Tuongee asubuhi star tv(live):mada ni maandamano ya chadema.

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Wadau ebu tufuatilie tuone kitakachozungumzwa.,ni kuanzia saa moja na nusu asubuh hii.
 
Kwa mtazamo wa wazunguzaji wote chadema iku juu kwa kuwa wote wapo pamoja na chadema.
 
Huyu mtangazaji inaonekana anamuogopa sana huyu grayson nyakarungu kwa kuwa anamkatisha sana.
 
Bahati mbaya wanafunzi wa vyuo vikuu wanafanya mitihani hivyo post mtaziona chache. Tawi la chadema la JF mtaliona limepwata hadi wamalize likizo.
 
Bahati mbaya wanafunzi wa vyuo vikuu wanafanya mitihani hivyo post mtaziona chache. Tawi la chadema la JF mtaliona limepwata hadi wamalize likizo.

du mkuu kama kweli ivi,naona post chache. Vp si kwamba wengi wako kwenye maofisi sa izi. Unajua pilika za kwenda kazini na zile morning briefing ndo zimewaweka watu bize!?
 
Bashiru amekua mnafiki matokeo yake kaishia kujichanganya, huyu mtangazaji wa mwanza bogus kabisa kujikomba ndio yule aliyeshushuliwa na Slaa wakati wa kampeni. Grayson amenyanyaswa sana na mtangazaji lakini kila alipotoa ni bomu, scud kwa kwenda mbele, huyu lawyer ndio kabisa kamaliza na kuua kishenzi na nimefurahi hakuwa intimidated na kupambanishwa na mwalimu wake, nasikitika Mnyika hakuhudhuria studio ya Dar maana anngemtengeneza Bashiru kama mshikaki, Abbass Mwinyi my foot, hana ubavu hao ndio wale wale the likes of watoto wa Gadafi
 
Huyu mtangazaji nilimdharau tangu ile siku alipoharibu interview yake na Dr.Slaa.Yahya upo wapi?Irudisheni ile star tv ya mijadala motomoto kama kipindi kile cha mgogoro wa kambi ya upinzani bungeni.
 
Paul mabuga mtangazaji wa star tv ni mtangazaji kilaza kuliko wote hapa nchini. Hajui kuendesha mijadala kwa sababu anaegemea upande mmoja unaounga mkono serikali, pia anawakatishakatisha wazungumzaji na kuchelewa kuruhusu simu. Simpendi. Bora vipindi viendeshwe na mkongwe samadu hassan, rymond nyamwihula au yahya mohamed, they are very smart.
 
Nina kiu ya kujua ni nini kimejiri huko, waungwana mwamweza kutudokeza hata kidogo au ni lini wanafanya marudio.
Elimu ambayo haijamfanya mtu kuwa mkweli ni sumu kwa mhusika na mtu mwenyewe ni janga kwa taifa. Kama hilo ndilo limedhihirishwa na baadhi ya washiriki basi tunahitaji rehema ndani ya taifa hili.
 
Back
Top Bottom