Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

Status
Not open for further replies.
M

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,605
2,000
hivi mkristo wa kibondo(na kwingineko) asiye na barabara na miundo mbinu mingine anafaidikaje na idadi kubwa ya viongozi wakristo serikalini?
 
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Hii sasa ni Jamhuri ya Kikristo ya TanzaniaKWA HALI ILIVYO sasa na mambo ambayo yamekuwa yakitokea kimyakimya kati ya serikali na kanisa hapa nchini ni dhahiri kuwa Tanzania hivi sasa haisthili kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali Jamhuri ya Kikiristo ya Tanzania.

Maana kigezo cha kutanabahisha kama mtu fulini ni hili au lile ni sauti na uwezo wake juu ya suala muhimu husika.

Katiba inadhihirisha kwamba kila mtu ana haki ya kuwa muumini wa dini anayoitaka na kuabudu kwa namna anayoitaka. Sasa Muislamu anapotaka kukamilisha ibada yake kwa kuwa na Mahakama ya Kadhi utailewaje serikali hiyo inapotafuta ushauri wa wasio Waislamu kama Waislamu waruhusiwe hilo au la.

Kwa kuwa aliyeachiwa uamuzi si serikali bali madhehebu za Kikiristo ndio maana tunasema kwamba SERIKALI TANZANIA INA DINI na sio vinginevyo na dini hiyo sio nyingine ila UKiristo!

Tunasema hivi kwa sababu zifuatazo:
1. Serikali haiwezi kutekeleza madai au haki yoyote ya Waislamu bila kushauriwa na kuruhusiwa na Kanisa au Wakiristo kwa ujumla wao.
2. Serikali imekuwa ikigawa kulia na kushoto mali zilizotaifishwa kwa makanisa na viongozi wao.
3. Kanisa limekuwa likiiandikia cheki isiyo na kiasi cha fedha chama tawala kila inapofikia uchaguzi.
4. Serikali imekuwa ikiliandikia kanisa cheki isiyo na kiasi cha fedha kanisa kila inaporudi madarakani.
5. Washauri wanaomzunguka kiongozi wa nchi karibu wote ni Wakiristo.
6. Idadi kubwa ya mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya na viongozi wengine wa juu ni wakiristo, mathalani, kati ya mawaziri wakubwa ni 15 tu ndio waislamu na takriban 35 ni wakiristo.
7. BAKWATA kiutendaji iko chini ya Waziri Mkiritsto. Na rushwa serikali inayotoa kwa BAKWATA ndiyo inayosababisha migogoro isiyoisha huko.
8. Kanisa linaendelea kumiminiwa fedha sio tu na serikali bali wafadhili wa ndani na nje wakati misaada yote ya Waislamu imepigwa 'X' kwa kisingizio cha Ugaidi au inaliwa na wakubwa wa serikali kama ilivvyofanywa kwa EPA.
9. Serikali imeruhusu kujengwa mabaa, masoko machafu na makanisa ya walokole karibu kila panapokuwepo na msikiti hivi leo.
10. Serikali inawakataza wafanyabiashara wa Kiislamu kuchangia upanuzi wa redio za Kiislamu na kuanzishwa kwa televisheni za Kiislamu wakati wakiristo tayari wana televisheni 7 na redio zipatazo 30.
11. Wakati shule za Wakiristo zinapata ruzuku toka serikalini shule za Kiislamu hazina bahati hiyo.
12. Mamia kama sio maelfu ya watoto wanaopelekwa kwenda kusoma nje hivi leo ni watoto wa viongozi wakiristo.
13. Fedha za kupiga vita umasikini nyingi zimeliwa au kuepewa wale wasio waislamu wakati waislamu ndio masikini wakubwa nchini.
14. Serikai inapiga vita kuwepo kwa kiongozi bora, safi na mwadilifu wa Kiislamu kwa kuunga mkono viongozi wasio na elimu dunia na wababaishaji hata katika hiyo ya dini.
15. Serikali imeamriwa na Wakristo kutoruhusu Mahakama ya Kadhi. Lakini wakati huohuo imelazimishishwa kuwapa kwa ubalozi wa Vatican hapa nchini kwa kisingio kwamba eti Vatican ni nchi wakati ni ufalme wa Kikatoliki ndani ya Italia.
16. Serikali imepiga marufuku Waislamu kupata misaada toka nchi za nje. Na misaada hiyo inapoingia inataifishwa na Benki kuu na kuliwa kama fedha za EPA!
17. Serikali na vyama vya siasa vinawatisha Waislamu viongozi kutotetea au kuundeleza Uislamu. Na imeshindwa kabisa kuwasaidia viongozi hao wasio na maarifa ya Uislamu elimu muhimu ya dini yao wakati wakiwa kazini.
18. Serikali inatumia vyombo vya habari (vyake au vya wamiliki binafsi) ama kuendeleza ukiristo au kupiga vita Uislamu na kuchafua maadili ya kumuhofu Muumba na ucha Mungu.
19. Serikali inatumia vyombo vya dola na mahakama kuwaadhibu na kuwaonea viongozi wa Kiislamu.
20. Bunge linadharau Uislamu na ibada zao. Kiasi cha kwamba siku ya Ijumaa ni shughuli kama kawaida na waumini wa Kiislamu ndani ya Bunge ama ni waoga au wanatishwa katika kulikataa hili.
mkutano wa mwisho kati ya Kanisa na serikali ulifanyika lini na wapi?

