SoC01 Tuorodheshe ushirikina kwenye ile vita ya Maadui Watatu...yaani sasa iwe Vita dhidi ya Maadui Ujinga, Umasikini, Maradhi na Ushirikina

Stories of Change - 2021 Competition

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Niliwahi kuja na andiko humu nikionesha huzuni yangu juu ya Kiongozi mmoja wa juu tena mwenye hadhi ya Udaktari aliyekuwa anaithibitishia Jamii kwamba kuna Mama kutoka eneo moja la nchi aliyekuwa na uwezo wa kushambulia Maadui zake akiwatumia Nyuki kwa njia ya nguvu za giza.

Kama haitoshi kumewahi kutokea kauli kama hiyo ya kuhusisha nguvu za giza kutoka kwa Kiongozi mmoja Mkubwa wa Nchi wa awamu iliyopita, yeye aliwaaminisha Watu ya kuwa kulikuwa kuna Wafanyakazi fulani wa barabara walijikuta wamelala nje ili hali walikuwa wamelala ndani ya Gari. Pia juzi juzi hapa tuliwasikia Jeshi la Polisi wakihusisha tukio la Askari kushindwa kumlenga Fisi kwa risasi kuwa lilikuwa na viashiria vya ushirikina.

Mambo haya kiukweli ni hatari sana kwa ustawi wa jamii inayopambana kujenga uwezo wa kutatua changamoto zake.

Ni kukosa bahati kwa hali ya juu kwamba Wengi wetu hatuioni hatari inayoikabili Jamii kutokana na janga hili.

Ni hali ya kutamausha sana pale unapokutana na Mtoto mdogo anayeanza kuamini kwamba kuna uwezekano wa Binaadamu kugeuka Paka au Nyoka/Chatu, au kuna uwezekano wa Mti uliokatwa kurudi na kusimama tena au kugoma kukatika.

Ifike mahali Serikali ijitenge kabisa na imani hizi na kuwe na sheria ya kuwazuia Viongozi, Watumishi wa Uma au Wasemaji wa Serikali kushadadia au kuhusisha tukio lolote na ushirikina kwa wakati wote wanaotumikia ofisi za uma. Na kuwe na utaratibu rasmi wa kutoa taarifa sahihi na elimu kila mara inapojitokeza taarifa potofu zinazoikanganya jamii.

Babu au Bibi anapohojiwa kwenye chombo rasmi cha habari na akasema kuwa Ziwa Ngozi ni la maajabu kwamba haliingizi wala kutoa maji basi hapohapo Chombo husika kiwajibike kutoa taarifa rasmi na sahihi kumsaidia Kijana Mdogo anayesikiliza ili naye asije kufikia mpaka kuwa Profesa na bado akaeneza taarifa potofu kwa wengine.

Tusitarajie kama tutakuwa na Kizazi kitakachoona haja ya kukaa maabara na kutafuta chanzo cha matatizo kwenye jamii zao kama tayari vichwani mwao wamebeba dhana hizi za kishirikina. Nani ataiona haja ya kuumiza akili kujua chanzo cha Watu wake kuugua kama tayari Jamii hiyohiyo inamwambia tatizo lililopo limesababishwa na kulogwa?.

Na tumeshashuhudia namna ambavyo imani hizi zinawasumbua hata timu zetu za Mpira. Vikongwe wanauwawa, Walemavu wa ngozi wanuwawa, ndugu wanauwana...na hakuna juhudi za wazi za kupambana na ujinga huu kwani hata Wasomi na Viongozi wetu wengi nao ni sehemu ya tatizo.

Tukuze Jamii inayotafuta taarifa na kutumia akili. La sivyo tutawategemea Wazungu kwa kila kitu na sisi kubaki kama Wasindikizaji tu hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom