Tuongee Ukweli Kuhusu Haji Manara

Nitaendelea kuheshimu mchango wa manara pale Simba no matter what!

Huyu barbara hana uwezo wa kushawishi shabiki aende uwanjani!
Halafu ni kiongo kiongo tu, kimeandika eti Simba imetimiza malengo yake kwa kufika robo final ya Africa, wakati kila mtu anajua lengo ilikua ni nusu final,

Hana uwezo wa kuwaaminisha wachezaji wa Simba, "kwamba pamoja na udogo wa majina yenu, mna uwezo wa kumpiga Al ahly kwa mkapa"

Na Al ahly akafa kweli,
View attachment 1871468
Simba lengo lake lilikuwa makundi, hayo ya nusu fainali ya kwako.
Aliyeset target anasema amefikia malengo, ila wewe mwenzangu unasema hapana.
 
Tanzania iliuweze kufanikiwa au upate umaarufu wewe kuwa mtu wa mambo ya HOVYO HOVYO utapata umaarufu na pingine kufika mbali kwenye maisha.

Mifano ipo mingi sn ya watu sample hiyo kuanzia WASANI, SIASA hadi viongozi wa DINI.
 
Ukweli mtupu umenena ila,kwa weredi wake huo na ukubwa wa jina lake ulimfanya awe na kiburi,mfano wa kiburi cha Haji ni kufokea waandishi wa habari baadhi yao kuwaambia anatamani wasije kwenye press zake.

Kingine ni kutoa maneno machafu kwa bosi wake,lakini akuhishia hapo voice note yake ya pili anasema hivi"hawa watu ni wabaya sana wanaweza kuniwekea hata unga au kinifanyia kitu kibaya"hao watu wanaoweza kumfanyia Haji kitu kibaya ni Mo, Barbara na Hanspop au ni kinanani hao?
Ukweli usemwe licha ya mapungufu ya manara ila hawa waandishi wa habari kiukweli wana hila na chuki mbaya sana dhidi ya simba. Hapa manara alikua sahihi kuwaita takataka

Mtu kama kitenge na dauda hata humu wamejadiliwa sana kwa chuki zao wanazozionesha dhidi ya simba, kupitia tukio hili unaweza kuona ni namna gani swala hili la manara kwao limekua ni sherehe kubwa sana.

Imagine manara kaachia ngazi kwa maamuzi yake alafu headline ya kitenge kwenye tukio hilo la manara imesema MANARA ABWAGWA

Kero ya manara, ni mtu wa sifa sana na asiyeheshimu mipaka yake ya kazi. Kipindi kile mo dewj hafahamiki yuko wapi manara akajitokeza kama msemaji wa familia ya dewj.

Manara alithubutu kuingiza habari za siasa kwenye michezo huku akijua wazi timu iliyomuajiri inahusisha mashabiki kutoka pande tofauti tofauti za vyama.

Kuna siku manara alikua anaisifia simba akiifananisha mipango ya bechi la ufundi la simba kua ipo madhubuti kama chama cha mapinduzi. Hapa manara kaingiza siasa kwenye mpira kinyume na majukumu yake ambayo amepewa ayatimize kwa ajili ya club na mashabiki ambao wanatofautiana kivyama

Kingine huyu manara ni mkurupukaji, naamini kabla ya ku leak ile clip hakushirikisha ubongo ilikua ni mwemko tu ambao naimani baada ya hapo alijuta.

Alitegemea kuona support nyingi kwa upande wake kwa imani aliyojiaminisha kua anakubalika sana na wanasimba kwa kufananisha na mpinzani wake barbra ambaye ni mgeni

Kitu kingine nilichokiona kwa manara baada ya ku leak ile clip, nadhani alitegemea kuona MO atamsuport au kusema chochote ambacho kitam favor.

Na ndio maana alipoona kimya ni kama manara alichukia akawa anapost bidhaa za bakhresa kwa mfululizo kila wakati kama kumkomoa vile MO. Kuna post moja akitangaza maji ya uhai ya bakhresa aliandika caption kua "haya ndio maji bora na salama kuliko yeyote hapa tanzania"

Nadhani alifanya hivi ili kudhihaki maji ya masafi ya mo, nasema hivyo kwasababu hana kawaida ya kuandika caption yenye elements za kushusha bidhaa zingine especially kama hizo bidhaa pia MO anazo
 
Manara hajafukuzwa tatizo mashabiki wengi ni wajinga

Manara kaandika barua ya kuacha kazi mwenyewe bila kulazimishwa na mtu.
Watopolo ndiyo wajinga kwenda kumbeba msomali anayewahadaa kila siku. Tumia lugha yoyote ile lakini ukweli Haji kafukuzwa Simba. Leo hii uto ndiyo watetezi wa Haji?
 
Pole sana , unamchukia mtu ambaye hakujui na anapiga pesa ndefu kwa kazi yake, wewe kumchukia imekuongezea sh ngapi kwenye akaunti benki, hapo mnafurah kua anaenda kuanguka, mtu ana mamikataba kibao na deals za kampun kubwa na subiri utachukia zaidi siku chache zijazo wakat akilamba dili zito la azam
Atleast hatokuwa tena na ile nafasi ya kuikejeli na kuitukana timu iliyomlea na kumlisha alipokuwa mdogo kupitia mshahara alio lipwa baba yake wakati akiwa ni muajiriwa na mchezaji mahiri wa Yanga.

Ezekiel Kamwaga hana tofauti na Hassan Bumbuli! Wote ni Waandishi wakongwe wa habari! Watatumia vizuri taaluma zao kutuhabarisha. Na siyo kutukana au kukashifu timu nyingine.
 
Sema nini..liManara linajua kuhamasisha watu waende uwanjani hasa match za kimataifa.

imagine mtu anashuka ndege (timu ngeni) anasikia "WAR IN DAR"
Hatukatai lkn izo idea za War In Dar sio zake peke yake kuna watu behind the scenes wanakuja nazo ndo wanafny implementation kwa kuwapa wapige mdomo kama kina Haji wafanye promo lkn usidhan iyo idea ni mawazo yake binafs.

Wanasemaga Ngoma ikilia sana inakarbia kupasuka kwhy Haji kafanya mazr yake lkn pia alikua na uswahili wake ngj akapumzke atafute changamoto nyngne.
 
Manara hakuibeba simba,ila simba ndo imembeba,kama ni yeye basi aende mwadui fc akaibebe tuone

manara ana mchango mkubwa sana sio simba bali katika soka la ukanda huu, nakumbuka pia jarida la the east african walishampa special respect katika soka la afrika mashariki, wewe unaweza kumchukulia poa kwa sababu mo amekuja na ela ila simba ile iliopita ambayo yanga walikua hawashkiki ndo umuhimu wa manara unatoa uko!

- Na pia lazima ufaham mashabiki wengi wa simba ni wa juzi juzi baada ya hamasa, mpaka wanawake saaahv wanashangilia mpira, kwa kifupi ni kwamba manara ni exceptional ukanda huu
 
Hakua anatunge ile misemo yeye ile ulikua inabuniwa na jopo la wanahari wapale msimbazi afu yeye anakuja kuongea public

kutunga ni swala moja na kutia uchizi mashabiki ni swala lingine, hata wewe umeenda shule ukasoma kila kitu lakini ulivokuja kwenye swala la kuapply kwenye maisha cha moto ulikipata
 
Nadhani alifanya hivi ili kudhihaki maji ya masafi ya mo, nasema hivyo kwasababu hana kawaida ya kuandika caption yenye elements za kushusha bidhaa zingine especially kama hizo bidhaa pia MO anazo

Moja kati ya faida nyingi za elimu ni mtu kuwa makini kwenye kufanya mambo yake ya kilasiku,lakini pia hekma na busara zinampa msaada mkubwa mtu kwenye maisha ya kilasiku,nasikitika kusema kwamba bwana Haji hivyo vyote hana.
 
Huyu barbara hana uwezo wa kushawishi shabiki aende uwanjani!
Sio kazi yake, na wala sio lengo la klabu. Simba iliichapa timu kali bingwa wa Nigeria (Plateau) goli 1-0 huko ugenini ikicheza bila mashabiki wa msimbazi. Simba iliichapa timu kali AS Vita Club goli 1-0 huko ugenini ikicheza bila mashabiki wa msimbazi. Simba ilitoka sare na timu kali El-Mereikh ikiwa haina mashabiki wake wa msimbazi. Kikosi kikali ndicho kitakachoamua matokeo ya uwanjani
 
Hii kasumba mpya, kwamba kila msemaji wa timu ili aajirike; lazima awe fundi wa maneno, vijembe, uropokaji ni utaratibu wa ovyo.

Manara na jerry mulo ni waasisi wa type hii ya ovyo ya kuvisemea vilabu vyao.

Eti kwamba kama huna mbwembwe umekosa sifa ya kuvisemea vilabu ni kinyume na kusudi la kuwa na kitengo cha habari kwny tim zetu.

Wengne wa type hii ni kifaru na bwire (niliwasahau)

Mimi sijaoina faida ya kuwa na aina hii ya wasemaji.

kama ni hamasa..hamasa itakuja yenyewe tu kama kandanda linatandazwa.

Maximo aliibua hamasa iliyokuwa imepotea kwa miaka mingi kwa vitendo/matokeo yaliyokuwa yanatokea sio kwa kupiga domo.

Huko nyuma wasemaji pia walikuwepo na mambo yalienda.

Akina manara type hawawezi kuwepo kwny vilabu vyenye mafanikio nje ya bongo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom