Tupeane maujanja ya Excel

Ethos

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
2,294
2,057
Wadau,

Kujua Excel Spreadsheets ni muhimu sana...

Tunaweza tukashirikishana tricks mbalimbali katika Excel hapa ili tujifunze wote..

Unaweza pandishwa CHEO au Kupata kazi kirahisi Kwa kujua EXCEL vizuri.. Watanzania wengi udhaifu wao upo hapo.. So Unaifanya WEAKNESS hiyo kuwa Strength kwako.Kwenye Ofisi yeyote mtu ambaye haogopi excel huwa anaonekana ni kichwa sana.. unaweza pia ukamvutia bosi wako kama utaijua kumshinda yeye na atakufanya rafiki yako ili usimuumbue...

Kwenye Interview ndio utawamaliza kabisa ..ukikutana na viherehere wakakuchokoza hapo ndio unawaonesha ujuzi wako wote... wengi huwa hawaijui kwasababu ya uvivu... Kwa hiyo usiogope..Niliwahi ulizwa swali na panelist kwenye Interview nikaenda deep mpaka akaogopa maana kuna vitu alikuwa havijui na yeye akaamua apotezee hilo swali akarukia kitu kingine kukwepa aibu..

Weka Trick yako hapo chini ili wengine wafaidi au kama unaswali uliza nitakujibu mimi au wadau wengine...

Ingependeza sana pale unapokwama uulize swali hapa.. Ili tujadiliane vitu ambavyo ni useful katika mazingira yetu ya shule au kazini...

Dunia ya sasa sio lazima uende darasani.. Unaweza tumia muda wako na MB zako vizuri mtandaoni na ukaongeza Ujuzi polepole

**Kama unatafuta kazi na umeandika Kwenye CV kwamba una ujuzi na Excel fuatilia huu uzi na group uwe updated na vitu mbalimbali ili usije umbuka siku ukiwa unafanya written au Oral Interview

** Nitakuwa naelezea Common questions ambazo waajiri hupenda kuuliza kukupima uelewa wako katika Spreadsheets.. Ni Muda na MB zako tu.. Sihitaji kingine...

Please NOTE

** Usiulize kitu unachokijua kupima watu Bali andika trick unayoijua ili wengine wafaidi na kama unaswali ULIZA wataalam tutakusaidia

PS:
Kama upo Telegram unaweza Ingia Kwenye Public Channel ipo hapo chini Kwa vitu ambavyo haviwezekani kuelezewa hapa vizuri..Kama video na files. Ni public channel ya kusoma na Sio sehemu ya chatting!

Naomba kuwasilisha!

Ethos
 
Njoo upate hayo maujanja ofisini kwetu The Computer Skills (ComSkills), Makumbusho Business Complex, 2nd Floor kuanzia saa 2 asub mpka 2 usiku. You will not be disappointed. Call 0717718519
Nataka watu wote wafaidi hapa... Ndio maana nimeanzisha uzi... Mnaweza mkatoa hints hapa ili tujue umahiri wenu..

Binafsi nataka kuanza kufundisha hapa bure kabisa
 
Nataka watu wote wafaidi hapa... Ndio maana nimeanzisha uzi... Mnaweza mkatoa hints hapa ili tujue umahiri wenu..

Binafsi nataka kuanza kufundisha hapa bure kabisa
Mkuu mimi nataka kutengeza page ya excel nitayoweka total number ya items... na kila nikitoa item moja mfano ziko jumla 20 basi nikitoa moja ibaki 19 automatically...nikitoa ingine zibaki 18 hivyo hivyo mpaka ziishe. Na zikiisha inipe alert kwamba zimeisha au zinakaribia kuisha!!! Nipe mwongozo hapo
 
Njoo upate hayo maujanja ofisini kwetu The Computer Skills (ComSkills), Makumbusho Business Complex, 2nd Floor kuanzia saa 2 asub mpka 2 usiku. You will not be disappointed. Call 0717718519
Hivi ukiandika hapa unaonaje?

1. Tuanze na hili maana watu hawasemi nini shida....
Kwa mfano unataka kuunganisha maneno mawili yaliyopo kwenye cell mbili tofauti... kwa mfano
-saba kwenye cell moja,
-saba kwenye cell nyingine
 
Nataka kujua namna ya kuweka 00, mwanzo wa namba mfano nikitaka kuandika namba moja 1, ianze na 001, hivyo hivyo mpaka mwisho
Asante Kwa Swali Lako Mkuu..

Nenda Kwenye Cell unayotaka iwe affected.. Right Click nenda hadi Kwenye FORMAT CELLS then click baada ya hapo zitatokea options nyingi chagua CUSTOM then upande wa kushoto inatokea options kibao ambazo zinaanza na ## futa weka 0 kulingana na idadi unayotaka then Drag..


Natumaini nimeweza kukujibu. Karibu Kwa Swali lingine...
eeb636925330c0bc626d85e01dd54f9c.jpg
 
Hivi ukiandika hapa unaonaje?

1. Tuanze na hili maana watu hawasemi nini shida....
Kwa mfano unataka kuunganisha maneno mawili yaliyopo kwenye cell mbili tofauti... kwa mfano
-saba kwenye cell moja,
-saba kwenye cell nyingine
Kama nimekuelewa vizuri,

Ni rahisi sana... Nenda Kwenye FUNCTIONS then chagua special function ya CONCATENATE then fill Arguments Kwa kutumia CELLS references ambazo hizo namba zipo.. Kama 7 ipo Kwenye A4 iandike na kama 7 ingine ipo Kwenye A6 iandike halafu bonyeza OK


Au unaweza andika

=CONCATENATE (A4,A6)
 
Back
Top Bottom