Tuorodheshe kero zinazowanyima raha walipa kodi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuorodheshe kero zinazowanyima raha walipa kodi wa Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngararimu, Jan 19, 2012.

 1. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Wana JF mimi ni mlipa kodi wa tanzania ambaye naumia sana kila ninapofikiria namna ya kutimiza jukumu langu la kikatiba la kulipa kodi. sababu zinazonikera zipo nyingi nimeona ni vizuri nianzishe uzi huu ili tuorodheshe kero zetu na mapendekezo ya kuondoa hizi kero tuliyo nayo huenda TRA wakayachukua na kuyafanyia kazi ili kutupunguzia shida.
  Pia kama TRA watazifungia macho basi zitakuwa zimewekwa wazi ili members ambao ni wabunge waliomo humu jukwaaani waweze kuzichukua waende nazo mjengoni kikao kijacho cha bajeti.
  karibuni tuchangie.

  1. kodi kubwa mno inatozwa kutoka kwenye pato la ajira PAYE
  - PAYE ishuke kutoka asilimia 14 mpaka 10 na jitihada zielekezwe katika kuhimiza wafanya biashara waliosajiliwa VAT watumie mashine za Kutolea risiti kikamilifu ili kuongeza kodi ya VAT inayolipwa na walaji kila mwezi - hatua hii itaziba pengo la kushuka kwa PAYE
  2. ..........................................................................
  3............................................................................
   
 2. M

  Mtazamotu Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Kuhusu suala la PAYE nadhani hiyo uliyoitoa (14%) haitoi uhalisia, hebu jaribu kucheck hapo kwenye note chini. Suala la msingi hapa pamoja na kupunguza asilimia tajwa kwa kila kiwango pia wanapaswa kupandisha kiwango cha mwisho i.e 720,000/= ili mtu ahesabiwe kuwa high tax payer na kukatwa 30% ya kiasi chote kinachozidi 720,000. Kiukweli hiki kikomo kinahitaji kuwa angalau 1,500,000\=Note; PAYE = IF(TTV>720000,112500+(TTV-720000)*30%,IF(TTV>540000,75000+(TTV-540000)*25%,IF(TTV>360000,39000+(TTV-360000)*20%,IF(TTV>100000,(TTV-100000)*15%,0))))where TTV means Total taxable value.
   
 3. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Duh! Bei za Vitu kupanda kiholela ni kitu kinachotuumiza zaidi end users. Unakuta mtu umepanga budget yako ya mwezi, ukifika dukani unakuta bidhaa ulotaka kununua imepanda kwa asilimia 250%. Hii inatulazimu kuishi bila budget, twafaaaaaaaaa
   
 4. m

  moghaka JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Asante sana mkuu kwa wazo zuri sana,
  Kwa mfumo wetu wa kodi ulivyo against mlaji katika soko la ushindani ni vizuri kujua kuwa mfanyabiashara ni middlemani tu hasa VAT, Tambua kila unapo ongeza kusajili wafanyabiashara kuingia VAT maana yake bidhaa kupanda bei kwa mlaji proportionally.
  Kuhusu kero, TRA wafikia hatua mbaya isiyo na tija kabisa kiuchumi, ni wazi kwa TRA kwamba ujinga(kutoelewa) wa mfanyabiashara ndio kodi kwa TRA na Rushwa, hawana nafasi hata kidogo ya kuelimisha mteja.
  Pili, TRA wamefikia hatua ya kugushi(forge) documents za mlipakodi na procedures kwa kushirikiana auditors ili kufanikisha kunyang'anya Kodi isiyolipika hadi biashara inafungwa na wao wanajisifia kwa kuwa na uwezo huo wa kufilisi biashara waziwazi.
  Tatu,TRA ni wala RUSWA wakubwa sana kwa kila hatua na ngazi.
  Nne,Utaratibu wa ukaguzi mahesabu(AUDITING) ndio wakati wa kukusanya rushwa na kufilisi watu(hakuna hesabu wala gharama hata moja watakayo kubali bila rushwa)== vyoote hatimaye ni mzigo kwa mlaji...ntaendelea baadae. . . . .
   
Loading...