Tuongee kiume: Kwanini mipango inayowekwa mwaka mpya haitimii?

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
Tunakwenda kumaliza mwaka, vipi nikikwambia kuna mahali sasa hivi yupo mwanaume mwenzetu anakula viapo, anajiambia mwakani naacha pombe, au naacha sigara, au naacha mambo ya wanawake, michepuko na nyumba dogo, au naacha mambo ya kufuatana na marafiki kama mtoto wa sekondari, au mwakani naacha hiki na kile.

Na vipi kama tukiamua kumkumbusha huyu mwanaume mwenzetu kwamba mwaka 2021 sio mwaka wake mpya, tangu amekuwa mwanaume ameshakutana na miaka mipya mingi na utamu zaidi ni kwamba karibu kila anapooanza mwaka mpya anafanya kama hiki anachofanya leo, anajiambia mambo mengi ambayo hataki kujiona akiyafanya mwakani lakini ikifika Disemba, akijifanyia uchunguzi hakuna alichokifanya.

Unajua kutamani kufanikisha jambo ni kitu kizuri sana, lakini mara zote wanaoweka malengo ya kufanikisha jambo kuanzia tarehe moja ya mwaka mpya hawajawahi kufanikiwa.

Unajua, watu tunajisahaulisha kwamba mfumo huu wa kalenda upo duniani kwa ajili ya kutufanya binadamu tuishi kibadamu, kimpangilio. Yaani tulipane mshahara kila mwisho wa mwezi, watoto wamalize muhula shule kila baada ya miezi sita na si vinginenvyo.

Kalenda haipo kwa ajili ya kutufanya watu wapya kila baada ya mwaka na kwa jinsi watu wengi tunavyoishi, ni wazi kwamba tunadhani kalenda ipo kwa ajili hiyo. Yaani tunaishi utadhani kwamba kama ulikuwa mlevi mbwa mwaka 2020, ukiingia tu mwaka 2021, basi utajikuta tabia yake ya ulevi haipo tena.

Na hii ni kweli, mimi nimeshawahi kuona mtu anasema, mwakani mimi naacha pombe, hiyo ikiwa ni tarehe 23, kisha ilipofika tarehe 25 sikukuu akagida ulabu kama hana akili nzuri. Nkamuuliza, vipi si ulisema unaacha pombe mwakani? Akasema ndiyo, nakunywa za mwisho mwisho — nikaishia kucheka tu.

Sina nia ya kurudishana nyuma, kuweka malengo ni jambo la msingi na linakuwa na raha zaidi ikiwa unaanza mwaka mpya ukiwa na malengo yako ya kufanikisha mwaka huo. Lakini hilo halihusiani chochote na kutimiza malengo yako. Yaani kama unataka kuachana na michepuko yako mwakani, lakini unashindwa kuachana nayo tarehe 27 ya mwezi Disemba eti kwa sababu mwaka mpya bado, basi ukweli ni kwamba una nafasi ndogo sana ya kufanikisha hilo lengo hata baada ya mwaka mpya kuanza.

Wazee, mwaka haubadilishi chochote kama wewe mwenyewe hujabadilika. Mwaka ni kalenda tu, ni namba tu, hazihusiani chochote na mabadiliko yako na malengo yako. Madiliko na mipango yako inahusiana zaidi na wewe mwenyewe. Na kama hutaki kuamini hili subiria tarehe mosi ya Januari mwaka 2021 uone kama utaanza mwaka ukiwa huna kitambi, huna madeni, huna michepuko au sio mlevi kama ulivyokuwa mwaka 2020.

Mwaka ni namba tu, nawatakia maandalizi mema ya kuuelekea mwisho wa mwaka.

©Mwananchi
 
Wengi tunapanga mipango mingi mizuri lkn hatuwazi namna ya kuitekeleza na kuifanikisha, tukiamini mwaka mpya huja na muujiza flani
 
Mara nyingi huwa tunaipanga huku tumeshalewa, si unajua wengi wetu badala ya kwenda kuupokea mwaka tukiwa Church kumshukuru Mungu na kumuomba kwa mwaka huu unaoanza na kwa mapenzi yake basi atupe uhai na afya ili tutimize yale tunayoyatamani, badala yake sisi tunaupokea tukiwa baa kwenye BIA TAMU, sasa hapo unategemea kuna mpango gani utafanikiwa
 
Mipango Mingi ni vichekesho 😂 Eti mwaka ujao nina mpango wa kununua Gari 😠

Ukitaka kuwini panga mambo utakayofanya, utakayoongeza au utakayopunguza ili ufanikishe lengo lako fulani.

So kama ni kuacha pombe basi usipange mwakani naacha pombe, bali panga kuacha mazingira yanayokufanya unywe. Kampani, bar, akili yako nk

Kama ni kununua Gari basi upange mwakani utakuwa unaweka Tsh 800,000 kila mwezi ili upate Million 8 kisha uagize gari.

So usiwe na illusions, uwe unapanga utafanya nini ili kupata nini.

So watu hawana Mipango au Malengo, bali ni WISHFUL THINKING tu 😂

Mpango wa kuacha pombe??? 🤣🤣🤣🤣
 
Tunakwenda kumaliza mwaka, vipi nikikwambia kuna mahali sasa hivi yupo mwanaume mwenzetu anakula viapo, anajiambia mwakani naacha pombe, au naacha sigara, au naacha mambo ya wanawake, michepuko na nyumba dogo, au naacha mambo ya kufuatana na marafiki kama mtoto wa sekondari, au mwakani naacha hiki na kile.

Na vipi kama tukiamua kumkumbusha huyu mwanaume mwenzetu kwamba mwaka 2021 sio mwaka wake mpya, tangu amekuwa mwanaume ameshakutana na miaka mipya mingi na utamu zaidi ni kwamba karibu kila anapooanza mwaka mpya anafanya kama hiki anachofanya leo, anajiambia mambo mengi ambayo hataki kujiona akiyafanya mwakani lakini ikifika Disemba, akijifanyia uchunguzi hakuna alichokifanya.

Unajua kutamani kufanikisha jambo ni kitu kizuri sana, lakini mara zote wanaoweka malengo ya kufanikisha jambo kuanzia tarehe moja ya mwaka mpya hawajawahi kufanikiwa.

Unajua, watu tunajisahaulisha kwamba mfumo huu wa kalenda upo duniani kwa ajili ya kutufanya binadamu tuishi kibadamu, kimpangilio. Yaani tulipane mshahara kila mwisho wa mwezi, watoto wamalize muhula shule kila baada ya miezi sita na si vinginenvyo.

Kalenda haipo kwa ajili ya kutufanya watu wapya kila baada ya mwaka na kwa jinsi watu wengi tunavyoishi, ni wazi kwamba tunadhani kalenda ipo kwa ajili hiyo. Yaani tunaishi utadhani kwamba kama ulikuwa mlevi mbwa mwaka 2020, ukiingia tu mwaka 2021, basi utajikuta tabia yake ya ulevi haipo tena.

Na hii ni kweli, mimi nimeshawahi kuona mtu anasema, mwakani mimi naacha pombe, hiyo ikiwa ni tarehe 23, kisha ilipofika tarehe 25 sikukuu akagida ulabu kama hana akili nzuri. Nkamuuliza, vipi si ulisema unaacha pombe mwakani? Akasema ndiyo, nakunywa za mwisho mwisho — nikaishia kucheka tu.

Sina nia ya kurudishana nyuma, kuweka malengo ni jambo la msingi na linakuwa na raha zaidi ikiwa unaanza mwaka mpya ukiwa na malengo yako ya kufanikisha mwaka huo. Lakini hilo halihusiani chochote na kutimiza malengo yako. Yaani kama unataka kuachana na michepuko yako mwakani, lakini unashindwa kuachana nayo tarehe 27 ya mwezi Disemba eti kwa sababu mwaka mpya bado, basi ukweli ni kwamba una nafasi ndogo sana ya kufanikisha hilo lengo hata baada ya mwaka mpya kuanza.

Wazee, mwaka haubadilishi chochote kama wewe mwenyewe hujabadilika. Mwaka ni kalenda tu, ni namba tu, hazihusiani chochote na mabadiliko yako na malengo yako. Madiliko na mipango yako inahusiana zaidi na wewe mwenyewe. Na kama hutaki kuamini hili subiria tarehe mosi ya Januari mwaka 2021 uone kama utaanza mwaka ukiwa huna kitambi, huna madeni, huna michepuko au sio mlevi kama ulivyokuwa mwaka 2020.

Mwaka ni namba tu, nawatakia maandalizi mema ya kuuelekea mwisho wa mwaka.

Mwananchi
Mipango sio matumizi
 
Back
Top Bottom