Ahsante Mkuu, nadhani hapa sina cha kuongeza.Wasio na dini wasitake practice ya imani yao (ya kutokuwa na dini) iwe official. Ni kosa......
We need not ban God from the public square. Those that have banned God from their own lives may not force us to do the same in our public life.....
Naona wengi mnatumia msamiati ambao siafiki. Mnasema serikali haina dini. Serikali ni KITU, na ni WATU tu ndio wenye uwezo wa kuwa na dini. Serikali inaweza ikawa ya dini, lakini kusema serikali haina au ina dini ni msamiati wenye makosa.
Serikali ya Saudi Arabia ni ya dini. Hatuwezi kusema ina dini. Haina utashi. Serikali ya Tanzania si ya dini yoyote. Hivyo ndivyo tunavyopenda. Lakini inatambua na kushirikiana na dini za Watanzania.
Kuna aliyesema hataki wanae walazimike kusikia kuhusu Mungu. Ili kutatua hilo, anataka wanetu walazimishwe kutosikia kuhusu Mungu! Kumuondoa Mungu kwenye Wimbo wa Taifa ni kulazimisha imani ya wale wasiomtaka Mungu iwe ndiyo imani inayotambulika na kitaifa!
JAMANI IKO HIVI: SERIKALI YETU HAINA DINI, ILA INAAMINI UWEPO WA MUNGU, NDIYO MAANA MUNGU ANATAJWA HATA KATIKA WIMBO WETU WA TAIFA.
"KUTOKUWA NA DINI" DOES IMPLY "KUTOKUWEPO MUNGU", ISIPOKUWA THE VICE-VERSA IS TRUE. MIMI NINAVOELEWA HATA WAPAGAN WANAAMIN KUWA KUNA MUNGU, SEMA TU SASA ISSUE INAKUWA KATIKA MODE OF WORSHIP WANAYOTUMIA INAKUWA TOFAUTI KIDOGO NA YA WAKRISTO, AU DINI ZINGINE. NI SAWA TU KAMA AMBAVYO WAHINDU NA WAKRISTO AU WAISLAMU WANAVYOWEZA KUTOFAUTIANA KATIKA NAMNA YAO YA KUABUDU. NI ATHEISTS TU NDIYO WANAOAMINI KAMA HAKUNA MUNGU. LAKINI SASA, TUMNACHAGUA VIONFGOZI KWA KUTUMIA DEMOCRACY, KWAMBA THE MAJORITY BECOMES THE WINNERS.BILA KUJALI DINI, NI DHAHIRI KUWA ZAIDI YA 50% YA WATANZANIA WANAAMINI UWEPO WA MUNGU.
JE KUNA SABABU GANI SASA YA MSINGI KUIZUIA SERILKALI YETU PIA KUAMINI HILO? KUNA SABABU ZIPI ZA MSINGI ZA KIFANYA SERIKALI YETU ISITOE SUPPORT ZA SHEREHE ZA KIDINI IWAPO INAAMINI UWEPO WA MUNGU? ATHEISTS NI WANGAPI WATUAMBIE SASA WANATAKA NINI NA SERIKALI WANAHITAJI IWAFANYIE NINI, NA SI KUANZA KUTAKA KUVURUGA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YA SERIKALI NA MUNGU PAMOJA NA DINI ZINGINE.
TATIZO NINALOLIONA NI KWAMBA WAKATI MWINGINE TUNAKUWA MA-RADICAL MUNO KIASI KWAMBA HATA PALE AMBAPO SRIKALI HAINA DOA, TUANJITOSA KWA NGUVU ZOTE KUKIKOSOA. NADHANI TUNAKUWA MUNO "ZAIDI YA WAPINZANI"
KILA LA KHERI
Wengi hatujui tofauti kati ya mungu na DINI. matokeo yake kuna watu wanaamini wanaweza kuishi bila mungu au DINI...
Hili ni somo pana sana na hapa JF square hapatoshi labda tupeana assignemnt kila mmoja azifanye kujifunza zaid.
DINI-ni mfumo wowote wa maisha ambao mwanadam kaamua kuufuata. Hivyo kila mtu ana DINI. inawezekana tu dini hio haina jina rasmi as Ukristo au Uislam...kwa utaratibu huo u-socialism nao ni dini..na mifumo mingine ya ulimwengu
[wengi wameelewa vibaya maana ya dini kwa kuinasibisha na IMANI, na ndo maana wengi wamekuwa wakisema dini ni IMAN..oh upendo n so on]...
Mungu- Maana ya Mungu ni kitu chochote unachokitumikia. Ikiwa MATAMANIO ya NAFSI Yako unayatumikia basi hayo yatakuwa Mungu wako. Wengi wameinasibisha maana ya mungu na supernatural powers. Ikiwa mtu bosi wake anamtumikia basi yeye huyo ndie mungu wake...
Ni kweli kuwa mambo mengi kenya yanafanyika kwa kuangalia majina na sehemu ya kuzaliwa kama ilivyo kawaida ya nchi nyingi za Afrika. Hili la uchaguzi unaokwisha ambao umeleta mzee kikongwe mwingine madarakani (miaka 76) na kinachoendelea sasa hivi ni lazima kifundishe mataifa mengine.
Kama vile kenya kulivyo na ukabila, siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania. Nilisikitika sana kuambiwa kuwa hata mashuleni siku hizi chaguzi za viongozi wa wanafunzi pia ni kwa misingi ya kidini!
Badala ya kukaa tunatoa macho kuwapondea wakenya kwa kile ambacho kimefanyika, ni vyema sasa Tanzania pia tukaacha haya ya udini ambayo sasa hata yanagawanya waislam (shia dhidi ya sunni) na wakristo ( walokole dhidi ya wasiookoka).
Tusipoacha hili, tusubiri tena vizazi vingine vitatu ili kupata maendeleo yale tunayopigania kwa mama yetu afrika.