Tupeane Machimbo ya Bidhaa za wanafunzi/shule Kuelekea January

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Tunaelekea kipindi ambacho Mahitaji ya Wanafunzi kwa ajili ya shule ndio kipaombele zaidi, tumeshatoka kwenye nguo za sikukuu n.k. Sasa tuna Switch ON upande wa pili.

Ni kipindi kifupi sana ila kinaweza kikupe mwanga mzuri kiuchumi ukipatia,

Tusichoshane, tupeana machimbo ya bidhaa hizi kwa bei ya jumla na iliyopoa,

Counter Books
Daftari ndogo za msomi n.k
Kalamu
School bags
Uniforms
Soksi
Viatu
Na chochote kama nimesahau

Tusiwe wachoyo katika hili, Wengi humu tupo mbali mbali sidhani kama ukimsaidia mtu humu ndio huyo huyo atakuja kukuharibia soko lako.

Mambo ya PM, tuyaache.

Saidia kwa kutaja bidhaa gani inapatikana maeneo gani na bei yake.

Unaposaidia nawe una saidikika, Funguka, Unaweza ufiche chimbo lako ukijua ndio mwisho kumbe mwenzako ana chimbo zuri zaidi.

Binafsi kuna machimbo nayafuatilia, nikasha fahamu ukweli wake nawaletea update hapa.
 
Me nawatafuta wale jamaa wa keko wanauzaga Matranka (Masanduku ya chuma ya wanafunzi) kwa bei ya jumla nilikuwa na namba zao nimepoteza afu niko mkoani
 
Ni wapi naweza pata oxford dictionary (English-swahili) kwa bei ya jumla.
K/koo nimezunguka Mawinga ni wengi na hawataki kutoa connection ya Machimbo yao.
Nahitaji kama 60 hivi.
 
Naomba kufaham chimbo la mifuko hii ya packeges. Kupakia Bidhaa kama karanga, Michele nk...
 
Back
Top Bottom