Tuongee asubuhi Startv : Mada: Athari za Siasa za Chuki na Visasi

Oct 9, 2016
96
250
Mwendesha kipindi amealika wazungumzaji wawili kila mmoja na mtazamo wake kuhusu siasa za Tanzania.

Anwar Saidi : Anazungumzia upepo wa siasa nchini.Amenukuu msemo wa Abraham Maslow : Ukiwa na nyundo kila tatizo unaliona msumari, amehusisha msemo huu na hatua mbalimbali za serikali za kuleta maadili kwa viongozi kwa hatua ya serikali ya kutumbua majipu bila ya kuangalia njia nyingine ya kinidhamu.Amegusia vilevile visasi na chuki za kisiasa za viongozi kwa watu wanaowapinga, ametoa mfano jinsi gani viongozi wanavyojaribu kunyamazisha wapinzani au watu wenye mawazo kinzani dhidi yao badala ya kufanyia kazi mawazo yao kwa mustakabali ya maendeleo ya watu.Mzungumzaji huyu ametoa mfano wa mataifa mbalimbali yaliyokuwa na hofu na wananchi wake kwa kuminya demokrasia.

Mzee Falijallah : Serikali hii ina uvumilivu wa hali ya juu wa kisiasa, mfano aliyekuwa kada wa CCM aliyehamia CHADEMA alipokuwa na nyadhifa mbalimbali CCM amevurunda sana badala yake amekuwa anasema hovyo kuhusu serikali hata hivyo anavumiliwa.Ameipongeza serikali ya awamu ya tano jinsi inavyopigania maisha ya Watanzania maskini kwa kuleta uadilifu serikalini na kuwawezesha kiuchumi, ametoa mfano hatua ya rais Magufuli kuruhusu wachimbaji wadogo wa dhahabu kuchimba dhahabu mgodi wa Kahama.Vilevile ameipongeza hatua ya Waziri Mkuu kuhamia Dodoma kama mji mkuu wa Tanzania.

Kipindi kinaendelea mengi yanajadiliwa.
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
50,953
2,000
Hio mada ni nzuri ila sidhani kama wataitendea haki,
Kwa woga huu watabaki kusifia sifia tu basi.
Mzee wa mijisifa hataki kupingwa
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,814
2,000
Mwendesha kipindi amealika wazungumzaji wawili kila mmoja na mtazamo wake kuhusu siasa za Tanzania.

Anwar Saidi : Anazungumzia upepo wa siasa nchini.Amenukuu msemo wa Abraham Maslow : Ukiwa na nyundo kila tatizo unaliona msumari, amehusisha msemo huu na hatua mbalimbali za serikali za kuleta maadili kwa viongozi kwa hatua ya serikali ya kutumbua majipu bila ya kuangalia njia nyingine ya kinidhamu.Amegusia vilevile visasi na chuki za kisiasa za viongozi kwa watu wanaowapinga, ametoa mfano jinsi gani viongozi wanavyojaribu kunyamazisha wapinzani au watu wenye mawazo kinzani dhidi yao badala ya kufanyia kazi mawazo yao kwa mustakabali ya maendeleo ya watu.Mzungumzaji huyu ametoa mfano wa mataifa mbalimbali yaliyokuwa na hofu na wananchi wake kwa kuminya demokrasia.

Mzee Falijallah : Serikali hii ina uvumilivu wa hali ya juu wa kisiasa, mfano aliyekuwa kada wa CCM aliyehamia CHADEMA alipokuwa na nyadhifa mbalimbali CCM amevurunda sana badala yake amekuwa anasema hovyo kuhusu serikali hata hivyo anavumiliwa.Ameipongeza serikali ya awamu ya tano jinsi inavyopigania maisha ya Watanzania maskini kwa kuleta uadilifu serikalini na kuwawezesha kiuchumi, ametoa mfano hatua ya rais Magufuli kuruhusu wachimbaji wadogo wa dhahabu kuchimba dhahabu mgodi wa Kahama.Vilevile ameipongeza hatua ya Waziri Mkuu kuhamia Dodoma kama mji mkuu wa Tanzania.

Kipindi kinaendelea mengi yanajadiliwa.
Fallijallah muulize
NHC inamdai Mbowe peke yake?
Muulize mwenye mashamba yasiyoendelezwa ni Lowasa na Sumaye peke yao?
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,634
2,000
Huyo mzee Farijala anatembea mlemle kwenye siasa za kinafiki kwamba wapinzani ndio tatizo la nchi. Kwa mtazamo wake viongozi ni watu wa kunyenyekewa tu na hata wanapokosea wanatakiwa kuambiwa kwa kubembelezwa. Huyu mzee ni wale wanaomini serekali ni kitu kitukufu hivyo haikosei bali inakosewa. Huyo mzee ndio walioifikisha nchi hapa ilipo, kosa lonatendwa na.viongozi lakini tuachane naye kwani ni mwenzetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom