Tupate wapi mtu kama huyu?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Tangu Baba wa taifa alipofariki duniani mnamo mwaka 1999 taifa hili limeshaharibu mimba sana! Sio kwamba mama Tanzania hazai kabisa, la! Anazaa sana, ingawa wale anaotuzaa sasa wengine ni mapooza, wengine hamnazo, wengine nafuu, na wengine afadhari.

Kwa sababu hiyo, kama taifa tumekosa utengamano wa kisiasa, kiuchumi, kijamii, au hata kiundugu. Ndiyo maana leo adui mkubwa wa mtanzania ni mtanzania mwenzake. Tumefika mahali wale tuliosifika kwa umoja, eti kwa sababu ya tofauti za kimtazamo, leo ni maadui wa kutisha! Kimsingi maisha tuliyonayo sasa yanatisha sana ingawa kule tuendako yatatisha zaidi.

Kwa usalama wetu ni nani atatengeneza mahali palipobomoka? Au tupate wapi mtu kama huyu?

Mtanzania mzalendo, ambaye hanunuliki wala kuuzwa hata kama mbingu zianguke chini. Mtu wa watu kwa ajili ya watu. Yule ambaye hatakuja kutumikiwa lakini kutumikia wengine. Mnyenyekevu atakayerudisha mamlaka ya nchi kwa wenyenchi.
Huyu sio wale wanaozima vipaji vya wengine, bali atakayevichochea na kuvitumia kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mtu ambaye umaskini wa watu wake unamuuma kuliko wa kwake.
Aliye na dhamira ya kweli isiyo na unafki ndani yake. Mwenye uwezo wa kuwageuka wenzake wachache, kwa ajili ya manufaa ya wenzake wengi.
Hakika atakuwa baba wa taifa la maendeleo. Kama tulivyo na baba wa taifa wa uhuru.
Nauliza tena "Tupate wapi mtu kama huyu"

Kama yupo semeni ili tusiomfahamu tumjue, na kama hayupo tufanyeje ili tumpate?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibaya zaidi watu ambao walikuwa ni wanafunzi wake na wenyewe now wanaondolewa kwenye wadhifa zao like mahiga

Nadhani moja kati ya watu wanaofaidika na kutokuwepo kwa nyerere ni bichwa maji BASHITE

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Kibaya zaidi watu ambao walikuwa ni wanafunzi wake na wenyewe now wanaondolewa kwenye wadhifa zao like mahiga

Nadhani moja kati ya watu wanaofaidika na kutokuwepo kwa nyerere ni bichwa maji BASHITE

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Taifa la mang'ombe
 
Back
Top Bottom