Tupe mkasa wako ulivyoishia kumuoa uliyedhani utapiga na kusepa

Nimejiwekea vitu viwili katika maisha haya.

1. Sitakua na mtoto wa nje ya ndoa

2. Hakuna mimba yangu itatolewa.

Sahivi nina 30yrs na bado hii miiko miwili sinaivunja.
Hujafa, hujaumbika. Muda ni Mwalimu mzuri sana. Mungu akusimamie katika hilo.
 
Miaka ya nyuma kidogo kuna jamaa yangu alienda mbeya huko vijijini ndani ndani kuna mishe gani sijui alikua anapiga huko. Sasa jamaa kutokana na hali ya kule baridi na nini akakamatia guluguja moja matata akawa anaso
Utoto ulimsumbua but trust me jamaa anaweza kuwa na amani ndoani kuliko waliooa pisi kali
 
Ninachokumbuka tu ni kwamba niliodhani nitawaoa na nilipowaacha walifeli hadi mitihani ya kidato cha nne.Walipata zero kabisa na lawama zikaangukia kwangu.Utoto ni shida sana🤔🤔🤔🤔
 
Baada ya kumaliza chuo, nikatafuta kashule kujishikiza nikisubiri ajira ya nilichosomea. Kuna wiki nilikua mwalimu wa zamu, ukiwa zamu unakaa skuli hadi weekends jmos na j2.

Sasa jumamosi hiyo akaja huyo binti. Aliwahi soma hapo kabla sijaja, kaja kufata vyeti vyake.. nkamwambia vyeti vinakaa ofisi ya mkuu, na mkuu yupo siku za kazi. Nikachukua namba kwamba jumatatu kabla hajaja nimcheki kama mkuu yupo au laa.

Siku ile ile nkaanza mtongoza kwa simu. Na wakati huo plan yangu ilikua nipite tuu maana nilikua na mchumba wangu nesi ambae nasubiri nipate ajira rasmi nioe.

Siku nyingine ya kazi kaja kuchukua cheti, jioni kapitia geto, ingawa alininyima mzigo kisa bado mapema.. ila weekend inayofata alikuna geto na akanipa mzigo.

So nikawa na mademu wawili rasmi. Tatzo likaanza, nkaona namna anavonihendo huyu denti, ni tofauti na mchumba wangu nesi.
Denti akawa so romantic, ananiita mume wangu, ananijali mno. Basi nkawa naendelea kumla. Ghafla mimba hii hapa. Na nilijiwekeaga kwamba sitakuja kutoa mimba yangu. Nkasema usitoe ntaitunza.

Nahisi kwao walimshawishi ahamie maana nkaona anahamishia kimoja kimoja. Siku akija geto anaondoka baada ya siku 3, mara wiki mara akahamia mazima..

Nkafanya process za posa, nkalipa mahali, akajifungua sahv dogo ana 4yrs. Mwaka jana 2019 nmefunga nae ndoa. Na sahiv ni mama k.

Back to nesi, ile me kuoa ilimvuruga sana. Sababu anasema alikataa wengi kisa alikua na uhakika na mimi. Age ilikua imesonga alkua na 27yrs ile 2017. Mwaka jana nilipofunga ndoa yeye akiwa na 29yrs akagive up kuhusu kuolewa, akaamua atafute mtoto.. katka kutafuta mtoto akakutana na jamaa kumbe ni hiv +. So nesi nae akaukwaa. Mimba akipata zinatoka. Hadi sahv bado hajapata.. (Hizi story nazipata kwa shosti yake ambae me ni rafiki)
Dah! Imeisha vibaya ya nesi.
 
Si kitu poa.. huwa namuonea huruma mno. Lkn sikua na namna na sina namna mpaka sasa. Sababu nmeshaoa na mke nilieoa sina kasoro yoyote naiona kwake. Ni mke bora kabisa..
All is well. Sio lazima mchumba awe mke. Hamna haja ya kuwa guilty. Ni bahati mbaya hamkuweza kuwa mume na mke. kulinda afya yake ni wajibu wake.
 
Kweli kabisa mkuu, sikufikiria kumuoa japo tulipendana sana lkn yeye ndio alikataa na kuniambia wala usiweke hilo akilini mwako,
Na hayo aliniambia baada ya kupata mimba aliacha kwenda kujiuza akaniomba nimsapoti adi mtoto akifika mwaka atalea mwenyewe maana hakua na akiba kubwa japo ktk uchunguzi nkajua ana m4 bank nkapotezea,
Yaani akiwa na mimba tuliishi km tumeoana anaeza lala home hata mwezi ndio anarudi kwao, alikua akinipikia, kufua na mengineyo adi kajifungua.

Ni mwanamke mzuri mwenye hashima sana pamoja na kujiuza hana zile tabia mbovu kama wengi wao walivyo.
Hawa wakibadilikaga huwa wanakuwa watu Pouwa sana. Nimekipenda kisa chako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom