Ferruccio Lamborghini
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 1,664
- 2,517
Kama una kawaida ya kwenda baa utakuwa unaelewa kuwa hiyo ndiyo sehemu hutokea mambo ya kushangaza zaidi ya sehemu yoyote ile. Nina uhakika ukiwa huko umewahi kushuhudia mzee mtu mzima akiwa amelewa chakari, amevua shati liko mabegani, anacheza wimbo wa ‘chizi karogwa tena’.
Lakini nakuhakikishia, katika mambo yote ya kushangaza niliyowahi kuyaona baa hakuna kitakachozidi siku nilipoona mwanamume ameletewa watoto wake baa na mke wake; nitakusimulia.
Mwanamume kuletewa mtoto sehemu isiyostahili sio jambo jipya kwangu. Nimewahi kuona mwanamume amepelekewa mtoto wake ofisini. Yaani jamaa alizaa na mwanamke ambaye hawaishi pamoja. Kumbe alikuwa na kawaida ya kupiga chenga kumhudumia. Siku hiyo yuko ofisini hana hili wala lile, mara anakuja kuambiwa kuna mgeni wako. Anashangaa mgeni wangu? Nani? Anakwenda mapokezi anamkuta mwanamke, mtoto wake wa miaka mitano na begi lenye nguo za mtoto. Mwanamke akamwambia “kama umeshindwa kumhudumia mtoto wako, nimekuletea umtafutie kazi ili ajihudumie.”
Lakini ya baa sikuwahi kuifikiria. Jamaa tuko naye hapa kila siku, tunakunywa naye, tunatazama mpira pamoja na wakati mwingine, hasa mwisho wa wiki tunamuacha hapa hapa.
Lakini kumbe jamaa nyumbani kwake ni kama sehemu ya kubadilishia nguo tu, yaani anarudi usiku mnene kutoka baa na anatoka majogoo kwenda kazini. Anarudi anakuta watoto wamelala, anaondoka hawajaamka.
Siku hiyo ilikuwa mwisho wa wiki, tulianza naye vizuri, tukanywa lakini mida mida tukaamua tubadilishe kijiwe, tukahamia baa nyingine. Basi mishale ya saa sita usiku hivi, hatuna hili wala lile tunashangaa mwanamke anakuja kwenye meza yetu akiwa na watoto wawili, mmoja mdogo wa miaka mitatu kambeba mwingine wa miaka sita anatembea mwenyewe.
Aisee, sijawahi kuona mwanamke kauzu kama huyo. Alipofika katusalimia tu, za saa hizi shemeji, kisha akamshusha mtoto aliyembeba huku anamwambia nenda kwa baba. Sasa jamaa yetu kabaki kaduwaa tu, haelewi nini kinaendelea, wala hajui afanye nini, ikabidi ampokee mtoto.
Basi ‘waifu’ wake akamwambia neno moja tu, ukirudi nyumbani utakuja nao. Jamaa ikabidi aulize ‘kulikoni mama Junio? Kuna tatizo gani?’
Akaambiwa wewe kila siku kurudi nyumbani unakuta watoto wamelala unaondoka hawajaamka, na sio kwamba upo bize na kazi, hapana, upo baa unapombeka. Muda kama huu ulitakiwa uwe nyumbani na familia yako. Mwisho watoto watakusahau, uje wakuite mjomba, kwa hiyo ili tusifike huko, nimekuletea watoto ukae nao hapa ili wasimsahau baba yao.
Alivyomaliza hotuba yake, akageuka, akaondoka zake. Basi mwenzetu ikabidi ainuke na watoto wake amfuate mke wake, na usiku huo hakurudi tena baa.
Ninachoweza kukwambia ni ile ilikuwa ni njia ya ajabu sana, lakini ilifanya kazi na inafaa kuwanyoosha baba wote wanaodhani jukumu lao ni kutoa pesa tu, sio kukaa karibu na familia zao.
©Mwananchi