Nipe namba ya cheki angalau moja ambayo kanisa limeiandikia serikali kabla ya uchaguzi. Pia nipe namba ya cheki ya malipo kutoka serikali kwenda kanisani

Washauri ni wakristo lakini viongozi wa juu ni Waislamu hapo je?

Hivi misaada ya jumuia ya kiislamu ni lazima ipitie serikalini?
Misaada ya kanisani inapitia serikalini?

Mahakama ya kadhi ni nguzo ya ngapi ya muislamu?

Seminari ipi inapata ruzuku toka serikalini?

Kuna kiongozi mkristo huko BAKWATA? Toba?

Mahakama ya kadhi anzisheni mkishindwa kuwalipa makadhi ombeni msaada.

Vatican ni nchi, ina kila sifa ya kuwa nchi.

Eti kwa sababu Swaziland yote ipo ndani ya nchi ya South Afrika itahesabiwa siyo nchi? Mrejee mwalimu wako wa siasa Jiografia na Historia.
Kuna Uhusiano gani kati ya Vatican na Mahakma ya kadhi. Mlinganyo huu wa Vatican na Mahakama ya kadhi unaongelewa kila siku na kila muislamu mwenye kudai mahakama ya kadhi. Ina maana ubalozi wa Vatican ndo kikwazo cha Mahakma ya kadhi? Ubalozi wa Vatican unalipiwa na Serikali ya TZ? Au namna gani? Naomba nielimishwe

Misaada ya Waislamu inatafuta nini BOT? Ninyi Waislamu ndiyo mnawaagiza wahisani wenu kupitishia misaada yenu serikalini?

Kwa nini mnaweka misaada mbele ya mambo yote?

Ni agizo la Tarehe ngapi kwenye gazeti la toleo gani la seriklai misaada kwa waislamu imepigwa marufuku?

Umasikini haupigwi Vita kwa fedha ila kwa kujenga mtizamo mpya katika jamii.
Hakuna kiasi cha fedha toka nje ya Tanzania wala ndani kitakacho maliza umasikini.
Kama unaongelea kufix Kuchacha hapo upo sahihi. Kuchacha na umasikini ni vitu viwili tofauti kabisa.

Kuna serikali za Kikristo Duniani German, Sweden,Finland, UK nk Tanzania si moja wapo.
Kuna serikali za Kiislamu Duniani kama Saudi Arabia na Iran Tanzania si mojawapo.
Kuna serikali zisizo na Dini Mexico,USA ,Brazil,China,Japan, Korea, Singapore Tanzania ni mojawapo.
 
Sokomoko

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Quran imeshindwa kuwaongozeni nakuwatatulia baadhi ya migogoro mpaka sasa mnaiacha njia ambayo mmeambiwa muifuate mnaanza kujitafutia njia zenu wenyewe za mahakama sio tena quran.

Nadhani kuna mapungufu ndio maana mnadai mahakama je mashekhe wenu wameshindwa kuwaongoza? au na shekh anayo mapungufu?Wewe umetumwa,hivi unadhani kwakuongea hivyo utamtisha nani kwakufanya hivyo hivi unadhani nyinyi ni watoto kana kwamba kila mnachotaka mnaanza kulia kama watoto ili msikilizwe.

Nyinyi kwanza wabinafsi sijui mmekosa nini kama maakama sizipo sasa isue gani imeshindwa kufanywa na mahakama zetu kwanza hiyo ni kudharau Dora (mahakama).

N:B haya matatizo gani ambayo yametokea hapa tz yakashindwa kuamuliwa na mahakama ya kawaida nyinyi ni wabaguzi ndio maana mnataka mahakama yenu wenyewe,Mkipewa mwishowe mtaomba mgawiwe nchi yenu wenyewe maana hamja acha fikra za kibaguzi za Warabu.
Samahani sana mkuu napendakukupa ushauri kuwa kama kitu hukijui ni bora unyamaze kuliko kusema usilolijua.

Ni kweli Quraan ndio inayotuongoza kwenye kutatua migogoro na maswala yahusuyo maisha yetu ya kila siku. Na hiyo mahakama amboyo hata United Kingdom ipo sijui wewe inakuuma nini hapa TZ kurudishwa hiyo mahakama?maana sio kweli kuwa unaanzishwa ila inarudishwa maana ilikuwepo tangu enzi za mjerumani kwahiyo hakuna jipya hapo wenye akili wataelewa na kunyamaza ila wenye vijiba na roho mbaya watatia maneno yao.

Serikali ina dini?

Ukitaka kujua ina dini au haina dini angalia hapa chini.

1. Ikiingia December tembelea ofisi za mashirika ya umma,wizara na taasisi za umaana. Ujionee mapambo yamamilioni ya pesa kwa ajili ya Christmass. Hapo ndio utajua kuwa hii serikali ya TZ ina dini? na dini gani?

2. Kwa uhakika kamali chokoza kuongelea Mahakama ya kadhi kurejeshwa nchini utaona hao wenye serikali yaowatakavyokuja juu.

3. Kama number 2 haijakuridhisha refer to number 1.
 
J

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,333
1,225
Moderater hapa sio sehemu yake kwa kuwa hii haikuwa habari lakini hata napenda kuwapa ushauri kidogo mnaopingana kuhusu dini.

  1. je mnajua kuwa wakati nyinyi mnapingana wanasayansi wako karibu kugundu kuwa dini ni kitu kilichotungwa na mwanadamu.
  2. Dini zote zimeiba idea zilitangulia kila dini kwa wakati wake, tafuta ukweli kuhusu dini ya Wamisri wa kwanza, pamoja na watu wa kale walioishi mexico utapata ukweli kuhusu dini mnazobishiana kila wakati.
  3. hivyo vitabu vyenu kila kimoja kina makosa makubwa ambayo kama wewe ni critical thinker unaweza ukaacha kwenda msikitini au kanisani.
  4. kwanini msimalize hizi tofautndogo badala ya kubisha kwa vitu vidogo kama hivyo.
  5. wanasayansi wanaprove sasa matukio ambayo dini zinatumia na kutoa sababu ya matukio hayo wala hayakuwa na miujiza yeyote ni vitu vya kawaida kama vinavyotokea leo hii vikiwa na maelezo ya kutosha.

Samahani kama nimewaudhi lakini ni vizuri dini zote zikishikamana hasa wakti huu na kumtafuta mwenyezi mungu kwani baada ya muda mfupi ujao anaweza kufutika katika akiri za wati kwani sayansi inazidi kujidhihilisha kuwa pale ambapo akiri ya mwanadamu inaishia tunasema kuna mungu lakini si kweli.

Mfano zamani tuliamini huko juu kuna mbingu lakini sayansi imeshadhibisha kuwa is just space nothing there, unless ni invisible kama kawaida ya vitu vya dini ukikosa explainations unasema mungu anauwezo ndio maana kaficha.

reference za story za kwenye vitabu vya dini sasa hivi sayansi inaweza kuzielezea kisayansi bila tatizo lolote na ukaona kuwa hakukuwa na maajabu yeyote.

Please badala ya kubishana tuungane tumtafute mwenyezi mungu kwani dunia inaangamia.
 
X-PASTER

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,640
1,250
Acha hoja zisizo na msingi, unataka ratio sawa kwa waislam na wakristo. Kama unajua hesabu fanya hivi, chukua idadi ya waislam waliopo katika serikali then wape vyeo kwa mlingano sahihi uone kama watawazidi wakristo. kubali usikubali wasomi waislamu ni wachache kulinganisha na Wakristo.
Pole ikiuma toa. Hamia ukristo unakaribishwa
Haishangazi...! Ndo maana nchi imefikishwa hapa ilipo...! Ongereni na usomi wenu ulio jaa ufisadi.
 
bokassa

bokassa

JF-Expert Member
May 19, 2007
403
0
Kwani Tanzania bado kuna waislam na wakristo serikalini!!!!!!

Kama viongozi walio serikalini wanaoitwa majina yafananayo na John au Ally ni wakiristo au waislamu basi hizo dini hazifai!!!!
 
Absolute

Absolute

JF-Expert Member
Jan 19, 2007
333
0
Moderater hapa sio sehemu yake kwa kuwa hii haikuwa habari lakini hata napenda kuwapa ushauri kidogo mnaopingana kuhusu dini.

  1. je mnajua kuwa wakati nyinyi mnapingana wanasayansi wako karibu kugundu kuwa dini ni kitu kilichotungwa na mwanadamu.
  2. Dini zote zimeiba idea zilitangulia kila dini kwa wakati wake, tafuta ukweli kuhusu dini ya Wamisri wa kwanza, pamoja na watu wa kale walioishi mexico utapata ukweli kuhusu dini mnazobishiana kila wakati.
  3. hivyo vitabu vyenu kila kimoja kina makosa makubwa ambayo kama wewe ni critical thinker unaweza ukaacha kwenda msikitini au kanisani.
  4. kwanini msimalize hizi tofautndogo badala ya kubisha kwa vitu vidogo kama hivyo.
  5. wanasayansi wanaprove sasa matukio ambayo dini zinatumia na kutoa sababu ya matukio hayo wala hayakuwa na miujiza yeyote ni vitu vya kawaida kama vinavyotokea leo hii vikiwa na maelezo ya kutosha.
Mh...Kazi ipo.
Afterall mie sifaidiki na vibosile waislam/wakristo advantage kubwa iko kwa ma2mbo yao na families and friends.

Kwani kuwa waislamu/wakristo ndo watafata maandiko ili kutetea dini zao labda ile michango ya kanisani/msikitini b'se kama mtakumbuka waziri flani mstaafu mwenye surname ya lion ni mgida alcohol sana though dini yake hairuhusu.Wengi wao ni waislamu/wakristo jina tuu

Kwahiyo mie sioni hata importance ya sisi kupotezeana seconds discussing this matter.

Mda umefika wa sisi kujikita zaidi ktk matters za nchi ye2 other than religious...tukianza tena ku-search Absolute ni dini gani na Invisible ni dini gani ha2fiki mbali
 
Malaria Sugu

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
0
Nimefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge kipindi hichi, nilisoma mwanahalisi la 8/7/2009 linalozunmgumzia Udini Bungeni. Naungana na mwanahalisi kwa habari ile. kwani udini unaonekana wazi wazi bungeni hasa akionekana mbunge muslim kama vile Msambya alakitetea Jambo ndani ya bunge kwa maslah ya Taifa kuhusu Islam huchekwa na wabunge wengine au kama alivyosema mwanahalsi kwamba wabunge mawaziri waislam waandamawa bungeni. na spika hazungumzi kitu. jee ni haki kwa spika kuchekelea
 
Kipunguni

Kipunguni

Senior Member
Jun 20, 2008
151
0
Mkuu, hebu elezea vizuri basi .... toa mifano, if possible!
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
..nadhani wa-Tanzania tunahitaji "TIME-OUT" ya kuzungumzia masuala ya Dini.
 
K

KipimaPembe

JF-Expert Member
Aug 5, 2007
1,285
1,225
Udini bungeni unaletwa na sera za kidini. Bungeni ikiwa ni mahali sahihi pa kutetea uislam, utarajie bungeni vile vile pawe mahali pa uislam kupata upinzani!!

Ikiwa Msambya anatumia jukwaa la Bunge kutetea uislam, kwa nini ushangae sera ya uislam kupingwa? Bungeni ni mahala pa siasa na kupingwa ni sehemu ya siasa ati!

Kwa hiyo ikiwa hoja za ndugu msambya ya kutetea uislam ndani ya bunge ina lengo la kutetea maslahi ya waislam, ukumbuke kuwa maslahi ya waislam hayahusishi maslahi ya wasio waislam. Sasa ikiwa waislam wanaanza kuwa kundi linalokuwa na maslahi ambayo ni tofauti na maslahi ya makundi mengine ya kidini ujue hayo makundi mengine nayo yana haki ya kutumia Bunge vile vile kudai maslahi yake na kujitetea.

Sera ya kuanza kuwagawa wananchi katika makundi ya waislam na wasio waislam ndo zinafanya dini kuingia Bungeni. Mbunge anayesimama kwa ajili ya kutetea waislam peke yake hatetei maslahi ya kitaifa bali maslahi ya waislam. Nitashangaa sana kama hili la kutetea maslahi ya waislam Bungeni hutaliona kama udini, ila udini uone kama ni wale wanaopinga suala hilo.

Lakini vile vile ukisoma kilichoandikwa katika mwanahalisi, nadhani hapa sasa lengo la CCM kuingiza udini linaanza kufanikiwa. Kwamba hata waziri akiwa challenged, kitu cha kwanza anaangalia dini ya mtu anaye mchallenge badala ya kuangalia hoja. Nadhani hii ni lowest point ambapo nchi hii inaweza kufika. Yaani waziri akibanwa kwa hoja ambazo ziko wazi anasema ni kwa sababu yeye ni mwislam au mkristo? Ooooh Tanzania, where are we going? Nadhani tunao mawaziri wenye uwezo mdogo kabisa kuliko wakati wowote katika nchi hii. Yaani waziri anashindwa kupangua hoja za wabunge anadai kuwa anabanwa kwa sababu ya din!!!!
 
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Nimefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge kipindi hichi, nilisoma mwanahalisi la 8/7/2009 linalozunmgumzia Udini Bungeni. Naungana na mwanahalisi kwa habari ile. kwani udini unaonekana wazi wazi bungeni hasa akionekana mbunge muslim kama vile Msambya alakitetea Jambo ndani ya bunge kwa maslah ya Taifa kuhusu Islam huchekwa na wabunge wengine au kama alivyosema mwanahalsi kwamba wabunge mawaziri waislam waandamawa bungeni. na spika hazungumzi kitu. jee ni haki kwa spika kuchekelea
Weeeee, taratibu ndugu yangu.
Kwahiyo we unataka spika awatetee mawaziri waislamu sio?Kama waziri ameshindwa kujibu hoja spika amsaidie ili iweje? Hata hivyo kwa upande mwingine, kwani ni mara ngapi tumemshuhudia spika akiwaokoa mawaziri wasisulubiwe kutokana na kujibu hovyo hovyo?
Halafu hii tabia ya waislamu kulia lia kila siku, kila mara, kila kitu wao ni kulialia tuuuuu kwamba wanaonewa inatokana na nini?
Rais wa nchi mwislamu, makamu wake muislamu.
Mwenyekiti wa chama tawala muislamu, katibu mkuu wake muislamu, sasa mnalalamika nini? Au mna agenda ya siri?hapana bana this is too much.kila kitu kulalamika tuuuu.
 
kinepi_nepi

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
0
Dini na JF haifai kabisa, na dini na bunge sioni mwisho mzuri. wajadili katiba na maswala ya nchi.

Dini ni mambo ya imani ni vigumu sana kujadili mambo ya imani kwa watu wenye imani tofauti, utofauti huu ndio umeleta dini tofauti, dhehebu tofauti na namna tofauti za kuabudu. na tulikubaliana kwenye katiba yetu kuwa kila mmoja ana uhuru wa kufanya ibada na kuamni anavyotaka bila kuvunja katiba na sheria za nchi. nafikiri tungeachia hapo na kuendeleza libeneke letu na kuacha kila mmoja akimtafuta mungu wake kwa staili yake ilimradi havunji sheria ya nchi.

Anayetaka kuabudu kwenye miti ruksa, kwenye mapango ruksa, nje ruksa juu ya mti ruksa, usiku ruksa, mchana ruksa. Tuaache dini zifurahie katiba inayojali wananchi wake na usawa kwa wote.

Utawala wa haki na sheria ndio utatokomeza haya yote.
 
Barubaru

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
0
Mimi naona Tanzania kuna udini tokea enzi. Utaona issue yoyote ile inapogusa maslahi ya waislam basi utaona wengi wanasema udini.

Mimi nakumbuka nilipokuwa Tanzania kulikuwa na kesi moja ya kijana mmoja wa kiislamu kule morogoro alihukumiwa kwenda jela kwa kosa la kusema YESU SI MUNGU. Na waislamu waliposimama kutetea basi ilikuwa tafrani sana.

Nakumbuka pia wakti waziri KAPUYA alipokuwa waziri wa elimu. Pale bungeni alilazimishwa kufuta usemi wake pale aliposema waislamu watoto wa kike waruhusiwe kuvaa hijabu kama sehemu ya sare zao za shule.

Sasa siku zote waislam wa TZ wamekuwa kama second citizen na wakristu especially RC kuwa ndio vinara wa kulisemea kanisa.

Kumbuka juzi tu wakti waziri wa Fedha wa TZ Mustafa Mkulo alipofuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini na NGO. Wa kwanza kulalama alikuwa Pengo na akafuatiwa na Kilaini.

Rejea nyuma kidogo Waziri wa mambo ya Nje wa Tz Bw Membe alikaripiwa vikali sana na Pengo na Maaskofu wangine aliposema Tz ipo katika mchakato wa kujiunga na OIC.


Sasa mimi naona haya yote ni mafundisho kuwa waislamu hawana uhuru ndani ya nchi yao. sasa wanapopata sauti na kukemea hapo unaitwa UDINI.
 
Dilunga

Dilunga

JF-Expert Member
Apr 8, 2009
679
0

Nimefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge kipindi hichi, nilisoma mwanahalisi l ... Naungana na mwanahalisi
Unasema umefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge, haya, nilieleze ni nini kilisemwa na mbunge gani, na waziri gani alilalamika, na alisema nini kuhusu uislam.

Hii inawezekana ni figment yako wewe na Said Kubenea tu, huenda hapa tunakuwa concerned na mambo ambayo sio pressing issue kwenye jamii ya Watanzania. Tuko out of touch, si ajabu.

Said Kubenea kaandika makala, mawazo yake yeye, halafu tunataka kuigeuza national debate. Haya, debate yenyewe hatujui hata yaliyosemwa ni nini, I mean, nani anajua Waziri alisema nini, na Mbunge alisema nini?
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,539
2,000
Unasema umefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge, haya, nilieleze ni nini kilisemwa na mbunge gani, na waziri gani alilalamika, na alisema nini kuhusu uislam.

Hii inawezekana ni mada yako wewe na Said Kubenea tu, huenda hapa tunakuwa concerned na mambo ambayo sio pressing issue kwenye jamii ya Watanzania. Tuko out of touch, si ajabu.

Said Kubenea kaandika makala, mawazo yake yeye, halafu tunataka kuigeuza national debate. Haya, debate yenyewe hatujui hata yaliyosemwa ni nini, I mean, nani anajua Waziri alisema nini, na Mbunge alisema nini?
Yeye kaandika hicho alichosikia na kusoma kwenye hilo gazeti. Sasa ni au wewe uridhike na aliyosema na ukae kimya/umuunge mkono, au tafuta hayo maelezo na uyalete hapa kuthibitisha kuwa jamaa maneno yake yamepishana na ukweli.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,158
0
Bunge linajadili ktu chochote ambacho either ni mahitaji ya jamii au ni problem ..sioni ubaya wowote kujadili dini, hayo yote ni sehemu ya maendeleo na mahitaji ya jamii..ulitaka wasijadili huo mjadala ufanyike wapi??? wakati hicho kinachojadiliwa ni mojawapo la tatizo katika jamii?
 
H

Heradius

New Member
Sep 27, 2007
1
0
hellow wanajamii,
chanzo cha udini ni mwenyekiti wetu wa nchi yetu make uteuzi wake kwa viranja wa nyadhifa za juu kuwa asilimia kubwa dini moja.
Civilians tunaona na kwa kuwa baadhi ya wenzetu hawawez kujizuia kusema ndo maana linatokea.Tusilaumu wabunge make nao ni wawakilishi.
Cheers
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,539
2,000
Nimefuatilia kwa karibu mjadala wa Bunge kipindi hichi, nilisoma mwanahalisi la 8/7/2009 linalozunmgumzia Udini Bungeni. Naungana na mwanahalisi kwa habari ile. kwani udini unaonekana wazi wazi bungeni hasa akionekana mbunge muslim kama vile Msambya alakitetea Jambo ndani ya bunge kwa maslah ya Taifa kuhusu Islam huchekwa na wabunge wengine au kama alivyosema mwanahalsi kwamba wabunge mawaziri waislam waandamawa bungeni. na spika hazungumzi kitu. jee ni haki kwa spika kuchekelea

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama tawala, amiri jeshi wa JWTZ ni MUISLAAM.
Makamba ni Muislaam.
Karume ni Muislaam.
Shein ni Muislaam.
Maalim Seif, Lipumba, Zitto ni Waislaam.
CCM imejaa Waislaam.
Rostam Azziz ni Muislaam........

Nchi mmeishika Waislaam. Madaraka ya Rais ni makubwa sana hadi mwenyewe alisema kuwa wanaangalia wayapunguze. Bado unaona mtu analialia hapa kuwa wananyanyaswa. Utafikiri Mzinga wa baba na msuli mzito linalalamika "sisi mashoga twaonewa..."
 
Dilunga

Dilunga

JF-Expert Member
Apr 8, 2009
679
0
Yeye kaandika hicho alichosikia na kusoma kwenye hilo gazeti. Sasa ni au wewe uridhike na aliyosema na ukae kimya/umuunge mkono, au tafuta hayo maelezo na uyalete hapa kuthibitisha kuwa jamaa maneno yake yamepishana na ukweli.
Sikonge, elewa kitu kimoja brother kaka. Makala ya Mwanahalisi ni mawazo ya Kubenea, sio taarifa, sio ripoti, kwamba kitu X, Y, Z kilitokea Bungeni, mbunge fulani akasema kadhaa, waziri fulani akamjibu kadha wa kadha.

Tujue kilichojiri kwanza, kabla hatujajikita kujadili mada. Sasa Sikonge, nambie, ni Waziri gani aliyesema kwamba wabunge mnaniandama kwa sababu mimi ni muislamu. Na mbunge alisema nini kuandama uislamu? Mbunge gani? Waziri gani huyo? Kipi kigumu, si tuwekeane rekodi ya maneno tu? Waliambiana nini kuhusu dini?
 
Status
Not open for further replies.
Top Bottom