi maslahi yao.
 
Serikali yetu ni ya kisecular lakini kwa nini MUNGU antajwa kwenye nyimbo ya Taifa?

Serikali inaweza ikawa iko close kwa kuwajengea wanancho bara bara nzuri, kuwakwekea taa za barabarani

kuwapa Uslama


Kuacha kuwalinda wezi serikalini kama kule BOT

Kuwalisha wananchi wake vilivyo


lakini siyo kuwakodishia ndege waende kuhiji halafu wakirudi wanakufa kwa malaria kisa hospitali hazina dawa wala madaktari

siyo kuweka bajeti za kununu Christmas trees na Christmas parties kwa kodi za wasio na dini
 
GT,
Who said secularism does not embrace the presence of God? You don't have to be a religionist to believe in there being a God, do you?
 
Lakini watu wanaounda serikali wana dini kwa hiyo hawawezi na hawapaswi kwenda kufanya kazi siku za matukio muhimu ya kidini. Kimsingi kusema serikali haina dini ni uongo, labda tuseme serikali haiendeshwi kwa sheria na taratibu za dini, hapo nafikiri itakuwa sawa.
 
pamoja na maelezo mazuri yaliyo tolewa na wachangiaji hapo juu, bado haijaniingia kabisaaa. gwaride na EID wapi na wapi???????,, ebu fikiria, tukianza kuwa na gwaride la eid, la x-mass, easter, la Kambi, la hindu, Budha, la akina Oldonyolengai, mulungu n.k????

Kama ni ulinzi sawa, lakini salute sasa na mwendo wa pole, na kunyakua??? may be am too naive!!!!
 
GT,
Who said secularism does not embrace the presence of God? You don't have to be a religionist to believe in there being a God, do you?

False. Religion is a personal matter, and one does not have to judge on the status of religion in human society.

I am more worried about raising a child in a society where they will be forced to believe in God because he is sang in national anthem and being sieged every now and then with religious fanatics are at the core of our Government

If religionists like our humble Government believe the opposite or that a God exists, they have never been able to prove it. And so they resort to "faith" that what they believe is so because they believe it's so.

Moreover, they challenged scientific atheists and chide them to prove there isn't a God. And that is a form of intolerance which is logically stupid, too. Since the burden of proof is on those who make the positive claim there is a God, and and not on those who don't, since they or no one for that matter are required to prove a negative.

History shows that Democracy requires a separation of state and church, because no democracy is possible in a theocracy where state and church are one. And if secularists thrive in a democracy, so why should they be abashed or even concerned if the religionists can't thrive in a democracy?

Atheists know how to mind their own business, and they have the lowest rate of incarceration in the world, while religionists have the highest rate of incarceration in the world. And that is historical fact.

Let people believe whatever they want, but keep the state secular. Secularism is crucial to the liberty and efficiency of the state apparatus.
 
kuna tofauti kati ya serikali(government) na taifa(nation). si kila kitu ni mali ya serikali, infact serikali yenyewe ni portion tu katika nation, au kwa lugha ya kihesabu tunasema serikali ni SUBSET ya Taifa(nation). kuna mambo kama wimbo wa Taifa, nao ni mali ya taifa(nation) na wala siyo mali ya serikali-ni kutokutumia misamiati yetu vyema tu ndo tumefikia mahali tukadhani kwamba kila kitu official basi ni cha serikali, mathalani siku kuu za waislamu na wakristo(katika uwingi wao) siyo za serikali lakini ni za Kitaifa(kwa maana ni za wenye taifa).
 
Naona wengi mnatumia msamiati ambao siafiki. Mnasema serikali haina dini. Serikali ni KITU, na ni WATU tu ndio wenye uwezo wa kuwa na dini. Serikali inaweza ikawa ya dini, lakini kusema serikali haina au ina dini ni msamiati wenye makosa.

Serikali ya Saudi Arabia ni ya dini. Hatuwezi kusema ina dini. Haina utashi. Serikali ya Tanzania si ya dini yoyote. Hivyo ndivyo tunavyopenda. Lakini inatambua na kushirikiana na dini za Watanzania.

Kuna aliyesema hataki wanae walazimike kusikia kuhusu Mungu. Ili kutatua hilo, anataka wanetu walazimishwe kutosikia kuhusu Mungu! Kumuondoa Mungu kwenye Wimbo wa Taifa ni kulazimisha imani ya wale wasiomtaka Mungu iwe ndiyo imani inayotambulika na kitaifa!
 
lakini jamani hapo la muhimu zaidi na la kuongelewa ni kuwa na li gwaride la eid!if it is hivyo then for me nadhani yatokana na majeshi yetu kujaa pasipo kuwa na kazi za ku do!mwee lakini yanafanywa kwa gharama za kina nani?
Eid Mubarak people
 
Nilipokuwa pale kwenye Blogu ya Michuzi, niliona kuwa huko Zanazibar sherehe za Idi zilisherekewa kwa kusindikizwa na gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama. Angalia Hapa

Ingawa kwetu sisi sikukuu za kidini zinatambulika kuwa ni za kitaifa, sijawahi kuona zikisherehekewa kwa kutumia vyombo vya dola kama vile kupigiwa wimbo wa Taifa au gwaride la kijeshi kama ilivyofanyika. Inawezekana nimekosea lakini nadhani kuwa si halali kusherehea sikukuu za kidini kwa kutumia vyombo vya dola. Je wadau mnaojua sheria ya katiba mnasemaje?
 
Kama Ni Kweli Huoo Ni Uchuro Wanatuletea ..kaswida Zingetosha ..yanini Kutumia Majeshi Wakati Serikali Haina Dini????
 
Status
Not open for further replies.
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom