TUONGEE NA HONDA AU TOYOTA WAJE TZ

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,538
6,456
1. Kenya wameshaunda gari za Volkswagen polo, wataanza kutuuzia muda si mrefu. kwa uzoefu, magari ya kijerumani huwa garama kuliko magari ya kijapan.

2. sehemu kuliko na magari ya nchi za ulaya, wajapan hupenda kuweka viwanda karibu nao kwaajili ya kushindana biashara.

3.hivyo, tz tuache siasa za kupoteza muda, tuweke mazingira mazuri kwa wawekezaji kuja kuwekeza na sisi tuunde magari hapahapa tuachane na kuumizwa pale bandarini tunapoagiza useds.

kwa kawaida, ili mwekezaji aje, lazima awe guaranteed mambo kadhaa. mambo mojawapo ni kwamba, anatakiwa kuhakikishiwa kwamba utawala wa sheria unafanya kazi, ili akigombana na wafanyakazi wake, akigombania ardhi anayowekezea/penye kiwanda, etc, ni mahakama pekee ndio itakayoamua, sio kiongozi mmoja atasimama na kusema mwekezaji ni mmoja wananchi wengi hivyo kumpunja maslahi bila kwenda mahakamani.

lazima tumhakikishie kuwa kutakuwa na umeme wa kutosha.

lazima tumhakikishie kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi viwandani wa kutosha, kuanzia wasomi na wasio wasomi. hapa vyuo vikuu, vyuo vya kati kama veta etc viimarishwe.

lazima ahakikishiwe kuwa atakuwa na urahisi wa kusafirisha magari yake kuuza nchi nyingine. tz tuna bahati, hapa ni kuboresha tu reli ya kati na reli ya tazara, hivyo tutakuwa na uwezo kuuza Rwanda (hata kama kutakuwa na volkswagen), zambia, burundi, congo na uganda etc.

kabla kenya hajaenda kuwakwapua toyota au honda tena, tuwawahi waje waweke kiwanda hapa tz.

ongezea mengine unayoyajua unayopenda kuisaidia serikali kimaendeleo.
 
Unajua unapoamua kufanya biashara lazima uangalie na wateja,kuweka kiwanda cha ku assemble magari maana yake ni kuwa gari inayotoka hapo ni mpya,sasa hebu chunguza ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kununua gari mpya?
 
Umenena mkuu
 
Tatizo mfumo. Haya yote tunayatamani ila hakuna wa kuyasimamia. Tuanze na viwanda vidogo vya kuprocess mazao ya wakulima kwanza.
 
Unajua unapoamua kufanya biashara lazima uangalie na wateja,kuweka kiwanda cha ku assemble magari maana yake ni kuwa gari inayotoka hapo ni mpya,sasa hebu chunguza ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kununua gari mpya?
mkuu, agiza gari yako japan, tufanye mfano rav4 used, hizi new model, hadi kufika hapa umeshatumia milioni 40. na watu wananunua kila siku. unafikiri watz hawatanunua magari ya mil. 40? na sio lazima kuassemble magari ya hadhi ya juu, hata hivyo hivyo vipanya kama volkswagen poli, golf etc bei zake ni za kawaida tu. kama watu wanaagiza gari japan, watashindwa kununua likiwa hapa?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom