Tupeane uzoefu wa vita dhidi ya maendeleo

ugalila

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
652
599
Kama mnavyojua wadau maendeleo ni vita, ukiwa katika harakati zako za kuhama kutoka katika kundi la umasikini kueleke katika tabaka la juu kuna watu wanakuwepo kwa ajili ya kukukwamisha kwa kujua au kwa kutokujua watu hao wanaweza kuwa ni ndugu/marafiki/wapenzi wetu na watu wetu tunaowaamini ikumbukwe pia kwa mazingira tuliyonayo watu watabaka la chini ni wagumu kuunga mkono jitihada zetu za kujikwamua zaidi zaidi wanapokuona unajaribu kujinasua wanakuwa wakosoaji wa kubwa wa njia zako za kufikia mafanio.

Ninachojaribu kutaka kupata kutoka kwenu ni jinsi gani mnakabiliana na changamoto ya watu wa karibu wanaojaribu kukukwamisha dhidi ya kujinasua kutoka kwenye umasikini. Kwani unaweza ukawa na rafiki/ndugu zako ukiwashirisha unataka kuanza biashara fulani wanakuzunguka dakika mbili mtu anakuja kukulilia shida hata kama una roho mbaya vipi unajikuta unalainika unajitoa ila kwenye kurudsha inaweza ikafanya hata urafiki/undugu wenu kuisha kwasababu ya magumashi.
 
Back
Top Bottom