Tupaze sauti zetu kwa watawala, tusijekosa wa kutuzika

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
4,829
6,376
Asalam Aleikum, Bwana apewe sifa, tumsifu Yesu Kristo. Nakusalimuni nyote kila mmoja kwa imani yake.

Ninaitwa Britho Lihakanga, ninaishi Tabata. Najua mtashangaa kuona leo ninaanika details zangu wazi. Sina uhakika na kesho yangu.

Kwa kifupi ni kwamba nina siku ya tano leo, nikipigania kesho yangu. Si kwa maana ya juma lijalo, la hasha ni siku inayofuata baada ya leo.

Ninajifukiza usiku usiku na mchana, mara ninapata nafuu, mara ninazidiwa. Sijakata tamaa, ninapigania uzima, japo ni Mungu tu ndiye anayeninusuru.

Nipo kitandani, sina hata hamu ya kuangalia TV, nikiulizia taarifa za habari zimebeba jambo gani zito, ninaambiwa misiba sana na karibu kila kona ya nchi ni misiba inayotokana na kushindwa kupumua vizuri.

Nimepata wazo kuwa tutakwisha huku mamlaka zimekaa kimya. Ni misiba ya wakubwa tu inatangazwa. Nina uhakika digidigi huku chini tutakuwa tunapukutika.

Tupaze sauti, vinginevyo tutakwisha. Tumwabie baba Jesca, lockdown haikwepeki, japo ni ile ya kiaina, shule zifungwe, tupunguze msongamano usio wa lazima na kila mmoja aseme wazi kwamba covid 19 is back and it is in another level.

Nikipona nitakuja kuandika tena. Vinginevyo, BuURIANI nyote ndani na nje ya JF.
 
Pole sana. Utapona kwa sasa zidi kua karibu na Mungu. Watawala hawatakusaidia wewe kupona hasa wakati huu.
 
Sawa mkuu. Kila heri! Ikitokea ukatangulia basi usiwe na kinyongo maana na sisi pia muda utakapowadia, tutaungana nawe huko paradiso.

Ila utapona tu. Hivyo endelea kupambana na kuchukua tahadhari kama sisi members wenzako. Si unafahamu katika hili kila mtu anapambana kivyake? Usikute hata Baba mwenye nyumba wako muda huu naye anajifukiza na kubugia supu ya malimao kama hana akili nzuri vile.
 
Pole sana, lakini Mungu hutenda lake pale anapoona inafaa. Tunakutakia afya njema tukismini utatimiza ahadi yako ya kuandika tena baada ya kupona
 
Ukiwa mtenda maovu siku zote lazima ugope kukutana na Mungu,.
Na ni kweli Mungu atakuchoma kwa maovu yako.

Ila kwasisi watenda mema hata kifo kitupitie leo safi tu tena wala hatuliilii kama mwanangu Wa Tabata.

Kuna wengine humu wapo tayari hata kubeba mabomu na kwenda jiripua.

Ukiona mtu anaogopa kifo ujue mtenda maovu.
 
Jiulize jambo,kujifukiza kunaongeza ama kuounguza oxygen kwenye mapafu?,ukipata jibu utajua usahihi ni kiacha ama kuendelea
 
Usisahau kunywa maji mengi ya moto kama yale ya chai kila wakati ni dawa ya kupunguza nosal and throat congestion, na kurekebisha blood circulation,
 
U
Usisahau kunywa maji mengi ya moto kama yale ya chai kila wakati ni dawa ya kupunguza nosal and throat congestion, na kurekebisha blood circulation,
Mambo ya afya waachieni wataalamu.

Mlishindwa kuwapa michai chai kina Balozi Kijazi kupunguza hizo congestion au kurekebisha hizo circulation?

Acheni usanii wauaji nyie.
 
Pole sana kama kweli unaumwa, Mungu akusaidie upone, Hili ni janga la dunia na ukweli hakuna mwenye na jawabu la moja kwa moja kwa sasa, lockdown haisaidii hata nchi zilizoweka lockdown hazikusaidika.

Jibu ni kila mmoja aelewe namna ya kujikinga. taasisi zetu za dawa zimetoa dawa tumia ila huwezi shindwa kununua, vitunguu saumu,vitunguu maji, limao,tangawizi,pilipili, tengeneza juice kama una Asali weka na tumia itakusaidia.

Usisahau Kunywa maji ya vuguvugu, Matunda kwa wingi na punguza Mafuta
 
Back
Top Bottom