Shairi: Tupe Nguvu Subihana!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
TUPE NGUVU SUBIHANA!
Na. M. M. Mwanakijiji

(Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.) Quran 1:5

Bismillahi naanza, kwa jina lake Rabuka,
Maliki alo wa kwanza, aloumba Malaika,,
Jalali mwenye uweza, Karima Muabudika,
Kheri zake atujaza, asiye na mshirika,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Ya Rabi twakimbilia, machozi yatudondoka,
Sisi wana Tanzania, madonge yametushika,
Zahama imetujia, taifa limeshtuka,
Yale tunashuhudia, ya mambo ya kimizuka,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Ngombe ulotujalia, wachache wamkamua,
Na ndama aliyezalia, naye wamemchukua,
Twabaki twaangalia, wenyewe wakikenua,
Mitima imeumia, kwa mambo ya kuchefua,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Mvua imeanza nyesha, sasa wanatetemeka,
Dalili umeonesha, kwamba umetukumbuka,
Na njia umeinyosha, sasa wanahangaika,
Mola wawapagaisha, tabasamu zawatoka,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Wale walotuibia, toka Benki yetu kuu,
Hawa twawatangazia, mwishoni wenu mwaka huu,
Vyote mlivyogaia, wanenu na wajukuu,
Hivyo mtatuachia, hakuna tena suluhu,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Na viongozi wazembe, mashujaa wa uvivu,
Na kiburi kama pembe, yamewavimba mashavu,
Mmekinywa kama pombe, ugimbi ulo mkavu,
Mmenona kama ngombe, mkepeana malavu,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Leo mnakamatana, ushirika wa wachawi,
Tena mmegeukana, mlojifanya viziwi,
Na sasa mwatafunana, mafisadi hamjuwi,
Kwa matendo mlikana, ya Mola hamtambuwi,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Ee Mola tunakuomba, wazee nasi vijana,
Waumbue walokomba, mali zetu kwa hiyana,
Na walie kama komba, ulanzi kutouona,
Waja wako tukaimba, Mafisadi kukiona,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Tuwashinde na usiku, na tuwashinde mchana,
Na tuwatoe mkuku, iwashukie laana,
Kwani hii ndiyo siku, uliyoifanya Bwana,
Umetujaza shauku, tumedhamiria sana,
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Nakoma kusema sana, adui kadhamiria,
Mafisadi mtaona, kwani mmejitakia,
Nyuma haturudi tena, twailinda Tanzania,
Wa kijiji nimenena, pingu zawasubiria
Tupe nguvu Subihana, tuwashinde mafisadi!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

NB: MoD ikiwapendeza mwaweza kuirusha kwingineko!
 
Tumwombee nguvu za ziada na busara nzito Rais wetu, mashahidi wote, Mahakama yetu na wadau wote wapenda haki na amani kwa Nchi yetu ili HAKI itendeke na ionekane wazi inatendeka na mali za Watanzania zirudishwe ili zitumike kwa manufaa yetu sote.
 
Mathayo 7:7 na Yeremiah 3:33(33:3)

Hii ya Yeremiah inasema hivi "Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo magumu usiyoyajua".
 
It is the time that will tell
Who shall win or fail
What we did,do,shall do or done
Yesterday, now or in the long run
I say with faith and this is real
That the truth at last shall prevail
 
Tumwombee nguvu za ziada na busara nzito Rais wetu, mashahidi wote, Mahakama yetu na wadau wote wapenda haki na amani kwa Nchi yetu ili HAKI itendeke na ionekane wazi inatendeka na mali za Watanzania zirudishwe ili zitumike kwa manufaa yetu sote.

- Maneno mazito sana haya mkuu, tupo ukurasa mmoja hapa.
 
Mwanakijiji I am not sure if you have spelt the word correctlly, it should be SUBUHANA and not SUBIHANA. I stand to be corrected!!
 
Since misspelling GOD"S name is blasphemous can someone tell me which is correct; is it SUBUHANA or SUBIHANA asd claimed by the villager.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom