Tuone uzalendo wa wale tunaodhani ni waadilifu CCM; Sitta, Magufuli na wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuone uzalendo wa wale tunaodhani ni waadilifu CCM; Sitta, Magufuli na wengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Thesi, Nov 19, 2011.

 1. T

  Thesi JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wana JF,
  Kumekuwa na watu wanaodhani baadhi ya viongozi CCM ni waadilifu na wapiganaji wa maslahi ya wananchi. Watu wengine wamefikia hatua ya kuwaita wanaowakosoa hao malaika wao wa CCM kuwa ni watu wanaotumiwa na mafisadi kuwadhoofisha.
  Tunaotaka ukweli usichanganywe na kitu chochote tunawaona watu kama Samwel Sita, Maghufuli na wengine kuwa si lolote si chochote au ni lolote lakini hawajafikia viwango vya kuitwa wapiganaji. Hawawezi kujibandua CCM kwani wanapenda maslahi wanayopata huko kuliko kuwatumikia wananchi kwa kukemea maovu. Yaani ni watu wanaouma na kupuliza. Uoga umewatawala na hawawezi kufanya jambo lolote linalohatarisha ulaji wa cha chao CCM kwani na wenyewe wanakula humo ndani.

  Jana bunge limepitisha muswada wa katiba mpya unaompa Rais na watumishi wa serikali mamlaka ya kuhodhi namna mchakato huo utakavoendeshwa kupata katiba mpya. Hili si jambo zuri hata kidogo kwani tunajua fika kuwa serikali wala CCM hawajawahi hata cku moja kuota ndoto ya kutunga katiba mpya itakayoboresha maslahi ya nchi yetu, kulinda haki za raia na kuweka msingi mzuri wa maendeleo yetu kwa miaka mingi inayokuja. Hivo CCM kutaka kuchukua mchakato wa katiba kuuongoza ni makusudio ya kutaka kupindisha mchakato kuleta ndicho sicho katiba kulinda maslahi yake kukaa madarakani na kuendeleza ufisadi kama kawa.

  Kwa mantiki hiyo kama Sita, Maghufuli na wengine wanaotaka tuamini ni watetezi wa maslahi ya nchi tunataka kuona uzalendo wenu kwa kupinga Muswada uliopitishwa na bunge la CCM. Tunataka kuwaona mkiungana na wanachi wazalendo, vyama vya kiraia, wanaharakati na mashirika ya dini kupinga ubabe huu wa CCM. Vinginevo ile imani yetu kuwa Sita, Maghufuli na wale wanaotaka tuamini kuwa ni wapiganaji wetu WANAFIKI, lao na mafisadi ni moja tu ila wanagombana tu kwa kuwa mafisadi wamewazidia ujanja kula minofu.
   
 2. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  absolutely...
   
 3. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Wataanzia wapi? Muulize kilichomkuta dr. Mwakyembe
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hata kama wangekuwa na afadhali, sijawahi kuwachukulia hao watu kuwa ni wapiganaji wala sitakaa nimchukulie kiongozi yeyote ndani ya ccm kuwa mpiganaji. Maovu ya ccm kwa taifa hili yanatosha kumfanya mtu yeyote mwenye akili timamu kujiondoa huko mara moja.
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  exactly mkuu. AMAUTI
   
 6. T

  Thesi JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni kweli tatizo ni jinsi wengi wetu tunavoweza kuhadaiwa na hawa wanafiki kina Sita. Kuna watu humu JF ukimgusa Maghufuli au Sita ni kwamba umetumwa na mafisadi wanaogombea mnofu. CCM imeoza na ukiwa mwadilifu huwezi kukaa humo na kuanza kukemea wezi waliomo. Ukiwa si mnafiki kemea CCM manake ndio mfumo unaolea ufisadi. Kusema mtu fulani ndani ya CCM
  ni fisadi hakutoshi. Sita, Maghufuli na wengine ni watu wanaotaka kupata umaarufu kwa kujifanya wanatetea haki wakati ni wezi kama wezi wengine make wako kwenye chama cha wezi.
   
Loading...