tuongee asubuhi,mijadala bungeni;kielelezo cha kukomaa kwa demokrasia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tuongee asubuhi,mijadala bungeni;kielelezo cha kukomaa kwa demokrasia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, Jul 15, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wadau mjadala umeanza star tv,karibuni tulidadavue bunge la sasa na changamoto zake.
   
 2. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Bunge letu limepoteza uelekeo kutokana na udhaifu wa kiti (spika, naibu spika na wenyeviti) ambao wapo kulinda masilahi ya serikali na sio heshima na wajibu wa bunge kwa watanzania. Kiti kimepya sana.
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tumekuwa na bunge linaloongozwa na sheria na kanuni za bunge la chama kimoja na madhara yake ni zaidi ya haya tunayoyaona,labda serikali iwe makini na isiwe na changamoto nyingi sana.
  bunge kuongozwa na mtu aliyeapa kuilinda serikali kwa lolote na hapohapo aongoze wabunge wa upinzani kuikosoa na wakati mwingine asimamie kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu hivi ni vichekesho.
   
 4. J

  JAPHETtumpa Senior Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Vingozi wa bunge wanadhani wanatetea chama chao kwa kuonyesha upendeleo wa wazi ama kwa kutumia kanuni sahihi za bunge au kwa kutumia mamlaka walio nayo.
  job ndugai atuambie inakuwaje anafurahia lugha za kuudhi zinazotolewa wabunge wa chama fulani kiasi cha kuomba neno husika lirudiwe wakati huohuo akionyesha kuudhika kwa haraka na lugha za wapinzani na inakuwaje kiongozi kumuita mbunge wa jimbo fulani kituko au kiongozi kutumia maneno tuliozoa kuyasikia mtaani kama kuwashwawashwa. ebu job ndugai atuambie lakini aelewe tunawafuatilia na mahakama yao ni 2015
   
 5. T

  Tanganyika2 Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarajio letu wabunge wajikite kuelezea taarifa za CPW juu ya utendaji wa viongozi wa Bunge kwa vigezo vilivyoainishwa. Kuwatambua au kutowatambua CPW si jukumu la wabunge au waziri, vipo vyombo kwa ajili hiyo, na hiyo haina tija kwenye taarifa zao. Sababu anazotoa Naibu Spika Ndugai kukwepa matokeo haya si sahihi: kwani Mwalimu ni lazima awe bora kuliko mwanafunzi, mbona wanafunzi wanafaulu kwenda vyuo vikuu huku walimu wao wakifeli mitihani iyo hiyo? Je yeye kwa mtazamo wake anakili kuwa hata matokeo yaliyopatikana kuonesha udhaifu wa uongozi? Tusaidie Yahaya ajibu maswali haya.NDUGAI ANASEMAJE JUU YA AINISHO LA TAARIFA HIYO KUWA KANUNI ZA 46 NA 55 NDIZO ZILIZOVUNJWA/KIUKWA SANA???
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mh ndugai ongelea kanuni za bunge acha kuingilia mhimili mwingine kila mhimili una kanuni zake.
   
 7. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Job Ndugai anawadjalilisha maofisa wa usalama kuwa hawawezi kuandika, maana siyo kama wananchi wa kawaida inasikitisha sana. Naomba viongozi bungeni tenda haki inayostahili maana wote mnatuwakilisha wananchi. Magazeti yanaletwa bungeni mbona Anna Kilango ameleta Nipashe juzi?
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mh ndugai naomba uachane na mahakama,hata mahakama haziwezi kutumia sheria za mahakama za kenya japo ni zote ni sheria.
   
Loading...