Tuombe Msaada wa Uchunguzi wa Kimataifa.....

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,958
718
Naamini umefika wakati watanzania tukaacha kuomba omba misaada ya fedha kutoka mataifa ya kigeni kukidhi bajeti yetu na badala yake tuombe misaada ya Uchunguzi wa Kimataifa dhidi ya mafisadi wote walioko ndani au nje ya serikali hata wale walioko nje ya nchi. Wengine wataniona mie mwendawazimu kuleta hii hoja hapa barazani lakini UKWELI DAIMA husimama. Ukijaribu kufuatialia kwa karibu utaona nchi yetu inaweza kujitosheleza katika bajeti yake bila kuwa ombaomba. Kwa nini nasema hivyo, tangu uzuke mjadala wa mafisadi, tumeona na kusikia mengi yakisemwa about EPA, TANGOLDS, MEREMETA, DOWANS na upumbavu wote ili mradi pesa yetu imekwapuliwa.
Mafisadi walioguswa na Mradi wa Meremeta/Tangolds wanadai hayo makampuni ni mali ya serikali, TANGOLDS ikirithi madeni ya Meremeta. Savings za TANGOLDS ni kama ifuatavyo:
1. Foreign account: US $. 12,997,950.84 (TShs. 16,365,672,850)
2. Local saving: Tshs. 1, 379,359,367.39.

Sasa hiyo ni akaunti ya kampuni ya serikali ambayo inalialia kuwa bajeti haitoshi. This is Bullcraps, una bilioni 18 wananchi wako wanakosa umeme huko Kigoma na sehemu zingine za nchi. Jamani kama hii si longolongo ni nini?? Rais Kikwete anatakiwa aulizwe maswali hapa ni kwa nini wananchi wanapata shida kama huko Buhemba na sehemu zingine wakati kuna fedha ambazo wana rights ya kupata huduma muhimu from that CASH? Na wala Kikwete hasije akaja na ushahidi wa kusema alikuwa hajui kama kuna hiyo fedha. Ninajua taratibu za kukabidhiana ofisi pindi ofisa particulary Rais anapochaguliwa kuchukuwa madaraka kutoka kwa anayemaliza muda wake. Na Kikwete anajua wazi kabisa ni kwa nini anamkumbatia Chenge, Mkapa, Rostam, Mgonja na wengine weeeeeeeeeeeeeeengi ambao sikuwataja hapa. Anajua siri ya kukenua kwake meno huku wenzake wanafukia korogesheni.

Hakuna cha uchunguzi hapo ni danganya toto. Hakuna cha TAKUKURU wala TAKO KUU, wote wanapaswa kuchunguzwa. Sasa wewe unafikiri huyo IGP anaweza kumuangusha shemeji yake? Mmmh akose Mseregeso, nani kakwambia hilo. Hosea na TAKOKUU si naye anachunguzwa kuhusu Bangaluu, na huyo Mwanyika naye si alikuwa msaidizi wa Chenge au mie nakosea. Usalama wa Taifa ni utumbo mtupu, hayo yote walikuwa wanajua, mtu hawezi ku-transfer pesa kama hiyo kwenda out of Country bila BOT na Usalama wa Taifa kujua. Yaani uongozi wote umeoza, nafikiri uitishwe uchaguzi mwingine maana hiyo pesa iliyoko kwenye akaunti ya TANGOLD inaweza kulipia process za chaguzi.
Na sasa mnamuajiri Nicholas Mkapa kuwa Mwanasheria wa serikali eti kanda ya Dar es salaam. Hivi kweli wee Mwanyika akili yako ina akili kweli? Najua ni haki ya kila mtanzania kuajiri na kuajiriwa ndani ya nchi yake. Lakini hapa tuangalie mgongano wa kimaslahi, Kwa nini msimpeleke huko kwao Nanyumbu huko nako si kuna ofisi ya Mwanasheria. Kanda ya Dar es salaam ina nini???? Au ndo apunguze na kuingilia uchunguzi unaomhusu baba yake kwa njia moja au nyingine. JK acheni masihara na fanyeni ambacho wananchi waliwaagiza. Huu usanii wa kuajiri mtoto wa Mkapa kwenye taasisi inayomchunguza baba yake si ukosefu wa Busara tu bali inaonyesha Serikali kwa sasa iko ICU na kwa msemo wa MWK "INCAPACITATED" maana haioni kuwa hapo INATOKOTA.

Kwa kuanisha hayo mie nilikuwa nafikiria ni busara sasa tuache kuwa ombaomba wa fedha za bajeti na sasa tuwe ombaomba wa Uchunguzi wa Kimataifa kutoka kwenye taasisi ambazo zinaweza kutusadia sisi watanzania ku-locate pesa zetu huko overseas. Kuna kama hayo mashirika SFO, FBI, Interpol na mengineyo. Naamini hata hao wafadhili na uchungu na pesa za wavuja jasho nchini mwao. Hivyo naamini wanaweza kutusaidia kuokoa pesa zetu ili ziwatumikie watanzania wote na si ukoo au familia fulani.
Mie binafsi nitaanza ku-solicit barua kwenda kwenye taasisi za uchunguzi na hata vyombo vya habari. siko hapa kumfurahisha mwana baraza au msomaji yeyote bali niko serious na hili. Litakalokuwa na liwe as long as ninatetea maslahi ya wananchi wenzangu.

MUNGU IBARIKI JAMBO FORUMS.
 
Huko hela zilipo ni vigumu sana kukubali kuzionyesha kwani wakionyesha zitarudisha na wao wanakuwa wamekosa foreign currencies
 
Back
Top Bottom