KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Bunge linajadili ktu chochote ambacho either ni mahitaji ya jamii au ni problem ..sioni ubaya wowote kujadili dini, hayo yote ni sehemu ya maendeleo na mahitaji ya jamii..ulitaka wasijadili huo mjadala ufanyike wapi??? wakati hicho kinachojadiliwa ni mojawapo la tatizo katika jamii?
Sasa ikiwa bungeni ndo mahala muafaka pa kujadili dini, basi tusishangae wengine wakipinga hoja za kidini zinazotolewa, iwe ni za kiislam au za kikristo. Mijadala bungeni huenda kwa kukubaliana na kutokubaliana. Sasa ikitokea mtu kutokubaliana ujue ni sehemu ya mjadala. Vile vile uwe tayari kuona na kuvumilia hoja za upande wa pili kwani dini ikishakuwa mjadala bungeni usitegemee wabunge wote wakubliane na dini moja; kwani wabunge wote si wa dini hiyo.