Tupeane maujanja ya Excel

Naomba maujuzi ya kuandika barua kwa ku2mia excell..
Hapo lazima ujue matumizi ya vitu km kumerge cell, kuzicombine nk lkn ni bora tu ukatumia word ila km una list ya vitu ambayo ipo kwenye excel na unataka kuoanisha au kuinsert kwenye barua iliyo kwenye word unaweza kutumia mail and merge
 
Nambieni jinsi ya kujiunga na hilo grupu la telegram sasa na mm nijiunge
 
Leo tuangalie kazi ya FILL

Kuna muda unakuwa na list ndefu mfano unataka uandike namba kuanzia 1 mpaka 1000 kwenye column A , hapa unaweza ukaandika 1 kwenye A1 na 2 kwenye A2 then ukadrag lakini itakuchosha sana.

FILL inarahisisha kazi na kufill series yako bila formula wala kudrag.

Andika namba ya mwanzo unayotaka ianze (mfano 1 kwenye A1) piga enter then select cell yako, baada ya hapo click FILL(FILL ipo kwenye categories za home tab,upande wa kulia mwishoni mwishoni )

Ukishaclick,kuna list itakuja ,chagua series.
Baada ya hapo kuna kibox kitakuja, chagua column kama unataka series yako ikae vertically, au row kama unataka series yako ikae horizontally.

Kuna option nyingine hapo kati, kwa huu mfano wetu tutachagua option ya linear.

Chini kabisa utaweka step value ambayo ni 1 kwa hii case yetu, na stop value tutaweka 1000 then click OK utaona series yako imejifill ktk column A.


Matumizi yake ni mengi, kwa mfano huu nadhani mtakuwa mmepata mwanga wa kutumia hiyo fill, unaweza ukaitumia kufanya autofill ya task mbalimbali bila ya formula ama kudrag
Dah Kuna watu wachawi aiseee, big up kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafanya assumption kwamba column ya kwanza ni column A na hiyo A imeanzia kwenye A2, andika hii formula katika cell unayotaka upate average
=(SUMIF(A2:A6,"A",B2:B6)+ SUMIF(A2:A6,"A",D2:D6))/(COUNTIF(A2:A6,"A")×2)

A6,B6, na D6 unaweza ukazibalisha kulingana na ukubwa wa table yako mfano kama table inaenda mpaka A100 basi range yako pia itabidi iwe inaishia na 100 (eg A100,B100 n.k). Ukihitaji avarage ya B utabadili kwenye formula,sehemu iliyoandikwa "A" utaandika "B"
OK mkuu! Nawezaje kuzibadili numbers zilizo ktk asilimia kuwa ktk number za kawaida.
Nauliza hivyo kwa kuwa nimetumia data kutengeneza histogram graph, sasa upande wa y-axis unaonyesha number zilizo na % zake. Nataka ni-format number hizo ambapo badala ya kuonekana na % zake zionekane namba tu. Mfano, 40% ieonekane 40. Thanks in advance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
OK mkuu! Nawezaje kuzibadili numbers zilizo ktk asilimia kuwa ktk number za kawaida.
Nauliza hivyo kwa kuwa nimetumia data kutengeneza histogram graph, sasa upande wa y-axis unaonyesha number zilizo na % zake. Nataka ni-format number hizo ambapo badala ya kuonekana na % zake zionekane namba tu. Mfano, 40% ieonekane 40. Thanks in advance.

Sent using Jamii Forums mobile app
Select cells zote then right click >> format>>badilisha hiyo data type iliyoandikwa percentage na uweke General
 
Mkuu mi nataka kutengeza page ya excel ntayoweka total number ya items...na kila nikitoa item moja mfano ziko jumla 20 basi nikitoa moja ibaki 19 automatically...nikitoa ingine zibaki 18 ivo ivo mpaka ziishe. Na zikiisha inipe alert kwamba zimeisha au zinakaribia kuisha!!! Nipe mwongozo hapo
Vipi ulifanikiwa?
 
Back
Top Bottom